Demu mwenye hashpapy ameniambia nije mtandaoni niwasifie Single mother ndio ainipe Uroda

Demu mwenye hashpapy ameniambia nije mtandaoni niwasifie Single mother ndio ainipe Uroda

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Anaandika, Robert Heriel Mtibeli
Chizi Mkarimu.

Niacheni niende zangu. Eeh!
Niende kula vya kwangu. Eeh!
Kalibonge kalibonge. Eeh!
Kalibonge kasichana....!
Leo tutaondoka kwa miondoko hiyo. Niite TaikonMaster A.K.A Chizi Mkarimu.

Hivi juzi nilikuwa zangu Makanya huko, nikiwa nimeenda kwenye Msiba wa Mjomba wangu. Sasa nikapitia Arusha.

Pale Arusha! Pale Arusha! Ayaa! Hili sio dukuduku jamani. Hii ni stori ya kweli lakini sio ya Msaga Sumu.

Nikiwa kwenye moja ya migahawa Pale Arusha Mjini. Mara anatokea mwanamke wa ajabu sana.

Mimi sijui walahi. Sijui kwa kweli nini kiliendelea Pale.
Hiyo sura mamaaaa! Nisipokufa mimi basi tena. Mtoto anasura nzuri kama sura ya vindege vya Peponi. Nilimtazama huku nikihisi roho yangu inatoka. Jamani mimi. Nimekwisha kabisa...

Mtoto alikuwa akija akiwa mbele yangu. Bunduki zimechomoza sio poah. Nywaa nywaa nywaa nywaa. Yaani nyonga zinavyoweweseka na kunipa magonjwa ya kale, magonjwa yaliyoua watu bila kutibiwa.

Sasa nilihisi Koo langu linakauka. Nikimeza mate hapa ingekuwaje. Mate hayatoki. Kinywa kiligeuka kikavu Tadhani ngozi ya Mamba. Nikanywa.

Mtoto akanipita, shingo nayo nikageuza. Mamaaa! Miye miyee miyee nifanyeje. Niende wapi jamani. Hashpapy! Hashpapy mtoto Hashpapy imesheheni. Hapana bhana! Sikubali!

Kwanza mapigo yangu yalianza kugonga kama kengele za kanisa katoliki. Ngele ngele ngele ngele, Robert angalia. Mtibeli usipandishe Sukari.

Nikasema liwalo na liwe. Acha nikajitose. Zile Hashpapy na bunduki hazitanipita nikiwa naangalia. Nipo tayari. Nipo hapa kulipa gharama.

Nikanyanyuka, nikamkabili. Kumbe kila mtu mule alikuwa akimuangalia huyo Malaika wa Chugga. Nikamfuata Pale alipokuwa amechukua siti.

Mnajua sisi Watibeli hatushindwi mambo madogo kama hayo.
Demu anaongea sauti nyembamba kama Mama Olie, Wema Sepenga. Jicho lilivyoning'inia daaah!
Nikajikaza kisabuni.

Demu kumbe ananichora ananijua fika. Inaonekana ni mtu wa mitandaoni huko.
Alinishtua alipotaja jina Mtibeli. Nikashtuka. Here! Huyu demu vipi.

Demu ananiambia yeye ni fans wangu. Ananifuatilia lakini ninamkera ninapowabatiza single mothers.

Demu anasema, anajua nimefuata namba ya simu. Nikamwambia sijafuata namba mimi. Nikamwambia nimefuata Hashpapy. Namba sina shida nazo. Ati anakenua na kucheeeka.

Akaniambia yeye hajiuzi. Nikamwambia hata mimi sipo kumnunua.
Nikamwambia Hashpapy napata au sipati. Ananiuliza hashpapy ni nini.

Nikamwambia acha ushamba. Mtoto mzuri, malaika wa Chugga unaleta mambo ya kireee.

Akaniamba oooh, kumbe wewe mtata. Mara oooh! Sikujua kwamba unajiamini hivi. Nikamwambia. Mimi sio kama najiamini. Mimi nimeona umebeba bunduki mimi nikaona nije nijilipue.

Sasa alinishangaza. Akaniambia; Nitakupa Hashpapy kwa sharti moja.
Nikamuuliza sharti gani.
Akaniambia niandike mtandaoni kwamba single mothers ni wazuri na vijana wawaoe.
Kisha atanipa Hashpapy.
Kama siwezi nimuache pale hataki usumbufu.

Nikamwambia sijawahi kukataza watu wasioe single mothers. Ila niliwaambia vijana waliochini ya miaka 45. Akasema haohao ndio niandike kwamba wake na wahakikishe wanaoa single mother kwani ndio wanawake wa dhahabu.

Moyo wangu ukaniambia. Andika. Kwani shi.ngapi. unajua moyo unauchu sana. Na ukitaka lake unakuwa na kisebengo.

Kweli imefikia hatua ninakosa uroda kisa mambo ya kuandika mtandaoni. Kweli? Kweli naadhibiwa hivi.

Kuna kiongozi mmoja nilimsikia juzi akisema oooh! Sijui tunaangalia mambo mnayopost mtandaoni. Kweli mpaka ninyi wa Hashpapy mnafanya hivyo.

Sasa sikieni.
Kazi zenu hatutaki.
Fursa zenu hatutaki.
Uroda wenu hatutaki.
Msitutishe.
Msitushinikize.

Tutasema ukweli ule tunaotaka kuusema. Masuala ya kuwekeana vikwazo mpaka vya uroda huko mmefika mbali lakini tutaenda hivyohivyo.

Nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Arusha.
 
🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴🥴
 
Mkuu Hapo kwenye sauti nyembamba ungemtoa wema sepetu ungemuweka diva the boss.
Nimepata msamiati mpya kindege Cha peponi.😀
Achana na uroda mkuu, Kuna jambo nimewai kukushirikisha PM na leo Tena nimekwama naweza kuja PM

Sijawahi msikiliza Diva Mkuu
 
Baada ya kuona yote hayo ukimbuke yule mrembo uliyemuacha pale nyumbani.

Hizo sura zipo tu!!
 
Mimi sijui walahi. Sijui kwa kweli nini kiliendelea Pale.
Hiyo sura mamaaaa! Nisipokufa mimi basi tena. Mtoto anasura nzuri kama sura ya vindege vya Peponi. Nilimtazama huku nikihisi roho yangu inatoka. Jamani mimi. Nimekwisha kabisa...
Watibeli kwa michepuko hamjambo Bora Sisi Wayebusi tunahesimu familia
 
Back
Top Bottom