Demokrasia ni mfumo mfu hamuwezi kufanikiwa duniani kwa sababu ya "Unafiki"

Demokrasia ni mfumo mfu hamuwezi kufanikiwa duniani kwa sababu ya "Unafiki"

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,683
Reaction score
14,060
Kwa wale wanao ona dunia itakuja kuwa chini ya utawala wa kidemokrasia kama ilivyo vitabuni basi hawapo sahihi wanaishi katika njozi.

Ili demokrasia iweze kufanikiwa duniani basi panapaswa kutokuwepo unafiki baina ya watu.

Unafiki ni kikwazo mojawapo cha asili cha sisi watu kinacho weka uzio wa kuja kuwepo kwa mfumo wa kidemokrasia.

Mfano kwa sasa mgogoro ulioshika kasi ni kati ya Ukraine na Russia, Israel na Palestine.

Wale wanaopinga dhuluma ya Russia kwa Ukraine wamegeuka kuwa waunga dhuluma za Israel dhidi ya Palestine.

Mfano wa karibu zaidi ni umoja wa ulaya na magharibi namna inavyo ichora picha Russia na namna inavyo ichora picha Israel ni mbingu na ardhi, namna inavyochorwa picha Ukraine na namna inavyochorwa picha Palestine ni mbali mbali.

Kwa namna hii utekelezaji wa demokrasia lazima ukutane na kikwazo cha kutokufanya kazi na kufanikiwa.

Demokrasia ili iweze kufanikiwa haitaki unafiki jambo ambalo ni gumu kwetu sisi watu.

Dunia inaongozwa kwa interests demokrasia haina nafasi yoyote mpaka sasa kuamuru mwenendo wa mataifa na duniani kwa ujumla.

Kama ambavyo ukomunisti umebaki ndoto kufanikiwa vivo hivyo demokrasia ni ndoto isiyoweza kufanikiwa kutokana na namna tulivyo watu kiasili.
 
Mfumo wa demokrasia katika kuongoza na suala zima la maendeleo haufai, hii inatokana na watu sisi kuongozwa na vitu kama vile tamaa, kujipendekeza, na unafiki.
 
Kwa hiyo ni mfumo gani unaona unafaa kama mbadala wa demokrasia na ukomunisti.
 
Hakuna mfumo uliokamilika katika suala zima la uongozi na utawala, ila mfumo wa demokrasia ndio mfumo wenye unafuu katika dhana nzima ya uongozi shirikishi.

Sema demokrasia ili ikamilike inahitaji mifumo imara na thabiti ya kuendesha nchi,hususani kuwepo na mihimili imara na inayojitegemea sio haya maigizo ya serikali ya ccm.
 
Back
Top Bottom