mkweliwatz
Member
- Dec 6, 2025
- 8
- 11
Hapa kwetu Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya DC), Mkurugenzi Mtendaji wetu, Erica Yegella ana changamoto kadhaa kuhusu matumizi ya ofisi yake:
1. Hakufanya kikao na Baraza la Wafanyakazi kabla ya Bajeti
Kila mwanzoni mwa mwaka kunatakiwa kufanyike Baraza la Wafanyakazi kwaajili ya kupitisha Bajeti ya Halmashauri lakini cha kusikitisha mkurugenzi huyu kwa makusudi ameamua kutofanya hilo Baraza.
2. Hana ushirikiano na Baraza la Wafanyakazi
Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wamejitahidi sana kuwasiliana naye lakini hakuwapa ushirikiano.
3. Hatulii ofisini kufanya majukumu yake
Mara nyingi hakai ofisini, ni mtu wa kusafiri sana kwa mambo yake binafsi, baada ya viongozi wa vyama kutumia baadhi ya viongozi wengine kumshawishi akutane nao ndipo akawaamuru wasaidizi wake waitishe kikao cha Baraza la Wafanyakazi Machi tarehe 16, 2026 ambapo bajeti zote za halmashauri zilishapelekwa Dodoma Bungeni.
Baraza hilo batili lilipoitishwa viongozi wa vyama walikutana na wasaidizi wake kabla ya kuingia kwenye kikao ili kuwekana sawa sababu zilizowafanya kutoitisha Baraza la Wafanyakazi kwa mujibu wa ratiba za miongozo, baada ya maelezo ya Kaimu Mkurugenzi viongozi wa vyama hawakuridhishwa na sababu zilizotolewa, hivyo kwa kauli moja waliamua kutoshiriki hilo baraza batili na kuondoka.4.
Hivyo, kikao hakikufanyika siku hiyo na kuwaomba wasaidizi hao kuwa wanataka kikao na Mkurugenzi Bi. Erica Yegella, Wasaidizi hao walitoa ushirikiano mzuri na kuahidi kuwa tarehe 23/03/2026 watatupatia majibu baada ya wao kuongea na mkurugenzi huko alipo.
4. Dharau kwa Watumishi
Kweli ilipofika tarehe hiyo walitoa majibu kuwa Mkurugenzi amesema akirudi ataitisha kikao na viongozi hao… lakini kwa dharau za Mkurugenzi alirudi na hakuitisha kikao hicho kama alivyoahidi, mpaka 27/04/2026 hakuna kinachoendelea.
Kazi mojawapo ya Baraza la Wafanyakazi ni kufuatilia stahiki za Watumishi kama zimeandaliwa kwa mujibu wa miongozo na zinakidhi mahitaji lakini pia kushauri uongozi kwenye masuala mbalimbali ya watumishi.
Hivyo, viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wanasikitika sana kuwa hata baada ya viongozi wa mkoa kujulishwa changamoto hii hakuna hatua zozote walizochukua na kwa huzuni kubwa bajeti iliyopelekwa bungeni Dodoma ni batili kwa kuwa haijapitishwa na Vyama vya Wafanyakazi kama sheria inavyotaka.
5. Manyanyaso kwa Watumishi
Vilevile, Mkurugenzi huyu amekuwa akiwanyanyasa sana watumishi wa pale halmashauri na wanamuogopa sana kwa kuwa alishajinasibu kuwa yeye ana watu wakubwa Serikalini wanamlinda, hivyo hawezi kuguswa na mtu.😭😭
6. Ujumbe ufike kwa Rais na Waziri Mkuu
Naomba ujumbe huu umfikie Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Dr Mwigulu Nchemba watambue watumishi wao tunachopitia.
Tunataka mamlaka inayomteua ijue kuwa huyu Mkurugenzi hatufai Mbeya DC na kwa kuwa tunaelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani tunaomba tuwasilishe kero hii kwa afya ya Watumishi wote wa Mbeya DC.
Alipotafutwa Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya DC), Yerica Yegella kuhusu madai hayo, amejibu:
Hiyo changamoto ya Baraza haipo, hakuna kitu kama hicho, huyo aliyeandika ni muongo. Mkutano wa Baraza umefanyika, hizo shutuma dhidi yangu nazikataa, sina ugomvi wowote na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi, wananitungia tu taarifa ambazo hazina ukweli.

===================================