Demokrasia bila ushirikishwaji wa wananchi ni Demokrasia?

Demokrasia bila ushirikishwaji wa wananchi ni Demokrasia?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Mfumo wa Demokrasia unahitaji wananchi kushirikishwa katika maamuzi ya nchi yao kwa kuchagua viongozi na kutoa maoni yao kuhusu sera na sheria.

Ushiriki wa wananchi sio tu msingi wa mfumo huu bali pia ni njia ya kuhakikisha kwamba serikali inawajibika vilivyo kwa maslahi ya wananchi wake kwasababu watakuwa wanafanya maamuzi wakiwa na taarifa sahihi.

Kama serikali au viongozi hawawaruhusu wananchi kutoa maoni yao, kuchagua viongozi wao kwa njia huru na haki, au kushiriki katika mchakato wa kisiasa, basi demokrasia inabaki kuwa jina.
 
Back
Top Bottom