kwa kuanzia universities ni pana in terms of fields za kusomea tofauti na Institute. kwa suala la ubora, inategemea university au institute husika imejikita zaidi katika kuelimisha fani zipi. vilevile namna ya ufundishaji katika universities na katika institutes ni tofauti (i.e. curriculum zao ni tofauti) universities zinafanya Knowledge Based Curriculum while kwenye Institutes wanafanya Competence Based Curriculum ndio maana the latter wako under NACTE na wengine wapo under TCU. suala la ruhusa ya kutoa shahada kwa upande wa Institutes linategemea sana mtaala wao kupata ithibati kutoka chombo chao cha usimamizi yaani NACTE. Kwahiyo kama taasisi imepata ithibati kutoka NACTE kuendesha mafunzo, hakuna shida yoyote.
muajiri ambaye anataka wahitimu wa vyuo vikuu pekee na kutoamini wa kutoka kwenye taasisi kwakweli labda niseme anahitaji kuwa updated. if u ask me uwezo wa mtu kudeliver anapokuwa kazini unategemea sana juhudi yake binafsi ya kugrasp na kuelewa yale aliyokuwa akisoma na bidii yake ya kutaka kuendelea kujifunza na nidhamu ya kazi. chuo kikuu au taasisi aliyotokea mtu, huwa na mchango ila ni kwa asilimia ndogo sana.
kwa suala la scholarship, wote wanapata, wawe wanatoka universities au institutes, it depends na GPA aliyonayo muombaji na mara nyingine chuo au taasisi aliyotoka inafahamika vipi na chuo anachoapply mhusika kwenda kwa masomo zaidi.
ni hayo niliyo nayo mimi, perhaps siyo yooote ila yatakuwa yamegusa palipoulizwa.