Demokrasia Marekani kubwa sababu wanasiasa wana shughuli za kuwaingizia vipato nje ya siasa tofauti na Tanzania

Mtu Kama Lissu hana kitu zaidi ya lile tumbo unategemea atafanya nini zaidi ya kuchukia wenye nacho?
Ukiwa mjinga utasema Lissu hana kitu.

Ukiwa na akili utasema Lissu ni tajiri mkubwa na utajiri wake upo Kwenye ubongo wake.

Hata akiacha siasa Leo Lissu atatengeneza mabilioni kwa kuandika vitabu na majalada mengine ya dunia.
Lissu atapewa kazi mara moja na vyombo vikuu vya dunia kwa Mfano wake wa mazingira ili awafanyie kazi.

Watanzania na ujinga wao wanafikiri utajiri ni kuhodhi mali nyingi za kuiba Kumbe utajiri sahihi ni elimu ya kweli iliyo kichwani inayohitajiwa na dunia.

Clinton alimaliza Urais akiwa na madeni sasa ni milionea. Obama na mkewe wamemaliza urais wakiwa hawana kitu, sasa ni mamilionea.

Unayesema Lissu ni maskini kweli wewe ni maskini wa akili😭😭😭
 
Akili sake zimemsaidia nini Kama kashindwa kujinunulia gari anaomba omba Kama matonya??
 
Ukweli.
 
Kwa ufupi,siasa za marekani, na nchi za ulaya, mwanasiasa ni mtumishi wa umma aliyeapa kutoa huduma na endapo atakosea,na akigundua, huwajibika. Siasa za kiafrika ni za kulindana, kiongozi akifanya kosa, au kuvunja katiba hawajibiki na akikosolewa, mkosoaji huonekane kama mhaini. Sasa tujikite kutafuta katiba mpya itakayowapiga Pini viongozi wetu ili watutumikie.
 

Ya Tanzania ni kubwa zaidi kuishinda ya Marekani ya Tanzania mgombea anakamata Begi limekaa kura feki zilizopigwa tayari, na hakuna mtanzania anafanya kitu, mwizi wa kura na wezi wa kura wanajulikana na wanajitangaza wameshinda kwa kishindo!!

Badili heading weka demokrasia ya Tz ni kubwa kuliko Marekani 😅😅🚴🚴
 
Ni sisi wenyewe hapa hapa JF huwa tunalalamika kuwaweka wafanya biashara kuwa kwenye nafasi za uongozi, tukisema wanatunga sera na sheria kwa manufaa ya biashara zao.
Wewe tena unalalamika wasio na kipato kuwa viongozi.

Hatueleweki..!!!!
Tajiri Anayeta ajira ndie apewe uongozi

Wakinufaika wananufaisha mamilioni

Sababu pia ni mlipa kodi tena mkubwa na wafanyakazi alioajiri pia wanalipa kodi mishahara yao

Anaajiri wafanyakazi familia zao zinatoka kimaisha wanapata pesa za kununua bidhaa ,biashara zinachangamka mitaani pia sababu mwajiriwa wao kapata mshahara .Na zenyewe zibalipa kodi

Hivyo mnyororo wa thamani wa ajira, kodi na biashara unaongezeka na quality ya maisha ya wananchi inaongezeka

Lakini ukiweka mtu mfano Lisu na Lema kwenye uongozi unaongeza thamani gani kwenye mnyororo wa ajira,kodi na biashara ? Ni hasara tu sababu wanapiga porojo tu
 
Ukiwa mjinga utasema Lissu hana kitu.

Ukiwa na akili utasema Lissu ni tajiri mkubwa na utajiri wake upo Kwenye ubongo wake.
Chadema kuendeshwa kinahitaji pesa kujiendesha sio ubongo wake unaozalisha maneno matupu hewa yasiyo na pesa

Hadi sasa huo ubongo wake umezalisha shilingi ngapi kuingiza kwenye akaunti za Chadema?

Chadema inataka Pesa sio ubongo
 
Akili sake zimemsaidia nini Kama kashindwa kujinunulia gari anaomba omba Kama matonya??
Akili yake ndio imemfanya awe Mwenyekiti wa Chadema. Hana muda wa kutafuta pesa Kwasasa ana muda wa kuwatumikia Watanzania.

Kibaya zaidi hata gari lake wajinga wamelipiga risasi.
 
Hii ni pointi
 
Akili yake ndio imemfanya awe Mwenyekiti wa Chadema. Hana muda wa kutafuta pesa Kwasasa ana muda wa kuwatumikia Watanzania.

Kibaya zaidi hata gari lake wajinga wamelipiga risasi.
Sio akili ni ulaghai na siasa chafu za kudhalilisha wengine bila ushahidi

Siasa kama hizo huwa hazina future

Uchaguzi hata uitishwe leo ile karibu asilimia 49 waliomkataa Lisu hawatampa kura akigombea .Na hao asilimia 49 walichaguliwa hivyo wao na waliowachagua hawatampa kura Lisu wa ndani ya Chadema

Hivyo uchaguzi mkuu hata uitwe leo Lisu awe na uhakika asilimia 49 ya wanachama wote wa Chadema hawatampa kura sababu kaingia kihuni kwenye uenyekiti na hadhi ya Mbowe hata akipita mtaani

Mbowe alikuwa akipita popote mtaani lazima palipuke shangwe
 
Huyo Lissu hats akitaka kuondoka leo na kutafuta kazi za juu za dunia anapata. Kazi za kulipwa dola zaidi ya laki mbili kwa mwaka.

Ila sasa hiyo akili yake kaamua kuitumia kuwakombia Watanzania waliolala kama wewe.

Unafikiri utajiri ni mali za kuiba. Kumbe utajiri ni kile ulichonacho kichwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…