Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Wamarekani wanapiga kura leo kuwachagua wabunge na maseneta, katika uchaguzi wa katikati mwa muhula wa urais wa Joe Biden.
Katika uchaguzi wa leo, viti vyote 435 katika Baraza la Wawakilishi vinapiganiwa, huku kwenye Baraza la seneti, viti vilivyo kwenye kinyang'anyiro hiki vikiwa 35 kati ya 100 vilivyopo.
Uchunguzi wa maoni ya wapigakura unabashiri kuwa chama cha Democratic cha Rais Joe Biden yumkini kitapoteza udhibiti wa mabaraza yote mawili.
Ikiwa chama cha Republican kitashinda kama inavyotarajiwa, uongozi wa Biden utakabiliwa na changamoto kubwa kwa sababu mipango yake yote ya mageuzi itazuiliwa.
Matokeo ya uchaguzi huu pia yataamua ikiwa rais wa zamani, Donald Trump, atajitosa kuwania tena urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2024.
DW