DEGREE MOJA YA ENGINEERING Medine n law

ni kweli kila fani ina umuhimu wake ila kwa waliosoma hizo tatu tajwa wanatoil sana na ni kweli ni ngumu huo ndo ukweli! swala la kufanikiwa ktk maisha ni ishu nyingine!
 

taaluma yoyote ambayo haina mitihani ya bodi au masomo ya ziada baada ya kumaliza shahada ya kwanza hiyo ni rahisi sanaa mfano
lawyers wana school of law engineers wana erb ,accountant wana cpa ,madaktari ukimaliza shahada ya kwanza unawekwa chini ya daktari bingwa je sociology, hr wanahuo utaratibu?
 
wewe ndo mbulula unayesoma socilogy

Nashidwa kushindana na wewe, kwamaana kupitia huu uzi wako nimegundua una uwezo mdogo mno wa kufikiri, yaaani labda chini ya megabyte 5. Kwa taarifa yako nimesoma Bsc. Computer science, Msc. Finance $ Investment na MBA plus CPA (T).
Jifunze kuheshimu taaluma za wenzako, au we ndo wale wa 60s% wa mwaka huu?
 

hata kama umeishia lasaba hautasema
 
absolutely umeonyesha intellectual immaturity yako. dunia hii ina division of labour since then! kweli hajitambui huyo!! asamehewe na kuelekezwa kwa upole!! maisha si kozi ulosoma,ni utafutaji wako tuu!
 
Mtoa mada yaonyesha ni mwanafunzi bado. Sera za kishule zinaonyesha hivyo hujakosea. Isipokua unapaswa kujua hakuna professional inayoweza kujiendesha yenyewe. Mfano mimi ni Mhandisi Civil Engineer (Structural Engineer and Geotechnical Engineer) lakini siwezi kuendesha shughuli za kiahandisi bila managerial skills. Utakuwa mzuri kwenye technical aspects lakini hutaweza kuongoza watu. Mfano mwingine,kama utaweza kufikia Senior position ni lazima uwe na uelewa wa human resource na hawa ndiyo wanaoangalia maadili ya wafanyakazi kwenye maeneo ya kazi. Naeleza haya kwa kuwa nimeyasoma na ninaelewa. Pamoja na human resource na management nyingine na uhandisi ama udaktari ndio unafanya shirika ama kampuni kukua. kampuni nyingi za hapa kwetu hasa za wataalamu (technologia ulizotaja) hazina watu wa Human resource,hivyo ukuaji wake unakua hafifu sana maana hawajui principles of employment/motivation/leadership nk ambazo ndizo key for company growth. Baada ya kusema hayo sina shaka utajirudisha nyuma na kutafakari maelezo yako
 
Mdogo wangu ukikuwa utakuja kugundua haukutumia werevu kabisa tangu kuanzisha hii Thread na wala unavyochangia.

Pamoja na kwamba nilisoma science tena PCB Alevel ila kwa kuwa shule niliyosoma O level ilikuwa ni ya biashara ilinilazimu kusoma Commerce mpaka form two na elimu yangu ya form 2A nilijifunza mambo ya specialization and division of labour, kauli kama hizi tulikuwa nazo those days nadhani inatokana na those days shule nyingi best students walikuwa ni watu wanaosoma science hivyo kishule shule tukawa tumejijengea kwamba science ni nzuri kuliko hizi zingine. All in all kila fani ina umuhimu wake hata huyo aliesoma Engineering anapotaka kutekeleza majukumu yake lazima ashirikiane na mtu wa Procurement ili taratibu za zabuni zifuate lakini pia anapokwenda site kama kazi anayoifanya ina-involve watu lazima mtu aliesoma Sociology apite kwanza kupiga mbili tatu na wananchi ili pindi shughuli inapoanza wasije wakaikataa na kusema hawajashirikishwa.

Ugumu wa masomo unategemeana na background yako kwa mfano mie huwa nina amini hisabati ni somo rahisi ila kwa kuwa ninaliweza na wengi huwa wanafeli nisijione kwamba mie ni mkali kwa kuwa nimeweza somo gumu kumbe kwa case yangu ni somo rahisi kutokana na background yangu the same kama ukinipa History kwangu mie itakua ngumu kwa kuwa sio uwanja wangu.

Mleta uzi kwa vyovyote akipewa taasisi aongoze kila siku kutakuwa kuna mgomo kwa kuwa anaamini science siku zote inakuwa mbele wakati ukweli ni kwamba ili science ifanye kazi vizuri (hardware) inahitaji watu wengine ambao sio pure scientist kufanya nao kazi kwa kuwa mwisho wa siku tunafanya kazi na jamii ambayo yenyewe inahitaji huduma zetu na wala sio nani kasoma kozi hii na mwingine kasoma ile
 

Umemaliza mkuu maana hata mie before nilikuwa nina mtazamo huo lakini nikagundua unapokuja huku kazini unagundua kumbe mambo ni tofauti na mbinu inayotumika ni integrated approach kwamba kila mtu kwa nafasi yake ana mchango wa kuhakikisha kazi inakwenda hata kama ni standard seven but ana kitu ambacho unaweza ukawa huna pamoja na kwamba umesoma. Mleta uzi ana hoja hapa ila the way alivyoiwakilisha inaonyesha kuziponda fani zingine, kama angesema ukisoma fani hizo za uhandisi unakuwa na wigo mpana wa kusoma fani zingine kwa level ya juu tofauti na watu ambao wamesoma hizo fani alizoziponda kwa kuwa hawana background ya hayo masomo katika level za chini.

Kutokana na mitazamo ya namna hii na ndio maana mwanafunzi yoyote wa higher learning lazima asome DEVELOPMENT STUDY (lengo ni kuwajenga watu wafikirie mambo in social perspective though wengi hili somo tunalichukulia kama uzushi flani hivi but lina maana yake kubwa)
 

liambie mkuu
 
hiyo ni stress.anasoma masomo magumu alafu hajui future yake iko vipi.so to gain confidence anauliza maswali ya kitoto.we jamaa soma kwanza watu wanapga shule ngumu zaidi ya ulizozitaja kwenye vyuo bora kabsa.poor u low thinker.
 
Haya sasa, vijana wa vyuo vya kata naona wanaruka na kukanyagana!
 

Aisee umesema ukweli, makazini watu tuliosoma sayansi tunatawaliwa na hao hao amabo watu hwadharau wakiwa vyuoni,huyo dogo hajui maisha bado mwache atajifunza! kama haoni tu wana siasa ndiyo wanatanua mwache aendelee na mawazo hayo ya engineering wengine tulitoka huko tunajua sasa na tunaona! kuna wajamaa kibao wameishia kua ma teller kwenye Bank na kutawaliwa na hao anao wadharau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…