kutolea mifano kwa nchi hii haimaanishi kuwa nakubali yale yanayofanywa ama kusadikika kufanywa na hivyo vyombo nilivyotaja hapo juu. Ukweli sera na sheria tunavyo ila ni butu. Think tank tunayo ila haina meno. Think Tank ya Hitler ilifanya kazi under great pressure, with all available resources at their disposal, na wali deliver. Hapa kwetu sio hivyo. Wataalam wetu wataandika wajuayo kuwa yana tija kimaendeleo na kisha kuikabidhi serikali. Sasa hapo ni juu ya serikali kuamua kutekeleza au kupiga danadana kwa visingizio vya 'vipaumbele' na 'bajeti finyu'. Nyerere yeye alisema kuwa hata angepewa miaka mingine 20 asingekuwa na jipya. Tujiulize ni kwa nini alisema haya. Ndipo ninaporudi kwenye hoja kuwa falsafa za mtu mmoja hazitoshi kuleta mabadiliko bali nguvu na mawazo ya watu kwenye mifumo ya kitaasiisi. Tulishaambiwa kuwa Afrika haihitaji tena strong men bali strong institutions. Hii ni kutokana na ukweli kuwa mambo yamebadilika
Mkuu
Hebu tuingalie jamii yetu, tuna rasilimali za kutosha lakini zinamnufaisha nani? Tuna rasilimaliwatu( vijana wakiwa wengi zaidi) lakini haiendelezwi, haina mwongozo wala kiongozi wa kumuangalia. Lakini katika hao wapo wachache walioendelezwa,tuna wataalamu karibu kila nyanja,ingawa sio wa kutosha,lakini wapo ila mbona hatuwatumii? Hawathaminiwi?mpaka wengine wanaende kuendeleza nchi jirani?
Tunaweza kutengeneza sera na sheria nzuri, tafiti mbalimbali zikafanywa lakini kwa hapa tulipo lazima awepo mtu wa kulianzisha, atakaye kuwa na moyo wa dhati kabisa kuzisimamia rasilimali zetu, kuendeleza rasilimaliwatu na kuufufua moyo wa uzalendo kwa watanzania, atakaeweza kukemea ukabila na udini bila ya haya wala woga, atakaerudisha misingi ya UTU na misingi ya mtanzania kama alivyofanya Mwalimu. Kwa sababu tukubali au tukatae hichi kiini macho tunakiita demokrasia kinaua moyo wa uzalendo, kwa jamii iliyoisusia ELIMU,iliyoamua kumuangalia mtu kwa misingi ya udini,ukabila,kipato na kuwatenga wasio na elimu democracy will never work hapa. Idadi ya wajinga inakua,siku hizi mtoto anayeenda kuanza kidato cha kwanza anakutana na mtihani unaitwa K.K.K( kusoma kuandika kuhesabu), hebu niambie hawa wanaweza kujua na kuchagua sera nzuri kwa ajili ya maendeleo yao? Au wanahitaji kushikwa mkono, kutolewa tongotongo za ujinga mpaka waweze kujua tofauti ya fisadi na mwanasiasa ndipo tuwaletee demokrasi!
Hebu jiulize Mwalimu pamoja na mapungufu yake yote ambayo watanzania leo hii mnayaona sana aliweza kuungana na nchi za afrika mashariki bila yeye wala nchi kumezwa na hizo nchi nyingine,kwa nini sisi leo tunaogopa sana hii kitu, kwa nini tunawaogopa sana wakenya na chuki juu yao lakini tunawakumbatia so called wawekezaji?
Rwanda inakimbia, wataalamu waliokua nje,waliokimbia wakati wa mauaji ya kimbari wanarudi kuijenga nchi yao, huu moyo wa uzalendo wameutoa wapi? Mbona sisi tunaojiita wakidemokrasia tunashindwa na "dikteta" Kagame?