Deni la Serikali ya Tanzania Lafikia Trilioni 98

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Ripoti ya mwezi ya Benki ya Tanzania inaonesha mpaka Julai 2024, deni la serikali lilifikia Trilioni 98.5 huku asilimia 67 ya deni hilo likiwa ni deni la nje sawa na dola za kimarekani Bilioni 24.69, ambazo ni Trilioni 66 za Kitanzania

Sekta iliyopokea mikopo mingi ni usafirishaji na mawasiliano ambapo ilipokea asilimia 25.9 ya mikopo yote ikifuatiwa na huduma za kijamii na mawasiliano iliyopokea asilimia 23.9 ya mkopo wote.

Kati ya mwaka 2020 na mwaka 2024, deni la ndani limeongezeka mara mbili kutoka Trilioni 15.1 mwaka 2020 mpaka kufikia Trilioni 32 mwaka 2024. Wakopeshaji wakubwa wa ndani ni Benki za Kibiashara (30.2%), Mifuko ya Hifadhi (27%), Benki Kuu( 23%), Kampuni za Bima (5.7%) na nyinginezo (14%).

IMG-20240926-WA0123.jpg
 
Anatupeleka Canaan Nchi itiririshayo asali na maziwa
Hahahahahaahahah

Zungumzia ongezeko la deni kwa kiasi hiki kikubwaa kwa.mda mfupi sanaa .
Hiyo Canaan ni Wana waisraeli pekee ndio wamefika huko.

Labda anatupeleka motoni kwa vitendo vya upotevu wa watu,kutekwa,Kuuwawa na kumwagiwa tindikali na vingine vilivyo kinyume na mpango wa Mungu
 
Ripoti ya mwezi ya Benki ya Tanzania inaonesha mpaka Julai 2024, deni la serikali lilifikia Trilioni 98.5 huku asilimia 67 ya deni hilo likiwa ni deni la nje sawa na dola za kimarekani Bilioni 24.69, ambazo ni Trilioni 66 za Kitanzania

Sekta iliyopokea mikopo mingi ni usafirishaji na mawasiliano ambapo ilipokea asilimia 25.9 ya mikopo yote ikifuatiwa na huduma za kijamii na mawasiliano iliyopokea asilimia 23.9 ya mkopo wote.

Kati ya mwaka 2020 na mwaka 2024, deni la ndani limeongezeka mara mbili kutoka Trilioni 15.1 mwaka 2020 mpaka kufikia Trilioni 32 mwaka 2024. Wakopeshaji wakubwa wa ndani ni Benki za Kibiashara (30.2%), Mifuko ya Hifadhi (27%), Benki Kuu( 23%), Kampuni za Bima (5.7%) na nyinginezo (14%).
downloadfile-1_edit_687965919538005.jpg
 
Mtaalamu kesho jukwaani ata kwambia deni letu ni dogo uki linganisha na USA, China ,Burundi kenya na canada aki malizia kwa kusema mbona hata north korea wana kopa
 
Back
Top Bottom