KERO DED wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga hatulii ofisini na hakaimishi majukumu, tunasota kupata huduma yake

KERO DED wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga hatulii ofisini na hakaimishi majukumu, tunasota kupata huduma yake

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Wananchi na Watumishi tunapata changamoto sana hasa tunapohitaji huduma ya Mkurugenzi (DED), zinaweza pita siku 5 hupati huduma unaambiwa hayupo na hajakaimisha mtu.

Kinachokera zaidi ni kuwa Halmashauri ni mbali kiasi kwamba hizo siku zote unaweza tumia zaidi ya Tsh. 70,000 kufuatilia huduma na hufanikiwi, tunaomba jambo hili liwafikie mabosi wake maana imekuwa 'too much', tangu mwezi Februari 2026 hali imekuwa hiyohivyo.

Nimeshuhudia hata Wazabuni pia wanapata changamoto ya kusainiwa hundi zao, nimeona wanateseka hata wiki wiki mbili kufuatilia, wanaambiwa watia sahihi wa hundi hawapo, hii sio sawa kabisa, wabadilike.
 
Matatizo yako hana muda nayo, yeye salary na posho vinaingia kama kawa.... na hakuna chenye utamfanya
 
Bora uyo ss alie mteua kila mara kiguu n njia unaambiwa. Poleni
Kazi ni kipimo cha utu
 
Kwa wakuu wa idara majukumu yao ni yapi hadi nyie mnaona lazima mkutane na DED mwenyewe?
 
Back
Top Bottom