Depression inaniathiri, nakaribia kujiua

Pole sana ndugu hizo ni changamoto za dunia jipe Moyo.

Mods tumewahi kuomba mara kadhaa kwamba wakati umefika tupate Jukwaa la "Mental therapy" na "Ushauri nasaha/Counselling"


Matatizo ya afya ya akili yanashika kasi sana nyakati hizi na mpaka kuja kugundua viashiria inakuwa too late na tunapoteza wapendwa wetu wengi.


Kama tumeweza kuwa na Jukwaa la Jokes ama Mizaha sidhani kama tutashindwa kuwa na Jukwaa muhimu linalohusiana na Afya Ya Akili. Naomba kuwasilisha.


CC Maxence Melo

JamiiForums
 
Najitahidi mkuu ila kwa kiasi fulani inakera sana ..
hiyo inayoitwa "kukera" itupe kwenye dust bin...enyoy maisha yako, focus kinachotakiwa kufanywa sasa kwenye maisha yako vs umri wako...... work hard man, earn big....hilo ndio la msingi mengine unapoteza muda wako na kujikabidhi kwa shetani kirahisi..
 
Asante mkuu
 
Mkuu we nyiuweee....maana maisha mbele Ni magumu Sanaa,nimesoma baadhi ya sababu zako nimeona unautoto mwingi.kuna watu wanavichwa Kama ngumi wanafurahia maisha,Kuna watu wafupi Kama themothi na wanafuraia maisha we jiuweee bwasheeee
Kuna utoto ndio sababu bado ni mtoto 19 yrs
Mshauri kama mtoto au mdogo ako basi!
Ni kweli hata mie nataka atambue kila mtu ana kasoro.shida ni jinsi ya kuhandle maneno ya watu na kufocus kwenye mambo yake.
Mtoa mada mi nakushauri uwe unavaa kofia kama hauko comfortable na hujajikubali.kinyume na hapo ujikubali tu na watu watakuzoea.
Mbona diamond alisemwa sana hadi Leo haters wanamwita domo ila hajali.
Acha na maneno ya watu,achana na ndugu zako.jikubali weka bidii kwenye malengo yako.ukifanikiwa watabadili maneno yaol
 
Asante mkuu
 
Asante mkuu kwa ushauri
 
Asante mkuu
 
Pole sana kijana,
Kwanza nikupongeze kwa hatua ya kwanza kabisa(kulisema tatizo) kwenye kupambana na mental problem ambayo inakusumbua.

Sjui hiyo mitaa unayotokea kama wamefikia hatua ya kufanya "bulling" mpaka muhusika ukajua kuwa kuna jambo wananionesha.
Kwa upande wangu ningekushauri njia kama tatu;

Moja, husisha familia na ndugu zako juu ya hili linalokukuta na madhara ambayo unayapata (ukieleza mpaka ishu ya suicidal ideation). Wazazi au ndugu yawezkana wamechkulia poa kwa sababu tu wao wanajua "hujafa, hujaumbika" hivyo hawaoni tatizo kwako ila ukiwaeleza kwa undani wao ndio msaada wa kwanza.

Mbili, waalimu shuleni, sio kila mwalimu aliyeshuleni atakuwa na uwezo wa kukusaidia ila naamini wapo walimu wenye uelewa wa maisha pamoja na dunia kwa ujumla hasa wale wenye umri mkubwa na busara. Mueleze kila kitu juu ya tatizo linalokusumbua atakusaidia hasa mazingira ya shule though yote hayo hayatabadili ukweli wa muonekano wako sababu tatizo ni kitu gani wanasema juu yako.

Tatu; nenda hospital kwenye kutengo cha ushauri nasaha au hata kwa magonjwa ya akili kwa sababu depression ni moja ya magonjwa ya akili yanayopelekea watu kujiua.

Lastly, tafuta hela mzee.
 
unazingua wewe..
Mimi mpaka leo sikio langu moja la kulia haliskii vizuri halafu unaskia vizuri, una akili, mikono, miguu.. Unajali nani akiongea? Cha msingi mambo yako yanaenda

Sikufichi mpaka sasa sikio langu moja haliskii vizuri.. Toka shule nimetaniwa majina ya kila aina lakini mpka leo nimekaza mambo yanaenda
 
Kwanza jikubali kwasababu wenye napungufu ni wengi duniani na wanaishi sababu wamejikubali.

Usikubali binadamu akuondolee furaha nafsini mwako kwa maneno yao kwasababu wewe haujajiumba bali umeumbwa hivyo na Mungu.
Asante mkuu
 
Asante sana mkuu
 
Hongera
 
Pole mkuu
 
Watu watakubeza ila naelewa Mkuu

Wengi wanaokupa ushauri hawajawahi kupitia hii bullying

Inaumiza unaweza jihisi una laana na kukosoa uumbaji wa Mungu

But keeping moving focus sna Kwa yanakuhusu (yaani wew mwenyewe)

Jifunze tabia ya kuwapuuza hii itakusaidia pandikiza +ve energy ya kujikubali
 
Aise, pole sana aise, usijinyonge, utakuwa mbinafsi nambari moja ukifanya hivyo. Wazazi usione hawana time. Ni vile wazazi wanaile nature ya kuwa protective kwa watoto wao hata awe mtu mzima. Hapo wameona hoja yako haina msingi na wanahofu badala ya kurekebisha ndio utajiharibu zaidi. Uamuzi wa kujinyonga ndio utawapa majonzi makubwa.

Cha kukushauri, puuzi mitazamo hasi yote juu yako, jikite kujenga maisha. Who knows?! Ukipata pesa yako hakuna atakayekuuliza, utaenda kufanya hizo plastic surgery vile utakavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…