Depositors alarmed as ATM theft rises sharply

Depositors alarmed as ATM theft rises sharply

Nimesoma comments za wadau hapo juu, kwa kweli security ya banking tanzania bado ina walakini. Challenges ambazo mimi nimeziona mara nyingi ziko pande zote .... bank na mteja .... ufunguzi wa account na uendeshaji


Kama kuna ambayo yanafanyika, hongera .... kama kuna yanayoweza kuongezwa katika ushauri kwa wateja wasilizwe sana itasaidia mkiongezea. Mimi nimeona haya machache kwa uzoefu na banks tatu tofauti tanzania:


Ufunguzi wa account:
Kuna baadhi ya banks zina msururu mrefu wa kufungua account pamoja na watu wengi wanaoshika file lako .... sina uhakika kama kukitokea tatizo wanaweza kutrace wote. Hapa nashauri wahusika wote watambulike na ikiwezkana mtu mmoja atoe maelezo yote ili mteja akija kufungua account anakuja na vithibitisho vyote sio njoo kesho kuna kitu umesahau. Wateja wapewe checklist ya vitu vya kukamilisha.

Challenge nyingine ni banks zitafute mbinu tofauti za kumfikishia mteja card yake ya bank na password/pin numbers bila kupitia kwa wale waliomfungulia account. Hii itapunguza wizi wa personal information.

Access ya account:
Nashauri access ya account iwe limited kwa wafanyakazi wachache wa bank, na mtu akiingia kwenye account ya mtu ionekane flani aliingia na ajieleze alikua akifanya nini kwa muda huo

Wahudumu wa kudeposit na kuwithdraw:
Hapa baadhi ya banks zinaboa, hawampi mteja privacy yake. Unakuta unahudumiwa anakuja mtu mwingine kuchomeka kikaratasi pembeni na kuongea na mtu anayekuhudumia

Mitambo ya ulinzi
CCTV camera na other online security details ziwe za hali ya juu na vifanye kazi muda wote, visingizio vya umeme umekatika au camera ilikua haifanyi kazi iwe sababu ya mtu kufukuzishwa kazi kwa uzembe.

Uajiri wa watumishi
Nashauri kuwepo na umakini kwenye uajiri ... hapa ni pamoja na references na addresses zake. Banks zijiridhishe na wanayemuajiri wamjue kiundani ili lolote likitokea wajue wapi pa kumdaka kuanzisha kesi.


WATEJA
Card ya bank, Cheque book, Monthly Bank statement, Online access, Terms and conditions (fees, etc) za account .... hivi sio hisani hakikisha unavielewa (kuwa na copy ya any documentation) na unalazimisha kuwa ni haki yako kupewa. Kucheki balance mara kwa mara huwa inapunguza sana wizi mdogo mdogo wa wafanyakazi wa banks.


SERIKALI
Wawe na sheria kali za kudhibiti hizi banks pamoja na insurances kwa wateja .... kwa mfano banks nyingi marekani mteja yuko guaranteed up to $250,000 ya deposit yake kwa any loss ambayo hajasababisha mteja. Hii inazifanya banks kuwa makini sana kwenye usalama wa pesa ya mteja









Hizi nimezikuta sehemu, zinaweza kusaidia kupunguza wizi wa mtandao

These are the essential tips to protect yourself:


- Don't ever give out your personal information to strangers.



- Never use personal details as passwords - such as birthdays of loved ones or your pet's name.



- If you're asked for personal details when signing up with a company, use a random word you'll remember instead. Just because they ask for your mother's maiden name doesn't mean you have to give her actual one.



- Don't do online banking in a public place, such as a cafe. By using wireless you expose yourself to the risk of fellow customers being able to hack into your account.



- Never write down your Pins and passwords in a book, even if it's locked in a filing cabinet. You may think that it's safe, but don't under-estimate criminals.



- Make your password as long and as random as possible. Modern software allows a computer to make 1,000 guesses a second - meaning that a random five-letter password can be cracked in four hours. But it would take a life- time for criminals to work out a 20-letter password.



- Get yourself an online mentor if you're not confident on the internet. This could be a close relative or friend. You shouldn't give them your bank details, but they can help you decide if something isn't right.



- If your gut feeling is that something is not right, contact the police and your bank. If you've been called by suspected criminals on your home phone, call from a different line.



- Never reply to emails that appear to be sent from your bank and, in particular, never give them your passwords or log-in details.



- If your computer is behaving strangely - windows keep popping up or strange internet pages are appearing - then don't log in to your bank account. It may be infected.





Asante sana mkuu kwa kutupa elimu mujarabu. Nadhani jambo la msingi ni kila mteja kuwa makini na fedha zake na kuhakikisha kwamba majizi hayakaribii kwenye kibubu chake. Mimi huwa siamini mabenki ya Tanzania. Kila nikienda kudraw pesa ni lazima niandike kwenye diary kiasi kilichobaki kwenye akaunti ili kama nikirudi siku nyingine kwenda bank nikute zimepungua nikinukishe. Siwezi kukubali wapuuzi wachukue fedha zangu kibwege....fedha ninazozitafuta kwa akili na maarifa halafu wapuuzi flani from no where waje watie mkono wao pale? Sikubali kamwe.
 
account yoyote ambayo ikigundulika haifanyiwi reconciliation ni fursa

Ni kweli mkuu....kuna akaunti za watu fulani zilikuwa dormant kwa muda mrefu, sasa wafanyakazi wa KBC Bank wakataka kuiba fedha za benki (sio za wateja) kupitia akaunti hizo. Wakajaza milioni 25 kwenye akaunti ya mfanyakazi mwenzetu ili baadaye wakazikombe kwa manufaa yao binafsi. Sasa ikatokea bahati kabla hawajazikomba yule jamaa mwenye akaunti akaenda akakuta kuna mamilioni yamejazwa kwenye akaunti yake. Akakomba fedha zote na kutokomea kizani!!! Sasa hivi yuko UK anakula maisha baada ya kuhitimu chuo kwa kutumia fedha 'alizozawadiwa' na wafanyakazi wa benki.

Kuna mwingine naye alijaziwa mamilioni ya fedha kwenye akaunti yake ya KBC...akaenda akakomba milioni 10...alipogunduliwa wakawa hawana namna ya kumuadhibu, ikabidi wawe wanamkata kidogo kidogo kwenye mshahara hadi pesa zitakapoisha (na kumbuka hakuna riba kwa kuwa huu haukuwa mkopo na wala hakukuwa na makubaliano yoyote ya kuwekewa fedha kwenye akaunti yake). Alipokomba hizo fedha akajinunulia usafiri wake muruwa...akala maisha kwa kwenda mbele!! Hii inazidi kudhihirisha jinsi wafanyakazi wa benki walivyo MAFISADI. So ni muhimu kuwa makini na hawa watu hata zaidi ya cyber criminals wengine.
 
Kwa huu wizi wa kutisha unaotokea kwenye mabenk naona hii ndio itakuwa solution. Unatafuta mtungi wako mkubwa mzuri unauchimbia nyumbani kwako, siku hizi wengine hata safe pia zenye nafasi ya kutosha tu huziweka majumbani mwao.


Wakijua zipo utajuta
 
Kama muhusika ana tabia ya kujipiga kifua mtaani kwamba yeye anazo nyingi sana basi wenyewe wataenda kumgongea ili awape kilicho chao na hata wanaweza kuchukua uhai wake.

Wakijua zipo utajuta
 
Mkuu, umeishawahi kusoma zile terms and conditions, zile zenye maandishi madogoooo ukurasa wa nyuma

uko sahihi ... ila sio bank zote unapata hayo ... kuna banks wanakwambia jaza form ... kinachofuatia unazungushwa tu siku ya kuja kuchukua kadi ....fees na vingenevyo unavijua juu kwa juu

kama umewahi kukaa nje hasa marekani na uingereza utajua namaanisha nini ... mteja anapewa mfuko wa documentations zote kwa kujisomea, kuweka record kuhusu uendeshaji wa account yake .... bongo banks nyingi hazifanyi hili!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wafanyakazi wa bank baadhi yao hujihusisha na wizi wa fedha za wateja wao na wizi mkubwa tu wa mapesa chungu nzima.
You are right rafiki......
Nilishawahi chezewa huo mchezo, mwaka huu huu. Nilikuwa napokea tu sms kuwa nimedraw kwenye ac yangu ya $ wakati hata hapo bank sijafika. Nikawapigia simu kuwaulizia wakairudisha, yaani nilishangaa sana. Nikajua ulikuwa mchezo wa wafanyakazi maana nilikuwa sijafanya transaction kwa karibia mwaka mzima wakaamua watest zari kama mwenye ac anaexist au la. Hii ni tabia mbaya sana kwa hawa wafanyakazi wa bank
 
Pole sana rafiki, ulikuwa na bahati kwamba pesa walizozichukua walirudisha mara moja, wengine huwachukua miezi chungu nzima kuwathibitishia bank kwamba transaction iliyofanyika katika bank accounts zao wao hawakuhusika, na wengine pesa zao huishia kupotea.

You are right rafiki......
Nilishawahi chezewa huo mchezo, mwaka huu huu. Nilikuwa napokea tu sms kuwa nimedraw kwenye ac yangu ya $ wakati hata hapo bank sijafika. Nikawapigia simu kuwaulizia wakairudisha, yaani nilishangaa sana. Nikajua ulikuwa mchezo wa wafanyakazi maana nilikuwa sijafanya transaction kwa karibia mwaka mzima wakaamua watest zari kama mwenye ac anaexist au la. Hii ni tabia mbaya sana kwa hawa wafanyakazi wa bank
 
Pole sana rafiki, ulikuwa na bahati kwamba pesa walizozichukua walirudisha mara moja, wengine huwachukua miezi chungu nzima kuwathibitishia bank kwamba transaction iliyofanyika katika bank accounts zao wao hawakuhusika, na wengine pesa zao huishia kupotea.

Inawezekana sababu nilipiga simu as soon as sms ya transaction ilipoingia kwenye simu yangu.......
na nikapiga mkwara wasipoirudisha hiyo siku, kesho yake naenda ofisini na barua, na mtu atapoteza kazi. wakaona isiwe shida, wakarudisha.....
All in all, kama unavyosema rafiki, inawezekana ilikuwa bahati yangu tu ikarudi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom