Depositors alarmed as ATM theft rises sharply


Asante sana mkuu kwa kutupa elimu mujarabu. Nadhani jambo la msingi ni kila mteja kuwa makini na fedha zake na kuhakikisha kwamba majizi hayakaribii kwenye kibubu chake. Mimi huwa siamini mabenki ya Tanzania. Kila nikienda kudraw pesa ni lazima niandike kwenye diary kiasi kilichobaki kwenye akaunti ili kama nikirudi siku nyingine kwenda bank nikute zimepungua nikinukishe. Siwezi kukubali wapuuzi wachukue fedha zangu kibwege....fedha ninazozitafuta kwa akili na maarifa halafu wapuuzi flani from no where waje watie mkono wao pale? Sikubali kamwe.
 
account yoyote ambayo ikigundulika haifanyiwi reconciliation ni fursa

Ni kweli mkuu....kuna akaunti za watu fulani zilikuwa dormant kwa muda mrefu, sasa wafanyakazi wa KBC Bank wakataka kuiba fedha za benki (sio za wateja) kupitia akaunti hizo. Wakajaza milioni 25 kwenye akaunti ya mfanyakazi mwenzetu ili baadaye wakazikombe kwa manufaa yao binafsi. Sasa ikatokea bahati kabla hawajazikomba yule jamaa mwenye akaunti akaenda akakuta kuna mamilioni yamejazwa kwenye akaunti yake. Akakomba fedha zote na kutokomea kizani!!! Sasa hivi yuko UK anakula maisha baada ya kuhitimu chuo kwa kutumia fedha 'alizozawadiwa' na wafanyakazi wa benki.

Kuna mwingine naye alijaziwa mamilioni ya fedha kwenye akaunti yake ya KBC...akaenda akakomba milioni 10...alipogunduliwa wakawa hawana namna ya kumuadhibu, ikabidi wawe wanamkata kidogo kidogo kwenye mshahara hadi pesa zitakapoisha (na kumbuka hakuna riba kwa kuwa huu haukuwa mkopo na wala hakukuwa na makubaliano yoyote ya kuwekewa fedha kwenye akaunti yake). Alipokomba hizo fedha akajinunulia usafiri wake muruwa...akala maisha kwa kwenda mbele!! Hii inazidi kudhihirisha jinsi wafanyakazi wa benki walivyo MAFISADI. So ni muhimu kuwa makini na hawa watu hata zaidi ya cyber criminals wengine.
 
Kwa huu wizi wa kutisha unaotokea kwenye mabenk naona hii ndio itakuwa solution. Unatafuta mtungi wako mkubwa mzuri unauchimbia nyumbani kwako, siku hizi wengine hata safe pia zenye nafasi ya kutosha tu huziweka majumbani mwao.


Wakijua zipo utajuta
 
Kama muhusika ana tabia ya kujipiga kifua mtaani kwamba yeye anazo nyingi sana basi wenyewe wataenda kumgongea ili awape kilicho chao na hata wanaweza kuchukua uhai wake.

Wakijua zipo utajuta
 
Mkuu, umeishawahi kusoma zile terms and conditions, zile zenye maandishi madogoooo ukurasa wa nyuma

uko sahihi ... ila sio bank zote unapata hayo ... kuna banks wanakwambia jaza form ... kinachofuatia unazungushwa tu siku ya kuja kuchukua kadi ....fees na vingenevyo unavijua juu kwa juu

kama umewahi kukaa nje hasa marekani na uingereza utajua namaanisha nini ... mteja anapewa mfuko wa documentations zote kwa kujisomea, kuweka record kuhusu uendeshaji wa account yake .... bongo banks nyingi hazifanyi hili!
 
Reactions: BAK
Wafanyakazi wa bank baadhi yao hujihusisha na wizi wa fedha za wateja wao na wizi mkubwa tu wa mapesa chungu nzima.
You are right rafiki......
Nilishawahi chezewa huo mchezo, mwaka huu huu. Nilikuwa napokea tu sms kuwa nimedraw kwenye ac yangu ya $ wakati hata hapo bank sijafika. Nikawapigia simu kuwaulizia wakairudisha, yaani nilishangaa sana. Nikajua ulikuwa mchezo wa wafanyakazi maana nilikuwa sijafanya transaction kwa karibia mwaka mzima wakaamua watest zari kama mwenye ac anaexist au la. Hii ni tabia mbaya sana kwa hawa wafanyakazi wa bank
 
Pole sana rafiki, ulikuwa na bahati kwamba pesa walizozichukua walirudisha mara moja, wengine huwachukua miezi chungu nzima kuwathibitishia bank kwamba transaction iliyofanyika katika bank accounts zao wao hawakuhusika, na wengine pesa zao huishia kupotea.

 
Inawezekana sababu nilipiga simu as soon as sms ya transaction ilipoingia kwenye simu yangu.......
na nikapiga mkwara wasipoirudisha hiyo siku, kesho yake naenda ofisini na barua, na mtu atapoteza kazi. wakaona isiwe shida, wakarudisha.....
All in all, kama unavyosema rafiki, inawezekana ilikuwa bahati yangu tu ikarudi.
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…