Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, ametoa onyo kwa Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Songea hadi Masasi kupitia Tunduru kilovoti 220 na kumtaka Mkandarasi huyo kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mradi ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo Julai 22, 2026, Mhe. Ndejembi amesema Serikali haitakuwa tayari kuona miradi ya kimkakati inayogusa maisha ya wananchi ikicheleweshwa bila sababu za msingi.