bado sijaelewa mwananchi anazurumiwa vipi? yaani kuna hasara gani kwa mwanachama maana naona maelezo tu kwamba DECI haifai kivipi?
Kuna thread nyingine inayoongelea hili. Katika thread hiyo Mwanakijiji ameeleza vizuri, lakini pia kuna michango mingi mizuri.
Nenda kwenye link hii:
DECI DECI.
Cha muhimu ni MSINGI wa mchezo huu.
Unapoweka fedha Benki, Benki wanazalisha pesa hiyo kwa miradi inayofahamika, na benki wanatutangazia ripoti zao za fedha waziwazi hadharani. Benki wanaweza kukopesha watu kwa riba kubwa kuliko wanazolipa wateja wa akaunti za akiba. Lakini pia Benki wana vitega uchumi ambavyo huzalisha fedha wanazopokea toka kwa wateja. Hii ndio hulipa faida wateja. Lakini faida hiyo mara nyingi haizidi asilimia 10 kutokana na hali halisi za kibiashara.
Lakini Schemes kama za DECI, hakuna uzalishaji wowote unaofanyika kwa fedha zinazokusanywa. Wanachofanya ni kupata wanachama wapya, na fedha za wanachama wapya ndizo wewe uliyepanda zamani unavuna. Sasa mwendelezo wa mchezo huu unategemea kupata wanachama zaidi ili uendelee kulipa faida.
Lakini kadri scheme inavyopata wateja zaidi, ndio jinsi inavyoelemewa na kuwajibika kupata fedha ambayo hawa wapya watavuna. Hatima ya scheme hii ni kuelemewa na kushindwa, ikiwa inadaiwa mamilioni ya pesa na "wawekezaji" wa scheme hiyo.
Charles Ponzi alianzisha scheme hii USA mwaka 1920, ikapata watu wengi sana. Lakini baadaye alishindwa kuwalipa wapya na akakamatwa na kufunguliwa mashtaka tarehe 12/8/1920.
Hivi sasa kama unasikiliza BBC au CNN yuko Bernard Madoff ambaye alijikusanyia mabilioni ya dola kwa mfumo kama huo, na sasa mwenyewe anakiri kuwa ni wa udanganyifu. Watu wengi wamepoteza mamilioni katika mfumo huo wa Madoff ambao msingi wake ni kama wa Ponzi.
Soma hapa kwa maelezo zaidi
link Ponzi