DED Makete Awahakikishia Wakulima wa Ngano Soko la Uhakika

DED Makete Awahakikishia Wakulima wa Ngano Soko la Uhakika

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

DED MAKETE AWAHAKIKISHIA WAKULIMA WA NGANO SOKO LA UHAKIKA

Halmashauri ya Wilaya ya Makete Julai 23, 2024, imesafirisha Tani 32, za Ngano, ikiwa ni awamu ya Pili ya Ununuzi wa Ngano baada ya hapo awali kusafirisha kiasi cha Tani 30, ambazo zote zimenunuliwa na Kampuni ya Bakhresa iliyopo Buguruni Jijini Dar es Salaam.

Ngano hiyo, ambayo Imesafirishwa kuelekea Mkoani Dar es Salaam, Ina thamani ya Shilingi Millioni 32, ambapo kilo Moja imekuwa ikiuzwa kwa shilingi elfu 1000, ikiwa ni Fedha za wakulima ambao wamekuwa wakilima zao hilo, kutokana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amegawa bure kwa Wakulima kupitia Kampuni ya ASA.

Ikumbukwe kuwa Julai 13, 2024, Wakulima wa zao la Ngano Wilayani Makete, walishauriwa kutumia Mashine bora za kisasa katika Uvunaji wa zao hilo, ambapo msimu wa Uvunaji umeshanza rasmi katika baadhi ya Maeneo ikiwemo kijiji Cha Mlengu kilichopo Kata ya Kigala.

Ushauri huo, ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Juma S. Sweda, akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, wakati wa Ukaguzi wa Uvunaji wa zao hilo katika Shamba la ekari 300, lililopo Kijiji Cha Mlengu Kata ya Kigala, Wilayani Makete.

Aidha, akizungumza Ofisini kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. William M. Makufwe, amewataka Wakulima kuendelea kukusanya Ngano katika Vituo vilivyoainishwa kwenye maeneo yao, kwakuwa soko la Ngano ni la Uhakika kupitia Kampuni ya Bakhresa iliyopo jijini Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano ya Serikali,
Halmashauri ya Wilaya ya Makete.
23/07/2024
 

Attachments

  • Screenshot 2024-07-24 at 14-17-05 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    Screenshot 2024-07-24 at 14-17-05 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    808.6 KB · Views: 3
  • Screenshot 2024-07-24 at 14-16-51 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    Screenshot 2024-07-24 at 14-16-51 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    748.4 KB · Views: 6
  • Screenshot 2024-07-24 at 14-16-37 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    Screenshot 2024-07-24 at 14-16-37 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    860.5 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-07-24 at 14-16-24 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    Screenshot 2024-07-24 at 14-16-24 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    792 KB · Views: 4
  • Screenshot 2024-07-24 at 14-16-09 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    Screenshot 2024-07-24 at 14-16-09 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    945.8 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-07-24 at 14-15-54 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    Screenshot 2024-07-24 at 14-15-54 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    817 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-07-24 at 14-15-39 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    Screenshot 2024-07-24 at 14-15-39 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    836.5 KB · Views: 4
  • Screenshot 2024-07-24 at 14-15-26 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    Screenshot 2024-07-24 at 14-15-26 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    891.5 KB · Views: 3
  • Screenshot 2024-07-24 at 14-14-57 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    Screenshot 2024-07-24 at 14-14-57 Makete Dc Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo Julai 23 2024 ...png
    1 MB · Views: 6
Back
Top Bottom