'DEMU' maana yake nini?

Ronn M

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2012
Posts
1,279
Reaction score
684
Utasikia oh, nataka nimwoe 'demu' wangu, mara oh naenda kulala kwa 'demu' wangu, mara 'demu' wangu anazingua, mara 'demu' wangu anataka pesa, hivi huyu 'demu' ni nani? Nini maana yake? Nini asili ya neno hilo? Hapa jamvini kuna 'mademu'? Nifafanulie!
 
Wewe pia unaweza ukawa demu.Wako wa aina mbili.
 
linatokana na neno la kiingereza DAMN...kazi kwako kufungua dikshenari.
 
It is from the word dame.. in american english it means a WOMAN...
 
Maana za maneno zinategemea jamii yanapotumika. Hata nchi moja ya continental europe demu ni mwanamke na haina maana mbaya.

Ila Tanzania hili neno limekuwa linatumiwa na wanaume wasiojiheshimu (wahuni) na linaonyesha jinsi huyo mwanaume anavyomchkulia cheap huyo anayemhita demu, hivyo wasichana wengi wanachukulia kama dharau kuitwa demu.

Nina rafiki yangu Mkenya yeye hapendi kabisa kusikia mtu anamwita rafiki yake shoga. Kwa wakenya neno shoga lina maana moja tu gay; wakati kwetu naweza kumuita rafiki yangu wa kike shoga yangu.

Utasikia oh, nataka nimwoe 'demu' wangu, mara oh naenda kulala kwa 'demu' wangu, mara 'demu' wangu anazingua, mara 'demu' wangu anataka pesa, hivi huyu 'demu' ni nani? Nini maana yake? Nini asili ya neno hilo? Hapa jamvini kuna 'mademu'? Nifafanulie!
 
oh, ok. . . . Im getting smthng here!
 
Kwa kweli nikijua mtu ananiita Demu hata kama anajitutumua na kujigamba kaniweza kwa jambo lolote. Kwa kweli hata kama nampenda na kumheshimu, kwa kweli hata kama simaanishi katika huo urafiki, akya Mungu walahi nikijua na nikisikia ndivyo anavyonitambulisha kwa rafiki zake kuwa mimi ni 'DEMU'.

Huo urafiki nitau-Restisha In Pisi. Kweli kweli kabisa I HATE IT!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…