Dennis Kitambi mchambuzi bora kuliko wote wa mpira

Inawezakuwa ila wapo tatizo hawapata fursa luningani
 
Hapa umenena aisee ila wakati mwingine kibongobongo wanasaidia si unajua simulizi ni kipaji
 
Kuwa simba kuna tatizo gani mkuu?!

Hamna tatizo, jeff Leah nahisi ni Simba, Mayay ni Yanga kila mtu anajua hilo! Kaijage atakuwa ............!
Ila hamna tatizo kuwa Simba, Yanga au Azam au timu yoyote ile!
Kitambi nilimsoma kuwa ni Simba mechi ya Prison na Yanga, alilalamika sana kuhusu magoli ya kizembe ya kipa wa prisons!
 

Usipotembeleatembelea nyumba za watu wengine Ni rahisi kusema Mama/mke wangu ndie mpishi bora dunia mzima! Hajawahi kutokea! Tafakari
 
Usipotembeleatembelea nyumba za watu wengine Ni rahisi kusema Mama/mke wangu ndie mpishi bora dunia mzima! Hajawahi kutokea! Tafakari

Nimezungumzia wachambuzi wa TZ...
nafikiri hujaelewa hilo
 
Reactions: MTK
Alishindwana na management ya ndanda kwa sababu ya Ndumba. Ye anaamini katika juhudi na vipaji zaidi, viongozi wanaamini katika uchawi zaidi. Wachezaji wanapigwa chale zaidi ya kufanya mazoezi halafu wanategemea kushinda. Juhudi kubwa alizokuwa anazifanya ni kuhakikisha wachezaji wanajiamini na kutumia vipawa na uwezo wao na hakuwa anataka waamini ulozi. Viongozi wakamkataa. Ni kocha ambaye anapenda sana style ya ufundishaji wa Mourinho. .
 
Alishawahi kuwabana wachezaji kwenye mazoezi mpaka wakakosa muda wa kupelekwa makaburini kuchanjwa chale. Management haikufurahishwa.
 
Majungu pembeni, Kitambi anajua mpira wa bongo kuliko wachambuzi wengi wa bongo, na usisahau ndio kaipandisha Ndanda. Mambo ya imani ya nguvu za giza ni uongozi ni suala la uongozi.
kwa hiyo kazi yake ilikuwa ni kuipandisha ndanda ligi kuu tu basi?!!! wala sio chuki binafsi kwenye ukweli lazima tuseme, inawezekana anajua mpira wa bongo akiwa studio na si kwenye field, tunachoongelea hapa ni hicho, kwani wakiwa studio hadi wanamkosoa mourino, wenger, ancelot na wote unaowajua wewe, makocha wakubwa duniani!! eti pale alikosea angetumia formation hiii!!! kweli jamani?? hao wengine kina shafi, kitenge hatujawahi kuwaona ki coach lakini ni wale wale tu, Huyu wa ndanda ukiona anavyo iponda timu ya ndanda huwezi amini kama ndiye aliyefanya usajili huo!! huu si unafiki.
 

Duh au wewe ni kiongozi ndanda?
 

Sasa ulitaka aisifie Ndanda hata pale inapovurunda kwa sababu tu alishawahi kuifundisha au kusajili wachezaji?
 
Usipotembeleatembelea nyumba za watu wengine Ni rahisi kusema Mama/mke wangu ndie mpishi bora dunia mzima! Hajawahi kutokea! Tafakari

Wachambuzi wa Tz na hasa wa soka la bongo, tumewaona wangapi TBC, star Tv, Azam, Itv wapo wa kumwaga!
Unataka atembee tembee wapi???
 

Kumbe unaongea tuu ili mradi!
Townsend wa Skysports kashinda mataji gani? lakini anawakosoa kina Mourinho na wenzake utadhani wao ndo wajuzi!
Huyu kijana Kitambi anaujua mpira, naona unasahau hata Mourinho na kina ancellot wameshawahi kukumbwa na fagio la chuma mara kadhaa!! Sasa kuachishwa kazi kwake Ndanda, sio kwamba anaujua mpira wa studio tuu, elewa kitu kimoja, unapoongea FIELD, kaipandisha timu toka daraja la kwanza na wachezaji wake aliowakusanya ndio wanaojitahidi sasa hivi na hiyo ndanda! Ni mwanzo ulikuwa mgumu ktk mazingira mapya ya ligi kuu, viongozi wa ndanda wakakosa subira! Simple!
Sasa kama kocha wa sasa anapokosea formation na timu kufanya vibaya ya Ndanda ulitaka aifagilie tu kisa ali-assemble wachezaji yeye? Mpira hauko hivyo!
 
Nimezungumzia wachambuzi wa TZ...
nafikiri hujaelewa hilo

AAh bana eeh; usiogope neno Dunia nzima; the whole world is a small village today! OK basi naondoa neno "Dunia nzima" naweka Daresalaam ili nipuinguze geographicla size; tatizo ni kwamba bado metaphor yangu itabaki na mantiki ile ile tu ! kwamba "usipotemebea tembea kwa majirani utafikiri mama au mkeo ndie mpishi bora zaidi Duniani"?!
 
Wachambuzi wa Tz na hasa wa soka la bongo, tumewaona wangapi TBC, star Tv, Azam, Itv wapo wa kumwaga!
Unataka atembee tembee wapi???

Alah; sample yako imeishia hapo tu?! just 4 media houses only?! tembea tembea bana panua sample yako ya uchambuzi!! uachie ubongo wako ujivinjari!!
 
Alah; sample yako imeishia hapo tu?! just 4 media houses only?! tembea tembea bana panua sample yako ya uchambuzi!! uachie ubongo wako ujivinjari!!

Wataje ambao wewe unawaona ni bora
 
Reactions: MTK
Hapana; Who am I to burst your bubble?!

The bubble ipo kwenye imagination zako
nimeleta hii thread nikijua kabisa wapo watu JF watachangia frpm both angles
watakaopinga na kutaja wengine i expected that.....
this is JF where we dare to talk openly...
 
Reactions: MTK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…