Demokrasia ni adui wa maendeleo

Korea zote ziliendeshwa kidikteta. Moja ikawa tajiri nyingine bado. Hiyo iliyokuwa tajiri ikaamua kuwa na demokrasia. Sina mfumo ninaotaka, ninachotaka ni tukae chini na kutafuta mfumo utakaoweza kuteletea maendeleo.
 
Naunga mkono As
Naunga mkono asilimia mia Ccm Daima
 
Naunga mkono title ya mada hii. Demkkrasia inafaa kwa mataifa yaliyoendelea tayari. Lakini kwetu sisi ni upotezaji wa rasilimali muda, fedha na nguvukazi
Ofcourse democarcy ina work well kwenye jamii ambazo tayari ni developed, organized, na zime staarabika.
Lakini si mfumo mzuri kwa jamii zinazoanza
 
Korea zote ziliendeshwa kidikteta. Moja ikawa tajiri nyingine bado. Hiyo iliyokuwa tajiri ikaamua kuwa na demokrasia. Sina mfumo ninaotaka, ninachotaka ni tukae chini na kutafuta mfumo utakaoweza kuteletea maendeleo.
Kwa nini Korea Kusini ambayo imekuwa na utawawa wa kidemokrasia kwa kipindi kirefu cha zaidi ya nusu karne imekuwa tajiri na yenye maendeleo makubwa sana kuliko Korea Kaskazini ambayo imekuwa na utawala wa kidikteta karne zote/maisha yake yote mpaka sasa??
 
..Udikteta umeshindwa kuleta maendeleo Afrika, ndio maana kumekuwepo na kelele za kudai demokrasia.
Udikteta umefanya kazi nzuri Africa kuliko demokrasia. Nchi kama Shelisheli, Libya na Misri ni mfano wa nchi chache zilizofanya vizuri chini ya Udikteta. Kwa miaka zaidi ya 30 "kelele za kudai demokrasia" na demokrasia yenyewe haijafanya chochote kuitoa Africa kwenye umaskini.
 
Kwa asilimia kubwa Africa haina demokrasia na bado inaongoza kwa umaskini na maendeleo duni.
Nchi kama South Africa tunaweza kusema ina demokrasia iliyokomaa vizuri kwa miaka 30. Kilichotokea ni demokrasia hiyo kuharibu maendeleo yaliyopatikana enzi za apartheid.
 
Korea zote ziliendeshwa kidikteta. Moja ikawa tajiri nyingine bado. Hiyo iliyokuwa tajiri ikaamua kuwa na demokrasia. Sina mfumo ninaotaka, ninachotaka ni tukae chini na kutafuta mfumo utakaoweza kuteletea maendeleo.
NK ilikuwa bora kuliko SK balaah lilianza miaka mwisho wa miaka ya 80s na anguko la Soviet liliizika NK ukichanganya na vikwazo vingi alivyonavyo ndio balaah linazidi.

Ila wakorea wana akili za kuendelea no matter what sema tu vikwazo vinawavuta nyuma kidogo na ndio maana pamoja na vikwazo vyake ila kwa vipimo vingi NK ni bora kuliko nchi nyingi sana za Africa kwa sababu hatuna akili za kuendelea pamoja na kuwa huru nje ya vikwazo vya kimataifa.

Korea zote mbili zimendelezwa kwa udikteta.

East Asians mfumo wa kidikteta upo ndani ya maisha ya unachochochea ni uharaka zaidi wa maendeleo na ndio maana wachina,wajapan,wajorea wana hizi elements popote walipo duniani.

Si ajabu Singapore kuendelea ukikata kuthibitisha hili kamsikilize Lee Kuan Yew akizungumzia vitu gani vinavyowasukuma wachina popote walipo kufikia maendeleo ukihusiana na tamaduni zao.

Je, waafrika tuna hizo akili za kujali maendeleo kama wachina, wajapan,wachina kwa kutumia utamaduni wa kidikteta kimanufaa au tuna tumia udikteta kujinufaisha sisi wenyewe na jamaa zetu waliotuzunguka ? Swali la kujiuliza na kujijibu
 
Maendeleo ya Korea kusini yanesababishwa na udikteta wa kijeshi chini ya sheria za kijeshi kwa muda mrefu juzi tu hapa Yoon Suk Yeol alitaka kuwarudisha kule walipo pazoea tuachane na hayo.

Ila Korea zote mbili maendeleo yake yamebebwa na udikteta kwa asilimia kubwa utofauti uliopo ni kati ya SK na NK ni katika vita baridi baada ya Eastern bloc kuanguka baada ya anguko la Usoviet kilicho fuatia ni anguko la NK pia toka miaka ya 80s wakati upande wa pili SK haikuathirika na anguko hilo kwa sababu haikuwa upande huo.

Baada ya hapo ni vikwazo vilifuatia kwa NK mpaka leo hivyo haishangazi SK kuwa bora kuliko NK
 
Waafrika hamuwezi kujua maana ya demokrasia kwa sababu ya roho mbaya, uchawi na kutomjua Mungu ile amri ya upendo ni 0 tena unakuta mpo misikitini na makanisani wakati hamjuhi kuwa muasisi wa demokrasia ni Mungu mwenyewe vinginenevyo waafrika wote tunapaswa kupotea kwenye uso wa dunia kwa sababu tunaleta jamu.
 
Korea Kaskazini hakuna maendeleo zaidi ya kutengeneza mabomu, muda mrefu tu wamekuwa wakipewa msaada wa chakula na Korea Kusini, Japan, China na Marekani. Korea Kaskazini ni tegemezi wa China.

Kwa nini Poland, Hungary, Romania, Bulgaria, Czech na Ukraine zilizokuwa chini ya USSR zimeweza kupata maendeleo makubwa katika demokrasia baada ya kuanguka usovieti(USSR) huku Korea Kaskazini ikashindwa kupata maendeleo chini ya udikteta wa familia ya Kim??
 
Unafafanisha nchi inayokabiliwa na rundo la vikwazo baada ya kuanguka kwa usoviet na hizo nchi ulizotaja upo serious kweli ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…