Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Bado sijajua kwa usahihi mpaka wa uchanga wa umri wa Taifa lolote ni miaka mingapi, ila nikiitazama Tanzania bado naona miaka 50 bado taifa hili ni changa. Katika uchanga huu ni lazima tukubali kutoa sadaka jambo moja kwa ajili ya jingine ili hilo lililotolewa sadaka lije kukutana na lile lililoachwa kushamiri. Nazungumzia Demokrasia na Maendeleo. Tukubali kama Taifa kuacha lipi kwanza na kuongozana na lipi kwanza.
Demokrasia yetu hadi sasa ipo katika nadharia tu hasa tukitilia maanani yale yanayotokea sasa na yaliyotangulia. Tangu kuanza kwa Taifa hili chini ya Uhuru toka wakoloni, pamekuwa hapana demokrasia ya uwazi kiasi cha kutosha kusema kuwa jambo hili linafanyiwa kazi kivitendo. Azimio la Arusha halikuwa na mrengo wa demokrasia japo lengo lilikuwa jema. Singependa kurudi sana huko awali. Mivutano ya leo katika siasa zetu ni picha ya wazi ya kukosekana hiyo demokrasia-utawala wa Raia na uhuru wa maoni, uhuru wa kuamini dini na itikadi pasina kuvunja sheria za nchi. Matokeo yake tunashuhudia mivutano, mitafaruku, mikandamizo, vitisho, na mauaji. Siasa ndio mwongozo wa taratibu za nchi. Siasa ndio maisha ya kila siku. Katika Demokrasia tumeshindwa.
Maendeleo ni uboreshwaji wa hali za kimaisha za watu katika jamii wanamoishi. Haya maendeleo huonekana katika miundombinu (barabara, madaraja, reli, anga, elimu, afya, lishe, n.k), matumizi ya rasilimali (watu, ardhi, maji, madini, misitu, n.k), sayansi na teknolojia, n.k. Kote huko sisi kama Taifa tumeshindwa kuwa na comparative advantage pamojja na kuwa na kila namna ya kutuwezesha kama Taifa kutumia tulivyo navyo kujiletea maendeleo.
Libya hapakuwa na demokrasia lakini palikuwa na maendeleo. Lakini kuminya moja na kukuza jingine isiwe ni ajenda ya kudumu. Wakati fulani katika Taifa watu wanahitaji kufurahia demokrasia na maendeleo kwa wakati mmoja. Hapa kwetu je? Tunafurahia vyote viwili kwa wakati ama tunaumizwa na vyote viwili kwa wakati mmoja?
Katika hili ndipo nataka pia kuhoji dhana ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Ni walewale? Watapeleka haya mambo mawili kwa pamoja au wataanza na moja? Wanaamini katika demokrasia na maendeleo au demokrasia kwanza, au maendeleo kwanza? Kipi kipewe kipaumbele; maendeleo ama demokrasia.