Denmark wagundua Dawa ya UKIMWI/HIV/AIDS, Kusambazwa punde, ARV basi

Ambiente Guru

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Posts
2,605
Reaction score
1,085
Gazeti la The Telegraph la Uingereza 27/04/2013 limeripoti kuwa Dawa ya kutibu Ukimwi itapatikana miezi michache ijayo. Ugunduzi umefanywa na wanasayansi watafiti wa Denmark. Tiba hii itasambazwa kwa kiasi kikubwa na kwa gharama ambayo waathirika na serikali zao wataimudu.

Kwa sasa wako kwenye majaribio ya mwisho. Virus vinavyosababisha UKIMWI vitaweza kuondolewa toka mwilini na kuangamizwa kabisa na kuondokana na kutumia ARV mara kwa mara.

Vyanzo: http://www.telegraph.co.uk/health/healthnews/10022664/Scientists-on-brink-of-HIV-cure.html

Cure for Aids 'possible' says Nobel prize-winning scientist who helped discover HIV - Telegraph[




Scientists on brink of HIV cure Researchers believe that there will be a breakthrough in finding a cure for HIV "within months".

With modern HIV treatment if medication is stopped, HIV reservoirs become active and start to produce more of the virus Photo: Alamy

 


jui!kama ni ukweli ashukuliwe sana mungu wetu!
 
Maelezo hayajafafanua ni lini ila yamesema ni ndani ya miaka minne. Cha msingi ni kuchukua hatua ziwezekanazo kwa sasa. Heri kinga,kuliko tiba.
 
si na Marekani waligundua?? yao ilifikia wapi?

chezea wazungu wew.. they are happy when we are sad at burial ceremonies
 


Wapi wameandika "miezi michache ijayo"?
 
Wako kwenye mchakato lakin hawajawa na uhakika wa dawa hyo kutibu HIV!
 
ikipatikana hakika wazinzi wataandamana kushangilia sipati picha machangu watakavyofurahia maana wale wateja wanaopenda kununua ila wanaogopa ngoma sasa watajitosa,ila pia wapo ambao vibarua vitaota nyasi,maana kwa gonjwa hili watu kibao wamelamba ajira kupitia ngo.
 
wanatamani waafrica tupungue'itachukua muda mrefu sana
 
Naona umetia chumvi hiyo habari...... Kwa kifupi habari ni:
Danish scientists are expecting results that will show that "finding a mass-distributable and affordable cure to HIV is possible".
Ni sio kama wewe ulivyoandika kwenye heading yako.
 
Maelezo hayajafafanua ni lini ila yamesema ni ndani ya miaka minne. Cha msingi ni kuchukua hatua ziwezekanazo kwa sasa. Heri kinga,kuliko tiba.
Scientists on brink of HIV cure
Researchers believe that there will be a breakthrough in finding a cure for HIV "within months".
 
Naona umetia chumvi hiyo habari...... Kwa kifupi habari ni:
Danish scientists are expecting results that will show that "finding a mass-distributable and affordable cure to HIV is possible".
Ni sio kama wewe ulivyoandika kwenye heading yako.
Scientists on brink of HIV cure
Researchers believe that there will be a breakthrough in finding a cure for HIV "within months".
 
Tumewazoea hawa Wazungu! Hawana nia nzuri na Waafrika hata kidogo,, tangazo kama hili, si mara yao ya kwanza!!
 
dawa ilishapatikana ni kung'atwa na nyuki mwili mzima ile sumu yao inauwezo wa kuvidhoofisha na kuviua vijidudu vya ukimwi

hivyo wazinzi mjipange kukutana na mizinga ili mpone
 
My friend, Tatizo la lugha limekukumba... Kichwa cha habari hakiendani na kilichoandikwa. Usikurupuke!
 
washenzi sana hawa, walikua wanatengeneza soko, sasa kuna wagonjwa wengi wa kununua dawa wanadai wamegundua,
 
duu kazi imekwisha sijui itafika mbali mpaka bongo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…