Duniani huwa hakuna jambo baya wala zuri.....! Ila kinachofanya jambo lionekana ni baya au zuri ni mtazamo wa watu tu....! Ndio maana hata kwenye jamii zetu tunatofautiana tamaduni, kuna tamaduni za jamii nyingine ni mbaya sana kwa jamii fulani lakini jamii husika inafurahis sana tamaduni zao, na ukiwambia kuwa tamaduni zenu ni mbaya hawatokuelewa....!
Na Sisi binadamu tulivyoumbwa tumepewa utashi wa kuamua jambo lolote kutoka ndani mwetu...! Kile kinachotawala akili yako ndicho utachokiishi katika maisha yako.
Sasa wewe inaonekana unapoteza muda kuifanya akili yako iwaze jinsi unavyofanyiwa ukatili wa kisaikolojia, na hali hiyo haitobadilika kamwe mpaka wewe mwenyewe ubadili mtazamo.....!
Kuanzia sasa akili yako iwe inawaza vile vitu unavyovipenda tu, vitu usivyovihitaji usivipe nafasi kabisa kwenye akili yako...! Kwa mfano unaweza ukawa unahitaji sana heshima na upendo toka kwa watu, sasa ili upate hiyo heshima na upendo inatakiwa kwanza ww uanze kujipenda na kujiheshimu...
Anza kujikubali na ujione wa kipekee sana hapa duniani, jiulize kwanini ww Mungu ameamua kukufanya tofauti na watu wengi? Bro wewe una bahati sana ujue, yaani katika mkusanyiko wa watu 1000 wewe unauwezo wa kuonekana kati ya wote. Hiyo ni bahati bro .
Ww ndio muamuzi wa maisha yako, wewe ndio muamuzi wa furaha yako, si baba yako wala mama yako.....! Anza kujipa thamani kwanza wewe mwenyewe, then sisi wengine ndio tuione hiyo thamani uliyoitengeneza....! Usitegemee kuonewa huruma Ikiwa ww mwenyewe hujiamini wala kujikubali.!