Deni la Taifa lafika TZS trilioni 91.03

Deni la Taifa lafika TZS trilioni 91.03

Mocumentary

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
806
Reaction score
2,049
Hadi Oktoba 2022 Deni la Taifa liliongezeka kufikia dola za Marekani milioni 39,006.1 (TZS trilioni 91.03) kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kati ya kiwango hicho, TZS trilioni 64 ni deni la nje, huku deni la ndani likiwa ni TZS trilioni 26.6.

----

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema deni la Taifa liliongezeka na kufikia Tsh trilioni 91, lakini hiyo haiifanyi Serikali kushindwa kukopa ili kuwaletea maendeleo wananchi wake.

“Deni letu ni TZS trilioni 91, bado tunakopesheka hatuna deni kubwa ukilinganisha na wengine na hatujaacha patakapoonekana hitaji la mkopo hatuna budi kukopa kuwaletea watanzania maendeleo cha kuzingatia ni mkopo wa mashart nafuu,” amesema Mwigulu Nchemba.

Hadi Oktoba 2022 Deni la Taifa liliongezeka kufikia dola za Marekani milioni 39,006.1 (TZS trilioni 91.03) kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kati ya kiwango hicho, TZS trilioni 64 ni deni la nje, huku deni la ndani likiwa ni TZS trilioni 26.6.
 
Nimeona hii habari huko tweeter. Mimeshika kichwa.. ndani ya mda mfupi sana awamu ya sita imekopa hadi imevunja record. Mama anaupiga mwingi.

---

Hadi Oktoba 2022 Deni la Taifa liliongezeka kufikia dola za Marekani milioni 39,006.1 (TZS trilioni 91.03) kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kati ya kiwango hicho, TZS trilioni 64 ni deni la nje, huku deni la ndani likiwa ni TZS trilioni 26.6.
https://twitter.com/swahilitimes/status/1601524551627612160/photo/1

Screenshot_20221210-140416_1.jpg
 
Hadi Oktoba 2022 Deni la Taifa liliongezeka kufikia dola za Marekani milioni 39,006.1 (TZS trilioni 91.03) kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kati ya kiwango hicho, TZS trilioni 64 ni deni la nje, huku deni la ndani likiwa ni TZS trilioni 26.6.

Swahili Times
Sawa tuu ilimradi watalipa
 
Kuna miradi inabidi imaliziwe, afe kipa afe beki na kwa kasi ya awamu iliyopita katika kukopa huku miradi mingi ikiwa haijaisha. Naamini hata ingeendelea bado mkopo ungeshoot tu kuja juu

Nafuu ambayo ingekuwepo ni moja tu, kudhibiti matumizi ya serikali kwenye kuajiri, posho, warsha na semina ambazo kwa kiasi flani zimerudi..

All in all ngoja nifunge bakuli langu maana hela ya kumlipa mtu aliyepona rungu la law school sina
 
Back
Top Bottom