DEMOKRASIA KAMA MSINGI WA MAENDELEO
Tanzania ni nchi ya kidemokrasia kwa mujibu wa Katiba ambayo viongozi wetu huitumia kuapa wanapoingia madarakani. Ibara 8(1) ya Katiba yetu inasema “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya kidemokrasia na haki ya kijamii na kwahiyo;(a) wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii.
“Ni kweli kwamba demokrasia haiwezi kudumu ikiwa wachache hawatakubali matakwa ya wengi. Lakini matakwa ya wengi hujulikana katika majadiliano au mazungumzo ya waziwazi. Kadhalika matakwa ya wachache hujulikana katika majadiliano na mazungumzo. Bila wale wachache kusema waziwazi matakwa yao, majadiliano hayana maana.Wakati mwingine hata baada ya majadiliano wachache japo wamekubali kutii uamzi wa wengi, wanaweza kuendelea kuamini kwamba mawazo yao ni sawa na yaliyo ya wengi yamepotoka. Demokrasia inawapa haki na ukweli unawapa wajibu wa kuendeleza mawazo yao mpaka wengi waone kuwa ni ya kweli. Bila hivyo maendeleo katika mawazo hayawezekani” (Tujisahihishe, uk 3, J.K.Nyerere 1962)
Lakini msingi mkuu wa demokrasia unaanza na uhuru wa maoni ambao umetamkwa katika ibara ya 18(1) inasema, “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi”
Kama taifa tumekuwa na utamaduni wa kukwepa mazungumzo ya vikao, siku hizi hata familia hazikai kama zamani kufanya mazungumzo ya kifamilia, mama au baba akiwa na jambo anaona haya kulifikisha moja kwa moja badala yake anasubiri mwenza wake aende kwenye shughuli zake kisha anatumia ujumbe wa simu (sms) kufikisha ujumbe au wengine wanakwenda kuandika kwa mafumbo kwenye mitandao ya kijamii mambo ya familia. Hii ni hatari kubwa sana kwa taifa, zamani tulizoea vikao palipotokea jambo fulani kwenye familia, watu waliitana kwaajili ya mazungumzo na ufumbuzi ulipatikana kisha watu kusambaa kila mtu akiwa na ukweli wa jambo.
Demokrasia inaruhusu uvumbuzi au maboresho (innovation), utamaduni wa kuzuia watu kuzungumza Afrika unatokea kwenye familia. Tumeona mara kadhaa hata mashuleni wanafunzi wenye tabia ya kuhoji wakidhibitiwa na baadhi ya walimu wao, leo watu wengi ambao ni viongozi wetu mahali popote ukiwauliza historia zao watakwambia misukosuko waliopitia na hii ilitokana na uwezo mdogo wa kujibu hoja wa wale waliokuwa wakiwasikiliza.
Watoto katika umri mdogo, wazazi na walimu wao wakiwa na tabia ya kuwakemea na kuwafokea maranyingi zaidi huwatengenezea udumavu wa fikra athari zake wanashindwa kuwa hata wabunifu katika maisha yao maana kila anachojaribu kufanya anaona atakosea. Mwisho tunatengeneza taifa la makondoo na mazombi matokeo yake wakiwa viongozi watashindwa hata kuhoji juu ya mikataba mibovu dhidi ya rasilimali zetu.
Mtu yeyote ambaye hajazoea kuhoji pia ni mdhaifu wa kujibu hoja za wengine anaona njia nzuri zaidi ni kutumia nguvu kuzima hoja badala ya kuzijibu. Bahati mbaya tunadhani demokrasia ipo katika usawa wa madaraka pekee, wanasiasa wengi wanapozungumzia demokrasia hulenga zaidi usawa wa kimamlaka bila kutazama athari nyinginezo zinazotokana na uminyaji wa demokrasia katika nchi, tujenge utamaduni wa vijana wetu kuwa majasili wa kujenga hoja zenye ushawishi kuliko kutisha watu hawa watakuwa viongozi wa kesho.
Demokrasia ni taa kwa wenye mamlaka kama inatumika vizuri, wasiyo na mamlaka wakisema hapa hamjafanya hivi na vile mnapima kisha yanafanyika marekebisho kesho watakuwa na yapi? Yako ya kupuuza na mengine ni ya kufanyia kazi, unapoyafanyia kazi tayari maendeleo yamefanyika.
Jambo muhimu sana kwa kila kiongozi ni kutofikiri kwamba mamlaka yanampa uwezo wa kiakili zaidi kuliko wengine, hivyo lazima kuyatafakari yale yanayosemwa na wengine na ukitaka kuyafahamu vizuri zaidi ni kukaa nao mezani kama ndugu kujadiliana na mwisho utagundua kwamba wewe ndiye uliyekuwa unakosea, hii ni kwasababu ukiwa uwanjani ni vigumu kugundua makosa.
Sifa moja kubwa kuliko zingine zote za kuwa kiongozi bora ni kuwa na uwezo wa kusikiliza zaidi hata yale usiyopenda kusikia, viongozi wengi dhaifu duniani hupenda kusikia yale tu yanayo wafurahisha, utasikiaje mabaya na mazuri ni katika uhuru wa maoni na maendeleo yametokana msuguano wa mawazo kwamba hili liko hivi na unaonyesha.
Nguvu hazijawahi kuzaa matokeo mazuri ya muda mrefu bali ni kwa muda mfupi halafu zinaishia pabaya tujifunze historia kisha tuchaguwe upande ulio mwema. Viongozi wa Tanzania, lazima wakubali kwamba, demokrasia ndiyo kiini cha Ujamaa (Nyerere, J.K 1977 Azimio la Arusha baada ya Miaka kumi).

Upvote
0