Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Ili kuishi comfortably kwenye mazingira ya kidemokrasia, ni sharti uwe mwenye uelewa na ufahamu wa kutosha kuhusu maana halisi ya demokrasia yenyewe. Zaidi sana yafaa, ufanye mazoezi ya mara kwa mara na ya kutosha, ya kushinda ama kushindwa si tu uchaguzi pekeyake, bali pia hata yale yenye ushindani nafsini mwako.
Demokrasia ni utamaduni wa kistaarabu wa kushindanisha maoni na mtazamo miongini mwa watu makini na mahiri, wanaokusudia kuwa viongozi katuka jamii fulani, juu ya mambo mbalimbali yenye faida na manufaa kwa jamii husika.
Ni fursa kwa aliekubalika katika jamii hiyo kutekeleza mipango yake iliyokubaliwa na jamii hiyo, huku yule ambae hakufanikiwa kwa wakati huo, kua sauti na mbadala wa mipango ambayo labada haifanywi vizuri na aliepewa ridhaa ya kutumikia jamii.
Demokrasia ni hiyari na ungwana wa kipekee sana na usio na shuruti katika kuchochea uwazi, uwajibikaji, usawa, haki, uhuru na maendeleo kwa jamii husika. Pakiwa na sura ya shuruti, maana ya demokrasia hupotea.
Tishio kwa anaye ongoza wakati huo, yafaa kuwa ni mipango mbadala mizuri, madhubuti inayokubalika na kuvutia kundi kubwa zaidi la walio wengi, na sio kulalamika na pengine kuzira, kususa au kugomea baadhi ya mambo, licha ya kwamba hiyo nayo ni sehemu ya demokrasia, lakini yenye tija kudogo sana na saa zingine hakuna tija kabisa...
Mipango mbadala makini ya wasio na ridhaa, huchochea mwenye dhamana kufanya bidii zaidi na hivyo kuchochea maendeleo. Maandamano, migomo, mihemko na fujo, hudidimiza maendeleo na kupelekea hali ngumu zaidi kwa kwa jamii nzima.
Uelewa na ufahamu duni wa masuala ya demokrasia huchochea kuzorota kwa ustaarabu, ungwana, ustahimilivu, kutokuelewana na kutoamainiana miongoni mwa jamii husika, na matokeo yake kuzorota kwa demokrasia, utoaji huduma kwa haki, usawa, uwazi, uhuru na kudumaza maendeleo katika jamii hiyo.
Ni vizuri kukubali kwamba vitu fulani huna, ujipange taratibu, ufanye bidii na polepole nawe uwenavyo, sio kulazimisha. Lakini pia kwenye ushindani kuna kushinda na kushindwa. Fanya mazoezi ya nguvu kukubali hali hizo mbili bila kua na visingizio. hakikisha umejiandaa vizuri kushindana.
Kwenye ushindani ukishinda shukuru, ukishindwa, kuwa muungwana mpongeze alieshinda, hukuridhika kua mstaarabu kuwasilisha malalamiko yako, ndiyo mila, desturi na utamaduni wa kidemokrasia