Lowasa atarudi madarakani muda si mrefu na anategemewa kuchukua uraisi hapo baadaye.
Kumbukeni Mwalimu Nyerere aliwakataa Kikwete na Lowasa kugombea nafasi hizo kubwa. Hawa jamaa kwa pamoja waliamua kung'ang'ania na kusaidiana kwa hali na mali hadi wakapata nafasi hizo kwa makubaliano ya kuachiana kiti cha uraisi. Hivyo Lowasa anajua kabisa kwamba ni lazima arudi madarakani haraka kadri iwezekanavyo ili iwe rahisi kwake kuwa raisi wa Tanzania.
Alichokuwa anafanya Lowasa katika nafasi ya uwaziri mkuu ni kukusanya pesa kwa kila namna ambazo zingemsaidia katika kampeni yake ya kwenda ikulu. Huo mradi wa Richmond ilikuwa ni moja kati ya njia za kukusanya pesa. Alikuwa ana mipango kabambe kabisa ya kuuza Bandari ili kukusanya pesa za kampeni.
Pamoja na makelele yetu yote bado Lowasa atarudi serikalini na kuchukua madaraka makubwa katika nchi hii.
Tanzania inamilikiwa na watu wachache sana na Lowasa ni moja kati yao.