Inasemekana kuwa kule East Africa Radio na TV Zembwela anakubalika sana kwa kuwa degree yake ya uandishi wa habari kaisomea ughaibuni.
Hivi ni nchi gani wakuu?
Kile kipindi ilitakiwa apatikane mtangazaji mwenye akili timamu, halafu Zembwela apewe EA Drive mida ya jioni wakati tunapambana na foleni kurudi nyumbani tunasikiliza ujinga wake
Huwezi kukosoa kitu usichokua na elimu nacho.Wewe umejuaje kama anaimudu?elezea katika misingi ya taaluma ya utangazaji na si porojo.Angekua anaimudu kama akina Soud Mnete,Regina Mwalekwa......si angekua amechukuliwa na mashirika makubwa.Radio broadcast sio kubwabwaja tu,ile ni taaluma baba.kwani elimu inapatikana darasani tu jamani [wewe mtoa uzi] ; jamaa anaelimu ndo maana anaimudu kazi; inawezekana hajaipata katka mfumo rasmi- lakini bado anaelimu!
Huwezi kukosoa kitu usichokua na elimu nacho.Wewe umejuaje kama anaimudu?elezea katika misingi ya taaluma ya utangazaji na si porojo.Angekua anaimudu kama akina Soud Mnete,Regina Mwalekwa......si angekua amechukuliwa na mashirika makubwa.Radio broadcast sio kubwabwaja tu,ile ni taaluma baba.
Hivi yule mtangazaji wa zamani wa CNN, Larry King, alisoma shule zipi vile?
Mleta mada kosa lake nn ??? Hata kama zembwela ni darasa la 2 watu wangependa kujua ili wenye vipaji kama yeye wasijidharau pengine sikumoja wanaweza kuwa kama yeye. Mbona kila siku humu if watu wanauliza CV za watu ??? Ya zembwela imekuwa nongwa!!!
Inwezekana huyu mleta mada kwanza nahisi anakaa nyumbani kwao au amepangisha tena uswahilini,ndiyo maana anaona degree kitu cha maana,nataka nimwambie watu wote wliyofanikiwa duniani,kama vile billgate,henry ford,thomas edison,yule jamaa wa facebook hawana degree,wengine hapa tanzania ni kina bakheresa,kwahiyo wewe baki na hiyo degree yako utakufa maskini na familia yako,unafikiria mtaani ni sawa na shule,huku moja jumlisha moja sio lazima iwe mbili majibu yako mengi,shuleni jibu ndiyo moja,ukikosa basi na wewe umefeli,ila mtaani majibu ni mengi sana ndiyo maana unakuta watu ambayo hawana elimu za juu wanafanikiwa sana kwasababu wanajiamini
Watu humu ndani mnapenda kuchepuka nje ya mada.
Hii mentality ya kuwathaminisha watu na makaratasi haitatufikisha popote kama taifa.
Ukishajua kama ana degree ya Chuo swali litakalofuata ni GPA yake.
Nimeona humu JF watu kuna thread zaidi ya 2 kwa ajili ya kumdiscuss Zembwela personal, hii inadhihirisha kwamba ni mkali na yupo ubongoni mwenu!
Atakuwa kawaketisha chini wenye vidigrii vyao vya darasani wanaoomba kazi EATV na Radio.
Haiwezekani mtu mmoja kudiskasiwa mara mbili on the same topic
Yani kama kijana una degree hata kama kwa sasa huna kazi usije ukadharau elimu yako hata siku moja kwasababu kuna watu wana tamani wangekuwa nayo endelea kuamini una asset nzuri