Demokrasia ya Magharibi na Muktadha Wetu

Demokrasia ya Magharibi na Muktadha Wetu

Amani Msumari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,830
Reaction score
972
Amani mtoto wa Msumari

Amani itawale kwenu.

Nimekaa na kutafakari sana kuhusu demokrasia. Jambo ambalo kwa hakika siwezi kulipinga ni ule ukweli kuwa, vyovyote vile, demokrasia ni jambo la muhimu sana kwenye jamii yoyote. Shida yangu iko kwenye dhana na maana ya demokrasia.

Dunia imepitia mambo mengi sana na hii ikazaa makubaliano ya kutenda mambo angalau kwa mfanano fulani (common practice). Hatahivyo, linapokuja suala la muktadha ni muhimu kuzingatiwa.

Hebu twendeni taratibu huku tukizitazama nchi ambazo zinajisema kuwa na demokrasia. Nchi za magharibi zipo kundi hili. Ukiangalia kwakina, utaona demokrasia yao imefungamanishwa na utamaduni, uchumi na mazingira yao.

Ni haki ya kila mtu kuwa huru kusema anachojisikia, hata kumdhalilisha Rais wa nchi, ni sawa tuu. Kwenye utamaduni wetu inaruhusiwa kumkosoa mtu mzima au kiongozi lakini kuna staha, miiko na taratibu za kufanya hivyo. Watu wetu wanaopiga kelele kuhusu demokrasia wanataka hii ibebwe kama ilivyo (copy and paste).

Ulaya na Marekani wanafanya hivyo, na sisi tufanye. HAPANA! uko wapi utamaduni wetu? Kwanini tulazimishe kuiga wengine? Kwetu, mtu mzima na kiongozi anautaratibu wake wa kumkosoa. Hatulazimiki kufanana nao.

Ulaya na nchi za magharibi huruhusiwi kumuadhibu mtoto wako. Ikifahamika, unachukuliwa hatua ikiwemo na kunyang'anywa mtoto kama itabidi. Wapiga chapuo wa demokrasia ya Magharibi wanataka haya kwetu. Copy & paste kama walivyotaka kulishughulikia janga la virusi vya korona.

Demokrasia ya magharibi inatambua haki za mtu ni pamoja na kufanya vile anavyojisikia kwenye mwili wake. Kama mwanaume ameona aolewe ni sawa tuu na sheria inamlinda na yuko huru kuonesha hivyo hadharani.

Napata taarifa kuwa huko ulaya na America ni kitu cha kwaida shuleni watoto wa jinsia moja kuwa wapenzi. Wazazi wao wapo, walimu wao wapo, serikali zao zipo na jamii zao zipo. Wenzetu hawa ndiko wanakokusudia kutupeleka.

Ukisoma historia, demokrasia inatajwa kuanzia Uingereza. Watu walikuwa wanapiga kura za wazi, baadae ikapendekezwa kura za siri ( secret ballots). Mchakato ulikuwa mrefu lakini ulioendana na mila, desturi na utamaduni wao. Sio lazima tufanane.

Huko magharibi kampeni zao za kisiasa sio tena kuleta maji, umeme, barabara, kujenga shule na hospitali. Wao wameshavuka huko. Sisi tunapambana kufika huko. Tunapambana huku tukilinda mila, desturi na taratibu zetu nzuri. Sio lazima tufanane.

Kama taifa, tunazo tunu zetu. Hizo ndio za kuangalia. Sisi hatusubiri kucheleweshwa na maadui wa ndani na nje. Sisi tumeamua kufa na kupona kufanya mambo yenye tija na maslahi kwa Tanzania na Afrika ya Leo na kesho.

Wenzetu wanaojitambua Kama akina Singapore, Taiwan, Russia, Malaysia,Japan n.k walishaliona hilo muda mrefu. Wanayo demokrasia waliyoitafsiri wao, kwaajili yao. Wananchi wao ni wazalendo kwelikweli. Wazalendo kwa vitendo.

Rejeeni mifano ya demokrasia iliyotafsiriwa na kulazimishwa huko Iraq,Libya, Tunisia, Egypt, Syria n.k.

Demokrasia yetu ni lazima iendana na mila, desturi na utamaduni wetu.

Amani Msumari
Tanga
 
Sasa hivi chini ya awamu ya tano ni ngumu sana kutofautisha uzalendo na ujinga. Na ndani ya awamu hii ya tano moja ya mafanikio yake ni kutengeneza wanafiki, waongo, hofu na wajinga wengi. Mleta uzi tafuta sehemu unayofit hapo.
Tindo hayo ni maoni yako. Mimi nimeeleza kile ninachoona ni sahihi huku nikijua fika watu Kama nyie mpo. Sina wasiwasi kabisa na komenti mbaya. Ninaelewa kuwa ninawapa hoja ambazo ni ngumu kuzijibu na hivyo mnaishia kuwa na hasira, mnapaniki na kutukana.

Badilikeni mazeee, tujenge hoja. Sio lazima kumgilizia mgombea flani ambaye mara zote anaongea kwa hasira na jazba na ukali mwingi. Moyo wake umejaa visasi na anataka kulipiza kwa watu wasiohusika. Looh! Watanzania tumemkataa.
 
Wazungu Sasa hivi wanajuta kupandikiza Demokrasia Yao Afrika na uarabuni

Mfano wakati madikteta akina Sadamm Hussein wabawala Iraki Iraki ilikuwa inawalika na hakukuwa na ugaidi walipomtoa Sadamm nchi haitawaliki hata vibaraka wao hawIwezi wanakimbia

Iran walimtoa mfalme wakidai Demokrasia matokeo yake Iran inatawaliwa kidini na mkono wa chuma wanatamani heri wangemwacha tu yule mfalme. Marekani na nchi za magharibi wanachukiwa sana Iran .Wakati kabla wakikuwa marafiki

Somalia dikteta Siad Barre aliiweza kutawala .Hakina msomali alileta fyoko pale nchi ilitulia na uchumi ulitulia walipomtoa nchi haitawaliki na Alshabab wameweka makazi!

Libya hivyo hivyo

SAsa hivi hawataki Tena kuhangaikia na Africa kuhusu utawala wameanza kuiga China ambayo wao hujali biashara tu hayo mengine wanaachia wananchi wenyewe wajiamulie
 
Amani Msumari,

Sasa hivi chini ya awamu ya tano ni ngumu sana kutofautisha uzalendo na ujinga. Na ndani ya awamu hii ya tano moja ya mafanikio yake ni kutengeneza wanafiki, waongo, hofu na wajinga wengi. Mleta uzi tafuta sehemu unayofit hapo.
Chadema mapenzi ya jinsia moja wameruhusu wabunge wa kike wameoana mgombea wao wa uraisi inasemekana Ni mpenzi wa jinsia moja na alihojiwa akasema anaunga mkono ushoga na usagaji je wewe tindo Ni upo kundi lipi la ushoga au usagaji?
 
Kwani kuna tatizo gani Tanzania hadi ukaamua kuandika haya? Naona umelalamika sana kama vile kuna kitu kinataka kutokea hapa nchini. Kuwa wazi ueleweke.
Tatizo ni watu kutaka tufanye kama wanavyofanya magharibi huko
 
Tindo hayo ni maoni yako. Mimi nimeeleza kile ninachoona ni sahihi huku nikijua fika watu Kama nyie mpo. Sina wasiwasi kabisa na komenti mbaya. Ninaelewa kuwa ninawapa hoja ambazo ni ngumu kuzijibu na hivyo mnaishia kuwa na hasira, mnapaniki na kutukana.

Badilikeni mazeee, tujenge hoja. Sio lazima kumgilizia mgombea flani ambaye mara zote anaongea kwa hasira na jazba na ukali mwingi. Moyo wake umejaa visasi na anataka kulipiza kwa watu wasiohusika. Looh! Watanzania tumemkataa.

..huu wasiwasi wa kulipiziwa kisasi unatokana na mabaya ambayo watawala wameyafanya.

..CDM na TL wamesema hakutakuwa na kulipiziana visasi. Wametoa kauli mbiu ya " no hate, no fear." vilevile wameahidi kuunda tume ya MARIDHIANO ndani ya siku 100 za uongozi wao ikiwa wananchi watawapa ridhaa.
 
Chadema mapenzi ya jinsia moja wameruhusu wabunge wa kike wameoana mgombea wao wa uraisi inasemekana Ni mpenzi wa jinsia moja na alihojiwa akasema anaunga mkono ushoga na usagaji je wewe tindo Ni upo kundi lipi la ushoga au usagaji?

Huna hoja, hapa naona unaanika nguo kavu tu.
 
Amani Msumari,

..umeorodhesha mambo usiyoyapenda ktk demokrasia ya magharibi.

..hebu sasa tueleze mambo gani unayoyapenda ktk demokrasia ya magharibi ambayo unadhani yanafaa kuigwa na waTz.

..mimi kwa upande wangu napenda uhuru wa mihimili ya mahakama na bunge. pia napenda uhuru wa vyombo vya habari.
 
Sisi timetafasiri maendeleo ni stend za mabasi,masoko,madaraja, mitaro and the like hata Kama wastani wa kipato Cha mtanzania ni shilingi milioni mbili kwa mwaka bado tumeendelea sana as long as tuna taa za barabarani Kila mkoa
 
Tatizo ni watu kutaka tufanye kama wanavyofanya magharibi huko
Ndo nauliza nini hicho kilichofanyika hapa kama western wanavyofanya? Toa mifano tukuelewe. Achana na maneno ya kijiweni, eleza mambo kisomi.
 
Mila gani unayoongelea wewe?

Huyo rais wako ndie anayeongoza kwa kupenda kutamka maneno yenye aibu kubwa mbele za watu! Mara anamwambia mwanamke anataka apanuliwe wapi?, mara barua ya mapenzi, mra barakoa kama chuchu za mwanamke, mara mnapenda kati kati...na ujinga wake mwingi kama huo!

Ingekuwa tuko serious na mila na desturi, hayu hafai kabisa kupewa nafasi tena ya uongozi, akakamue maziwa ng'ombe wake huko kwao!
 
Ndugu Amani usishangae kukutana na matusi, afadhali ungekutana na upinzani wa hoja zako kwa sababu naamini atakaepinga hoja zako atalazimika kuzipinga kwa hoja. JF imebadilika sana hasa kipindi hiki, imejaa watoto ambao uwezo wao wa kusoma, kuelewa hoja na kujenga hoja pinzani hawana. Kimbilio lao kubwa ni matusi na ushabiki usiokuwa na tija kwao as individual and as group. Hakuna ataeibuka kuzipinga hoja zako kwa hoja, hatimaye mjadala ukaanzia hapo, never!
 
Kwani kuna tatizo gani Tanzania hadi ukaamua kuandika haya? Naona umelalamika sana kama vile kuna kitu kinataka kutokea hapa nchini. Kuwa wazi ueleweke.
Hukumuelewa mtoa post. Kitu kitakachotekea hakuna anaejua, na kitakapotokea wapo watafurahia na wapo hawatafurahia. Maisha yataendelea kama kawaida.
 
Hukumuelewa mtoa post. Kitu kitakachotekea hakuna anaejua, na kitakapotokea wapo watafurahia na wapo hawatafurahia. Maisha yataendelea kama kawaida.
Mleta mada ni wale wanaopenda kuhadithia mambo ya kusikia vijiweni, not knowledgeable in what he was presenting hata kidogo.
 
Mleta mada ni wale wanaopenda kuhadithia mambo ya kusikia vijiweni, not knowledgeable in what he was presenting hata kidogo.
Unaweza kutoa ufafanuzi wako
Ndugu Amani usishangae kukutana na matusi, afadhali ungekutana na upinzani wa hoja zako kwa sababu naamini atakaepinga hoja zako atalazimika kuzipinga kwa hoja. JF imebadilika sana hasa kipindi hiki, imejaa watoto ambao uwezo wao wa kusoma, kuelewa hoja na kujenga hoja pinzani hawana. Kimbilio lao kubwa ni matusi na ushabiki usiokuwa na tija kwao as individual and as group. Hakuna ataeibuka kuzipinga hoja zako kwa hoja, hatimaye mjadala ukaanzia hapo, never!
Umeongea kitu kikubwa sana. Nimekuwa nikiongelea hilo mara zote
 
Mila gani unayoongelea wewe?

Huyo rais wako ndie anayeongoza kwa kupenda kutamka maneno yenye aibu kubwa mbele za watu! Mara anamwambia mwanamke anataka apanuliwe wapi?, mara barua ya mapenzi, mra barakoa kama chuchu za mwanamke, mara mnapenda kati kati...na ujinga wake mwingi kama huo!

Ingekuwa tuko serious na mila na desturi, hayu hafai kabisa kupewa nafasi tena ya uongozi, akakamue maziwa ng'ombe wake huko kwao!
Sawa, anapokosea aambiwe kwa ustaarabu ingawa hayo yote unayoyataja hayakuwa na muktadha huo unaousemea ww
 
Back
Top Bottom