Depression inaniathiri, nakaribia kujiua

Duniani huwa hakuna jambo baya wala zuri.....! Ila kinachofanya jambo lionekana ni baya au zuri ni mtazamo wa watu tu....! Ndio maana hata kwenye jamii zetu tunatofautiana tamaduni, kuna tamaduni za jamii nyingine ni mbaya sana kwa jamii fulani lakini jamii husika inafurahis sana tamaduni zao, na ukiwambia kuwa tamaduni zenu ni mbaya hawatokuelewa....!

Na Sisi binadamu tulivyoumbwa tumepewa utashi wa kuamua jambo lolote kutoka ndani mwetu...! Kile kinachotawala akili yako ndicho utachokiishi katika maisha yako.

Sasa wewe inaonekana unapoteza muda kuifanya akili yako iwaze jinsi unavyofanyiwa ukatili wa kisaikolojia, na hali hiyo haitobadilika kamwe mpaka wewe mwenyewe ubadili mtazamo.....!

Kuanzia sasa akili yako iwe inawaza vile vitu unavyovipenda tu, vitu usivyovihitaji usivipe nafasi kabisa kwenye akili yako...! Kwa mfano unaweza ukawa unahitaji sana heshima na upendo toka kwa watu, sasa ili upate hiyo heshima na upendo inatakiwa kwanza ww uanze kujipenda na kujiheshimu...

Anza kujikubali na ujione wa kipekee sana hapa duniani, jiulize kwanini ww Mungu ameamua kukufanya tofauti na watu wengi? Bro wewe una bahati sana ujue, yaani katika mkusanyiko wa watu 1000 wewe unauwezo wa kuonekana kati ya wote. Hiyo ni bahati bro .

Ww ndio muamuzi wa maisha yako, wewe ndio muamuzi wa furaha yako, si baba yako wala mama yako.....! Anza kujipa thamani kwanza wewe mwenyewe, then sisi wengine ndio tuione hiyo thamani uliyoitengeneza....! Usitegemee kuonewa huruma Ikiwa ww mwenyewe hujiamini wala kujikubali.!
 
Nashukuru mkuu
 
Ubarikiwe sana mkuu
 
1. Tafuta mtu ambae ana uelewa mpana wa mambo haya( anaweza kuwa mtaalamu) Mueleze tatzo lako

2.muone mtu ambae anaweza kukusikiliza na kukusaidia.
Kwanza mchunguze atalipokeaje swala lako


3. Sikushauri hili swala umuelezee mtu ambae hatakuwa na msaada. > Watu wengine hali yako wanaweza kuchukulia ni kitu cha kawaida, wakakupa majibu kama
"Tafuta hela kijana"
"We bado mdogo, soma"
"Hicho ni kitu kidogo, fanya mambo yako...."
"Mbona mimi Sina ............ Ila nafanya mambo yangu tuu"
Nk. Lakini kumbe wanakosea, depression, suicidal thoughts zinaweza kumpata mtu kama matokeo ya jambo lolote.
Mwingine ni body appearance tuu, mwingine ni economic reason, mwingine mi relationship problems.
Wakati huohuo kuna watu wengine watapitia matatizo hayo lakini bado watakuwa vizuri.


Bado kwenye jamii yetu elimu ya afya ya akili iko nyuma.
Hii inafanya wenzetu, wanaopatwa na matatizo haya, wasijue wapi wanapata msaada.(wengi wanakata tamaa ya kuishi)
Lakini pia, jamii haijui ni vipi inaweza kuwasaidia wenye matatizo haya
Mwisho tunaishia kuwatia moyo( hii haisaidii sana) au kuwavunja moyo.
 
Pole Sana noble.Dunia tupo wengi tunaopitia magumu ambayo yanatuacha na option moja tu.
Lakini usijidhuru kikubwa kubaliana na Hali kuwa wewe ni mtu tofauti.
Pitia uzi wangu kwenye bio uone ninachopitia pia lakini nipo najipa moyo tu
 
Usithubutu kujaribu wala kufanya lolote linalogharimu maisha yako kisa eti unamuogopa mwanadamu tena ambae hajakamilika, hakikisha kila jambo unalolifanya iwe ni kwa bidii ipo siku Mungu atakulipa na hao wanaokucheka watahitaji msaada wako.
 
Poleh sana mdogo wangu
Nashauri uende kwa wanaotoa ushauri/wanasaikolojia

Mueleze hio shida
Mwambie akupe mbinu za kujipenda na kujikubali jinsi ulivyo
Utasogeza muda
Ukiwa na hela yako mwenyewe utaamu ujikubali ama ubadili mwonekano.,
 
Hakuna watu wenye stress kama wenye vibamia mkuu, na wanaishi! Mimi nna madikio pengine yanazidi yako, nishaitwa ponjoro, masikio popo, majina ya kishenzi kama yoote kipindi nipo mdogo, lakini leo hii masikio yangu yapo vile vile na sisikii hizo habari na kama wapo wanaonisema basi si mbele yangu, sijali na mi mwenyewe najiona wa kawaida tu na maisha yanaenda fresh! Usijitie msongo wa mawazo mkuu, unaonekana una akili, itumie ndugu utafika mbali, acha kifo kikutafute chenuewe sio wewe ukitafute! Kuanzia sasa achana na fikra hizo kabisa, wengi wamekushauri mambo ya msingi na nnaamini huko uliko ushhapata nguvu ya kitosha sana kusonga na kuachana na nawazo ya kutaka kuwaachia dunia wapuuzi ambao woote wana vilema vyao.
 
Hata ambao hatuna chura tunasimangwa kweli sio wewe tu hebu jiamini wewe mwanaume anatakiwa awe na sura mbaya ya kutishaaa
Binadamu sometimes tunachezewa tu kisaikolojia, mtu anaweza kukutamkia kuwa kitu fulani ni tatizo na wewe ukaathirika kabisa kisaikolojia.
 
Asante sana mkuu
 
Wewe mtoto naomba kwanza amini Mungu anakupenda na ndio maana alikuumba!! Mtu asiyeweza hata kujiongezea unywele mmoja asikutishe!! Uzuri au ubaya wa sura waachie wanadamu!! Jikubali na mtu akikuoneshea dharau ukiweza mwambie nashukuru sana kwa kuwa wewe unaweza kuumba walio wazuri!!! Amini Mungu anakupenda saanaa!!
 
Nashukuru mkuu
 
Asante mkuu
 
Pole Sana noble.Dunia tupo wengi tunaopitia magumu ambayo yanatuacha na option moja tu.
Lakini usijidhuru kikubwa kubaliana na Hali kuwa wewe ni mtu tofauti.
Pitia uzi wangu kwenye bio uone ninachopitia pia lakini nipo najipa moyo tu
Sawa mkuu ngoja nifanye hivo
 
Usithubutu kujaribu wala kufanya lolote linalogharimu maisha yako kisa eti unamuogopa mwanadamu tena ambae hajakamilika, hakikisha kila jambo unalolifanya iwe ni kwa bidii ipo siku Mungu atakulipa na hao wanaokucheka watahitaji msaada wako.
Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…