PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini mwaka 2020/25, Deo Mwanyika (CCM) leo Julai 01, 2025 amechukua Fomu ya kuwania Ubunge awamu ya pili katika Jimbo la Njombe Mjini.
Mwanyika amechukua Fomu hiyo katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Njombe ambapo amekabidhiwa Fomu na Katibu wa CCM wilaya ya Njombe Bi. Mariamu Kreti.
Akizungumza na Kings Fm muda mfupi baada ya kuchukua Fomu hiyo, Deo Mwanyika amesema lengo la kurudi kuomba ridhaa ya kugombea tena katika awamu ya pili ni kuendelea kuwatumikia Wananjombe na kuendeleza pale alipoishia.