Demokrasia ndani ya TFF inasiginwa, wanaharakati kimya

Kajeba

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2020
Posts
1,057
Reaction score
2,364
Hii ndio Tanzania, huwezi kuta hao wanaojiita wanaharakati wanaharakatia kitu kisichokuwa na maslahi ya kifedha kwao

Demokrasia ni pana sana, hao wanaharakati wanajua upana wake na wapo kutetea haki na misingi ya democracy hapa nchini isisiginwe

Wanaharakati wa chadema na mitandaoni wapo kimya as if hakuna kinachoendelea huko TFF.

Mko wapi ninyi watu wa twitter, Jf na chadema kupinga kwa nguvu haya yanayoendelea Tanzania?

Mko wapi msiandae petition kwenda FIFA ishushe rungu lake Tanzania?

Au sababu hakuna maslahi ya moja kwa moja kwenu?
 
FIFA, CAF na TFF walijiwekea "mfumo" ambao hao wanaharakati uchwara hawawezi kufua dafu!
 
Hiyo nafasi mpaka utolewe ni mpaka zengwe
Ukiona mpaka sahvi kimya,basi mjue zengwe hakuna

Ova
 
Kwa kweli demokrasia inasiginwa ndani ya TFF.

Jana, msimamizi wa uchaguzi wa TFF, wakili jina lake la mwisho Karume, nilimsikia akisema, kwa kuwa Karia hana mpinzani, basi anasubiri kuidhinishwa na wajumbe wa mkutano mkuu.

Kitendo hicho ni cha kuvunja demokrasia, kwa sababu anatakiwa apigiwe kura ya ndio au hapana. Sasa, kama ni mgombea peke yake kwa nini kanuni haziruhusu kupigiwa kura ili ajijue, na akipigiwa kura ya hapana, basi atafutwe mgombea mwingine!

Wamezidiwa na CCM ya Ujamaa, ambapo mgombea alikuwa ni mmoja, lakini alikuwa anapigiwa kura!

Pia, TFF wameweka vi-kanuni vya kuwaminya wagombea wengine ili iwe rahisi kuenguliwa.
 
TFF wamejaza kufuli wamejifungia ndani asiingie mtu na hata mwingine atakae iingia pia mwendo utakua ndo huo.hii ndo bongo mizengwe kila sekta na ndo hulka tuliyojijengea sisi wabongo.,wizara kimya,takukuru kimya,wanaharakati kimya utadhani yanayoendelea TFF ni sahihi.
 
Ni kweli inaweza ikawa hivyo, lakini ningependa sana kujua sababu za kwa nini wagombea wengine walienguliwa. Ni kweli walikosa sifa za kugombea? au kuna kingine nyuma ya pazia. Lakini pamoja na hayo,kwa maoni yangu kuhusu wale wagombea walioenguliwa naona hakukua na serious candidate wa kum-challenge Karia. Wengi walienda kujaribu tu na kuongeza CV zao kiasi fulani.
 
democracy imesiginwa unataka sababu gani tena za hao wengine kuenguliwa?
 
Yaani kwa namna ilivyo unaweza kudhani sifa ya mgombea wa Urais (TifuTifu) ni kuwa na kitambi.

Maana kila mmoja kaondolewa kuwa hana sifa za kugombea.
 
Legacy ya mwendazake
 
Mkuu siasa za mpira ni tofauti kabisa na hizo ambazo wanafanya hao wanaharakati, nikumbushe Tu kuwa raisi wa FIFA aligombea mwenyewe, raisi wa CAF aligombea mwenyewe

Kwahiyo Hilo sio Jambo geni kwenye Mpira, kwenye Mpira huwezi kumtoa raisi aliepo madarakani Hadi amalize muda wake au aundiwe zengwe, kwahiyo ukisema wanaharakati waingilie Kati basi itabidi waingilie duniani kote maana hakuna nchi yenye demokrasia kwenye kupata maraisi wa mashirikisho ya Mpira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…