sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,745
- 1,171
Takribani miaka minne toka Rais mrithi wa awamu ya tano B apokee kijiti baada ya kifo cha aliyekuwa Rais na mtawala wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Kipindi cha miaka minne ya mwisho ya Awamu ya Tano B chini ya Rais aliyepatikana kwa mujibu wa katiba,tumeona mambo mengi makubwa yanayostaajabisha,lakini kubwa kuliko ni kukua kwa deni la Taifa kwa kasi kubwa na weredi wa hali ya juu kunako simamiwa na waziri wa fedha!
Sanjari na kukuwa kwa deni la Taifa kwa kipindi kifupi cha miaka minne kwa 100% pia ongezeko kubwa la kasi ya uvunjwaji wa makusudi wa haki za binadamu nao umeongezeka kwa kasi kubwa kwa kipindi kifupi sana,hali iliyoichafua nchi kwa mara ya kwanza kwa kusemwa na mataifa mbalimbali duniani.
Ongezeko hili mpaka tarehe 13/06/2025 wakati inasomwa bajeti ya Taifa kwa mwaka 2025/2026 limefikia Tilioni 107/-,fedha ambazo hakuna Mtanzania atayegongewa kuulizwa, kama alivyowahi kutamka Waziri Mwenye dhamana na madeni.
Kwa mujibu wa waziri,deni letu ni himilivu,kwa maana bado tunakopesheka na tuna uwezo wa kulipa.
Suala si kukopesheka,suala hapa tunakopa ili iweje wakati miradi mingi imesimama wakati wakandarasi wamekimbia site kwa kutolipwa madeni yao.
Mradi wa bwawa la Mwl Nyerere ambalo mpaka sasa hatujui chanzo cha fedha za ujenzi zinatoka wapi kutokana na ndimi mbili ndani ya serikali moja. Ndimi moja inazungumzia fedha za ndani na ndimi ya pili fedha za wahisani.
Miradi imeendelea kuwa white elephants kupigia deal za wanufaika wachache waliokamatia fuko la hazina ya nchi,ilihali walipaji deni hilo ambao ni wananchi wakiendelea kutaabika ndani ya Taifa lao.
Ukitazama kipau mbele kwa Taifa ambacho kimsingi huenda ndicho kinaligharimu Taifa kwa matumizi makubwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu ambazo zimechangia matumizi yasiyo na tija kwa Taifa.
Mathalani unamkamata mtu Mbinga unamsafirisha kwa msafara wa magari si chini ya matano,mpaka Dar es Salaam,ukitumia mafuta,posho za safari na muda unatumika kufanya utalii wa utekaji wa ndani unaondolea sifa ya kuwa na utawala bora.
Unakamata Wanaharakati wa nchi jirani na kuwatesa,kisha unawasafirisha mpaka kwenye mipaka ya nchi zao na kuwatupa huko,bila kujali kuwa mnaathiri mahusiano ya kidiplomasia.
Gharama ya kuvizia wapinzani na kuwapoteza zimezidi kushamiri katika kipindi hiki kifupi cha deni la Taifa kupaa kwa kasi ya AVIATOR.
Miongoni mwa watekwaji ni Mdude Nyagali,Mbise,Soka na wengine wengi. Hali inayofikirisha huenda kipau mbele ni kuzimisha wapinzani wa kisiasa,kwa kuwa mauaji yote na utekaji wote huo serikali ipo kimya.
Angalia nguvu kubwa ya kudhibiti uhalali wa ibara ya 18.- (a) - (d) kwa kanisa la Ufufuo na uzima kufungiwa na gharama ya ulinzi wa kulilinda waumini wasiingie kusali kwa kuwa Askofu wake amepaza sauti ya kilio cha mwananchi asiye na sauti juu ya UTEKAJI ikiwa chini ya kodi za walipa kodi wa nchi hii.
Gharama zinazotumika kudhibiti upinzani na kuhakikisha mkakati wa kugharamia kufa kwa vyama vya upinzani vilivyoundwa kwa mujibu wa sheria namba 5 ya mwaka 1992,sura 258 kifungu cha 9(2) ni kubwa kuliko gharama za kuusimika mfumo wa vyama vingi kwa miaka zaidi ya 30.
Huduma za kijamii kama afya na elimu zimekuwa duni ikitokea huna fedha,maanake unachagua kufa au kuwa mjinga pamoja na kulipa utitiri wa kodi zisizo na tija zaidi kwa kuwa serikali imeamua kufanya biashara kwenye ustawi wa Taifa.
Ukiukwaji wa ukuaji wa deni la Taifa umeenda sambamba na matumizi makubwa ya nguvu kwa vyombo vya dola,ikiwa pamoja na kununua vidhibiti maandamano,mabomu ya machozi na silaha za moto dhidi ya wapinzani.
Unajiuliza pamoja na kuwa waziri wa fedha na madeni amedhihaki wananchi kwa kauli yake kuwa serikali haitamgongea mtu kulipa deni hilo la Tilioni 107/- ,amejisahaulisha kuwa serikali hii inawagongea mlango wananchi kwenye matumizi ya umeme kwa kodi ya kila mwezi,kwenye kodi ya ongezeko la thamani inayolipwa na mlaji!
Taarifa ya mkaguzi wa serikali inasema takribani Taslimu 571,000,000,000/- zimetumika kwenye matumizi yasiyo na tija,unajiuliza kwenye hiyo fedha Tilioni 107/- na hizi zimo!
Taifa limefikia kuaminishwa kuwa zintendwa mbali zinlongwa mbali,kinachozungumzwa na kufanyiwa budgeting hakina uhalisia,tuna tumia kingi kiholela kwa kukusanya ndogo.
Bajeti ya serikali inaingia mara mbili kwenye deni la Taifa,tufanye kwa miaka minne ya awamu ya Tano B baada ya Awamu ya Tano A,serikali ya Awamu ya tano B imekopa zaidi Tilioni 50,tujiulize kizazi hiki cha kuhoji,miradi yetu ina jumla ya thamani gani kulingana na deni hilo!
Uhimilifu wa deni ulioibukia kwenye Awamu ya tano A unatija gani kwa Taifa wakati mzunguko wa shilingi mtaani umefifishwa kwa kodi zinazopingana na kipato cha mlipa kodi!
Tumeona uholela wa matumizi yasiyo rasmi yenye kutumia kodi kubwa ya wananchi kwa TUME zinazoundwa bila suluhisho la matatizo kusudiwa.
Hivi karibuni Rais wa awamu ya Tano B aliunda tume ya haki Jinai,ambayo imetumia mamilioni ya shilingi,lakini maazimio ya TUME hiyo utekelezaji wake uko wapi zaidi ya ongezeko kubwa la wananchi kupotezwa kwenye mikono ya vyombo vya Dola!
TUME nyingi zimekuwa zikijirudia kuundwa pasi na suluhisho la uundwaji hizo TUME hali inayosababisha wananchi kukosa imani na serikali ya mama kama anavyopenda iwe hivyo.
Gharama za uundwaji vikundi vya kumtegemea mama vinapata wapi bajeti ya kuendesha taasisi hizo kwa lengo la kumsemea mama kama si matumizi mabovu ya fedha za umma!
Yapo mengi yanayotafakarisha,lakini tuna swali la kujiuliza,tuendele kuwa mtambo wa kutengeneza maisha binafsi ya watu wachache waliohodhi mamlaka ya wananchi kwa kura zetu au tuamue kujenga Taifa lenye nidhamu kwa matumizi na kudumisha msingi wa ibara ya 8 ya katibu wa Jamhuri ya Muungano!
Wakati wa kusimamia katiba juu ya mamlaka yetu ni sasa,hii itapingana na dhana inayojenga kibri na ulevi wa akili unaolewesha madaraka ya umma,unaofanywa na watawala wanaoamini vikundi vya kumsemea vina nguvu kubwa kuliko mamlaka ya kikatiba chini ya ibara ya 8.
Maamuzi yetu ya msingi ndiyo yatarudisha uvumilivu uliopotea utakaowezesha mchakato wa kuipata amani iliyoondoka na muasisi wa Taifa hili la Tanzania lililoimeza Tanganyika.
Maamuzi hayo ndiyo chachu ya kuirudisha Tanganyika iliyojificha kwenye koti la Muungano ambao unalindwa kwa gharama kubwa kwa kuwa ndiyo uchochoro wa kupoteza rasilimali zetu.
Mungu ibariki Tanganyika,Mungu wabariki Wahanga wa mfumo kandamizi.