Demokrasia ni adui wa maendeleo

Zote zimekuwa zinatawaliwa kidikteta kwa zaidi ya karne ila bado ni masikini wa kutupwa.
Kwa nini hazijapata maendeleo??
Hizo ndizo North Korea na South Korea kwa ulicho kiandika ?

By the way sipo hapa kutetea udikteta kwa namna yoyote ile.
 
Umeletwa mada nzuri sana kama unaishi katika mawazo yangu.
Asante sana kwa hoja nzuri zenye nguvu na mifano halisi kiasi kwamba kila mwenye akili ameelewa matatizo ya hili balaa linaloitwa demokrasia tulilowekewa na mabeberu toka ulaya.
Shida ni namna gani tunaweza kubadili mfumo huu muovu ambao unazidi kuzoeleka pamoja na kwamba ni mgumu kutekelezeka na kurudi kwenye utawala wetu wa asili
(utawala wa watemi na machifu )!
 
Mnayo demokrasia?
Mko katika utawala wa kidemokrasia?
 
Kwa asilimia kubwa Africa haina demokrasia na bado inaongoza kwa umaskini na maendeleo duni.
Kule kutajwa tu kuwa ni Nchi zinazofuata Utawala wa kidemokrasia hata kama haki za kidemokrasia hazifuatwi tayari zimo kwenye matatizo kama alivyofafanua mleta hii mada !!
 
Kule kutajwa tu kuwa ni Nchi zinazofuata Utawala wa kidemokrasia hata kama haki za kidemokrasia hazifuatwi tayari zimo kwenye matatizo kama alivyofafanua mleta hii mada !!
Zikitajwa ni nchi za kidekteta kama hazina udikteta zinakuwa zimeondoka kwenye matatizo??
 
Kama udictator ndio unaamini unaleta maendeleo, basj africa ilapaswa kuwa mbele sana kimaendeleo maana ndio imejaza madictator..
 
Uzi wa kijinga sana huu.

Inaonekana mleta mada umezaliwa kuanzia mwaka 2000 na kuendelea.

Hivi hujui Tanzania kuanzia 1969 - 1992 tulikuwa hatufuati mfumo wa kidemokrasia kama tuliokuwa nao sasa?

Tuliendelea?

Tumeendelea zaidi baada ya kukumbatia zaidi demokrasia au tulivyokuwa kipindi hicho?

Huwezi kumkuta mtu ambaye amekimbia North Korea anakwambia mfumo wa kidikteta ni mzuri

Wewe unaleta hizi hoja zako hapa kwa sababu you are priviledged individual ambaye hujawahi kuishi kwenye udikteta.

Again huu uzi ni wa kipuuzi mno
 
Kidole kimoja hakivunji chawa, hapa ili kuendelea ikabidi Afrika karibia nzima iwe na madikteta na sio ilimradi tu madikteta ila madikteta wenye dira ya pamoja
 

Ni mwaka gani huo au at point in history ambao North Korea alikuwa better kiuchumi kuliko South Korea? Em tuelimishe?

Unaposema Korea zote mbili ziliendelezwa kwa udikteta unamaanisha nini?

Kama unamuongelea Park Chung Hee inaonekana huijui kabisa historia ya ile nchi and the science behind the miracle of Han RIver.
 
Unataka kusema sasa Tanzania inafuata demokrasia ?

Au unachanganya mabadiliko ya uendeshaji wa uchumi kwa kiasi ndio utofauti wa miaka ya enzi za mwalimu na sasa ?

By the way mabadiliko kadhaa ya uendeshaju wa uchumi hata China wakati wa Deng Xiaoping walifanya haina tofauti na wakati wa Mwinyi ila haimaanishi China waliachana na udikteta na kukumbatia demokrasia hata Tanzania haikuachana na udikteta na kukumbatia demokrasia.

Mfano nbona hiyo demokrasia iliyopo Zambia na Kenya hazijazifanya nchi hizo kuwa hata zaidi ya China ya kidikteta ?
 
Ametoa mfano wa nchi kama china na Korea! Na Mimi naongezea Japani ,Urusi na nchi za kiarabu zinazotawaliwa kifalme kama Saudi Arabia , Dubai , Kuwait , Emirates nk.
Hizo zote ni nchi tajiri kwa sababu huu upumbavu unaoita demokrasia hawataki kuusikia.
 
Sasa kwa nini bado Tanzania ni masikini kama haikuachana na udikteta na kukumbatia demokrasia??
 
Sasa kwa nini bado Tanzania ni masikini kama haikuachana na udikteta na kukumbatia demokrasia??
Umasikini wa Tanzania hauna mahusiano ya udikteta wala demokrasia ni masikini kwa sababu imejaza watu wa wajinga wajinga kama tu ilivyo nchi nyingi za Afrika.
 

We are not fully developed democracy.

Lakini at some point tulikuwa hatufuati demokrasia kabisa na HATUKUENDELEA. So whats your point?

Unachukulia mfano wa China. Lakini ebu pitia G20 pale angalia ni nchi ngapi ambazo zina udikteta zimeingia kwenye ile list.

Acheni kutetea udikteta kama haujwahi kuishi kwenye huo mfumo.
 
Mpaka miaka ya 60 NK ilikuwa mbele ya SK leta hiyo historia ya tofauti inayopinga udikteta na impact yake katika maendeleo ya SK.

Elezea hiyo historia ya SK unayoijua wewe hapa.
 
Kwa nini Nepal, Jordan, Lesotho, Cambodia na Myanmar sio nchi tajiri?
 


Usichanganye kutawaliwa kifalme na kukosa demokrasia

Pia Ungeendelea kuzitaja mkuu hizo nchi, NK ndo nini?

Uko tayari na mimi nikutajie nchi ambazo zina democracy ya kutosha na zina maendeleo makubwa kuliko hizo nchi ulizozitaja?
 
Sijui ni ujinga gani unaotaka kuhararisha kuhusu Tanzania.

Countries: Argentina, Australia, Brazil, Canada, China, France, Germany, India, Indonesia, Italy, Japan, Mexico, Russia, Saudi Arabia, South Africa, South Korea, Turkey, the United Kingdom, and the United States

Nchi kariba zote hapa zina historia mbaya ya udikteta na impact yake katika maendeleo yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…