unajua sijui ni ushama au upungufu wa akili kwa kweli kama hawa DECI wangekuwa na la maana wanalofanya kungekuwa na faida inayoonekana, ila kwa akili zetu fupi za madafu hatukuangalia kama wanafanyia nini hizo pesa, eti jamani huenda uchumi wangu ni wa vidudu maana kwa nijuavyo mimi hamna biashara ya faida zaidi ya asilimia mia ndani ya muda mchache jamani lazima kuna michango mengine itakayofanya returns ziwe kidogo chache au naongopa, haya wabongo ambao tunajidai ni risk takers hilo limebumburuka kama maji ya kunawa, na halijaanza hili nakumbuka kuna kipindi pia kulikuwa na fomu zinatandazwa eti ukiweka elfu hamsini halafu baada ya muda unapata mafao mengi ikawaliza wanafunzi wengi wa UDSM ila bado hatujifunzi tuu. sijui na mimi nije na wazo langu mbona kilamtu anavuna jamani?