GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Wakenya wanastahili pongezi kwa hatua waliyofikia katika demokrasia. Lakini kama demokrasia ikiwa inakiuka maadiki ya Jamii husika, inakuwa ni ya hasara badala ya faida.
Nionavyo, kwa sababu ya uhuru wa kujieleza, baadhi ya Wakenya, hasa vijana, wanatumia hiyo fursa kufanya mambo ambayo ni ya "aibu" kwa Jamii za Kiafrika.
Fikiria:
1. Kipindi fulani, nilimsikia mwanasiasa mmoja akimtukana Rais Ruto kwenye mkutano wa kisiasa. Akiwa anashangiliwa na wafuasi wake, alimtukana matusi ya nguoni
2. Kuna video clips nyingi za Wakenya ambazo ni kama zinahamasisha ushoga na usagaji. Fikiri binti anaulizwa kama alishawahi kuingiliwa kinyume na maumbile, au kama alishawahi kujamiiana na mwanamke mwenzake. Hiyo inaashiria nini kama siyo kuhamasisha ushoga na usagaji?
3. Maswali wanayoulizwa mabinti na vijana wa kiume kuhusiana na mapenzi, mengine yana ukakasi sana. Hayakupaswa kuulizwa hadharani. Wakati mwingine unawaza, wazazi wake watajisikiaje ikitokea hizo clips zimewafikia?
Demokrasia inatoka uhuru wa kujieleza, lakini kwa ajili ya afya ya kimaadili, ni muhimu demokrasia ikawekewa mipaka kuepusha kuwa kichocheo cha mmomonyoka wa kimaadili.