Kama ndiyo kusema ya kwamba pamoja na kukopa kote huko na hali bado ni hii. Sasa sijui kama tusingalikopa hali ingalikuwaje.
Akili yote ya viongozi wa sasa imeshikiliwa na majigambo kuhusu maendeleo ya vitu tu. Kupitia ktk picha hii ambayo nimembatanisha, na ambayo nimeipata humu humu jukwaani, imepata kunitafakarisha kwa kina kuhusu tofauti kubwa kati ya maendeleo ya watu na yale ya vitu, tena kwa kujumuisha kukua na uhimilivu wa deni la taifa.
Ni picha ambayo imebeba ujumbe wa kweli na kutoa maana kubwa sana kuhusu hali halisi ambayo inawakabili wanachi wengi hasa waishio maeneo ya vijijini., ambao habari zao hazisikiki na wala pia hawana mtu sahihi wa kuwaongelea kuhusu ya maisha yao. Hawa ndiyo ni wale waliotopea ndani ya lindi la ufukara na umaskini wa kutupwa licha ya majigambo na majisifu mengi ya awamu hii kuhusu maendeleo ya vitu.
View attachment 1501450