Demokrasia ya Magharibi na Muktadha Wetu

Demokrasia ya Magharibi na Muktadha Wetu

Sisi timetafasiri maendeleo ni stend za mabasi,masoko,madaraja, mitaro and the like hata Kama wastani wa kipato Cha mtanzania ni shilingi milioni mbili kwa mwaka bado tumeendelea sana as long as tuna taa za barabarani Kila mkoa
Hili sidhani kama ni sahihi
 
Wazungu Sasa hivi wanajuta kupandikiza Demokrasia Yao Afrika na uarabuni

Mfano wakati madikteta akina Sadamm Hussein wabawala Iraki Iraki ilikuwa inawalika na hakukuwa na ugaidi walipomtoa Sadamm nchi haitawaliki hata vibaraka wao hawIwezi wanakimbia

Iran walimtoa mfalme wakidai Demokrasia matokeo yake Iran inatawaliwa kidini na mkono wa chuma wanatamani heri wangemwacha tu yule mfalme . Marekani na nchi za magharibi wanachukiwa sana Iran .Wakati kabla wakikuwa marafiki

Somalia dikteta Siad Barre aliiweza kutawala .Hakina msomali alileta fyoko pale nchi ilitulia na uchumi ulitulia walipomtoa nchi haitawaliki na Alshabab wameweka makazi!!!

Libya hivyo hivyo

SAsa hivi hawataki Tena kuhangaikia na Africa kuhusu utawala wameanza kuiga China ambayo wao hujali biashara tu hayo mengine wanaachia wananchi wenyewe wajiamulie
Kuna haja kubwa ya kujifunza kutoka kwenye nchi hizo
 
Definition ya demokrasia tunayotumia imekuwa imported,hatujawahi kuwa na definition ya demokrasia iliyoundwa Africa ndiyo maana inakinzana sana na tamaduni zetu.....tumeshachelewa kutengeza chetu
 
Definition ya demokrasia tunayotumia imekuwa imported,hatujawahi kuwa na definition ya demokrasia iliyoundwa Africa ndiyo maana inakinzana sana na tamaduni zetu.....tumeshachelewa kutengeza chetu
Bado hatujachelewa. Kelele zote hizi n kwasababu tunalazimisha kufanya Kama magharibi wafanyavyo
 
Bado hatujachelewa. Kelele zote hizi n kwasababu tunalazimisha kufanya Kama magharibi wafanyavyo
Uko sahihi, ningumu kwasasa.... Mtu anavyoona Trump anavyotukanwa hadharani analeta kama ilivyo na kusahau huku ni Africa
 
"Kuogopwa ni sifa na ada ya kiongozi dikteta"!-Mwalimu Nyerere!

Sasa mleta mada unaendekeza tumuogope Magufuli,kati yako na Nyerere nani yuko sahihi?Maana siku hizi mkikosolewa kwa kuambiwa ukweli mnaita matusi!
 
Amani mtoto wa Msumari

Amani itawale kwenu.

Nimekaa na kutafakari sana kuhusu demokrasia. Jambo ambalo kwa hakika siwezi kulipinga ni ule ukweli kuwa, vyovyote vile, demokrasia ni jambo la muhimu sana kwenye jamii yoyote. Shida yangu iko kwenye dhana na maana ya demokrasia.

Dunia imepitia mambo mengi sana na hii ikazaa makubaliano ya kutenda mambo angalau kwa mfanano fulani (common practice). Hatahivyo, linapokuja suala la muktadha ni muhimu kuzingatiwa.

Hebu twendeni taratibu huku tukizitazama nchi ambazo zinajisema kuwa na demokrasia. Nchi za magharibi zipo kundi hili. Ukiangalia kwakina, utaona demokrasia yao imefungamanishwa na utamaduni, uchumi na mazingira yao.

Ni haki ya kila mtu kuwa huru kusema anachojisikia, hata kumdhalilisha Rais wa nchi, ni sawa tuu. Kwenye utamaduni wetu inaruhusiwa kumkosoa mtu mzima au kiongozi lakini kuna staha, miiko na taratibu za kufanya hivyo. Watu wetu wanaopiga kelele kuhusu demokrasia wanataka hii ibebwe kama ilivyo (copy and paste).

Ulaya na Marekani wanafanya hivyo, na sisi tufanye. HAPANA! uko wapi utamaduni wetu? Kwanini tulazimishe kuiga wengine? Kwetu, mtu mzima na kiongozi anautaratibu wake wa kumkosoa. Hatulazimiki kufanana nao.

Ulaya na nchi za magharibi huruhusiwi kumuadhibu mtoto wako. Ikifahamika, unachukuliwa hatua ikiwemo na kunyang'anywa mtoto kama itabidi. Wapiga chapuo wa demokrasia ya Magharibi wanataka haya kwetu. Copy & paste kama walivyotaka kulishughulikia janga la virusi vya korona.

Demokrasia ya magharibi inatambua haki za mtu ni pamoja na kufanya vile anavyojisikia kwenye mwili wake. Kama mwanaume ameona aolewe ni sawa tuu na sheria inamlinda na yuko huru kuonesha hivyo hadharani.

Napata taarifa kuwa huko ulaya na America ni kitu cha kwaida shuleni watoto wa jinsia moja kuwa wapenzi. Wazazi wao wapo, walimu wao wapo, serikali zao zipo na jamii zao zipo. Wenzetu hawa ndiko wanakokusudia kutupeleka.

Ukisoma historia, demokrasia inatajwa kuanzia Uingereza. Watu walikuwa wanapiga kura za wazi, baadae ikapendekezwa kura za siri ( secret ballots). Mchakato ulikuwa mrefu lakini ulioendana na mila, desturi na utamaduni wao. Sio lazima tufanane.

Huko magharibi kampeni zao za kisiasa sio tena kuleta maji, umeme, barabara, kujenga shule na hospitali. Wao wameshavuka huko. Sisi tunapambana kufika huko. Tunapambana huku tukilinda mila, desturi na taratibu zetu nzuri. Sio lazima tufanane.

Kama taifa, tunazo tunu zetu. Hizo ndio za kuangalia. Sisi hatusubiri kucheleweshwa na maadui wa ndani na nje. Sisi tumeamua kufa na kupona kufanya mambo yenye tija na maslahi kwa Tanzania na Afrika ya Leo na kesho.

Wenzetu wanaojitambua Kama akina Singapore, Taiwan, Russia, Malaysia,Japan n.k walishaliona hilo muda mrefu. Wanayo demokrasia waliyoitafsiri wao, kwaajili yao. Wananchi wao ni wazalendo kwelikweli. Wazalendo kwa vitendo.

Rejeeni mifano ya demokrasia iliyotafsiriwa na kulazimishwa huko Iraq,Libya, Tunisia, Egypt, Syria n.k.

Demokrasia yetu ni lazima iendana na mila, desturi na utamaduni wetu.

Amani Msumari
Tanga
Wanataka kusodomalize, eti ndo demokrasia
 
Kuelekea maadhimisho ya miaka 21 ya kifo cha baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere, upi ulikuwa mtazamo wake Kuhusu demokrasia?
 
Back
Top Bottom