Depression inaniathiri, nakaribia kujiua

Poleh sana mdogo wangu
Nashauri uende kwa wanaotoa ushauri/wanasaikolojia

Mueleze hio shida
Mwambie akupe mbinu za kujipenda na kujikubali jinsi ulivyo
Utasogeza muda
Ukiwa na hela yako mwenyewe utaamu ujikubali ama ubadili mwonekano.,
Asante mkuu
 
Kuna wakati fulani nilipanda mlima Kilimanjaro sasa katika group tulilokuwa mimi kidogo ndio nilikuwa mdogo kiumri na kiumbo pia wakati ndio tumeanza safari nilikutana na kijana kama mimi kiumbo na umri pia unaonekana ulikuwa kama wangu sasa, chakushangaza yeye katika mguu wake wa kulia alikuwa amekatwa mguu yani huu unyayo wa kukanyagia chini au eneo linalovishwa kiatu hakuwa nalo, na just imagine kwamba alipanda kama poster ( mbeba mzigo with 20 KG mgongoni ) alafu anapandisha mlima. Nilipomwona nilimuonea huruma na kabla ya safari niliingiwa na hofu ya kutoweza kupanda mlima. Toka nilipomwona nilipata ujasiri kuwa mimi ni mzima na ninaweza

Toka nilipomwona huyo jamaa sikuwahi kata tamaa katika jambo nalolifanya, nikimkumbuka ananipa ujasiri mkubwa wakufanya maajabu.
 
Asante kwa ushauri mkuu
 
Asante mkuu
 
😁😁😁😁😁😁😁
 
Asante kwa inspiration mkuu
 
Ignoring na kuchukulia kawaida sana kutakuokoa pia jione you are the best above anyone
 
Mkuu pole sana kikubwa ni kujikubali jinsi ulivyo , Ni watu wengi sana wana matatizo kama yako tena la kwako dogo. Jikubali wewe ni mtoto wa kiume usiyumbishwe na maneno ya watu tena wapumbavu. Fight umezaliwa wa kiume pambana, Mtangulize Mungu kwa kila jambo usiogope chochote.

UKITAKA MSAADA NI PM ANY TIME NITAKUSAIDIA
 
Nashukuru sana mkuu
 
Nakumbuka wakati niko mtoto, katika vurugu za utoto kuna mtoto aliwahi kusema eti nina pua kubwa🀣

Kweli nikawa nikijiangalia kwenye kioo, najiona kweli nina pua kubwa kweli, wakati kawaida tu 🀣
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ tuma picha hapa tuone kubwa au ndogo kweli
 
Nashukuru sana mkuu
Mleta mada pole kwa changamoto unayopitia lakini nakushauri usikate tamaa na wala usifikirie kujiua mimi pia katika makuzi yangu nilipitia changamoto kama yako mimi ilikuwa ni muonekano wa mdomo kuwa mkubwa like diamond hii ishu ilinitesa sana kwenye makuzi mpaka nilifikiria nikikua nitafute hospital yoyote ya upasuaji yaani hata nikiwa uwanjani maana nilikuwa na kipaji futball mashabiki pinzani walikuwa wananitania kinoma age ya kuanzia miaka 6,7,8,9 mpaka 16 nimepata shida but nikaamua kukubali hali yangu from now nachukulia normal wewe mcheki Manara jinsi alivyo lakini anaenjoy life so minakushauri jikubali na pambana kwenye life ili uje uwe kioo cha jamii
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ tuma picha hapa tuone kubwa au ndogo kweli
Ni ya kawaida tu maana sijawahi kuwa bullied wala kuambiwa na mtu mwingine tena...Kitu kingine ni mimi ni mweusi ila siyo kama Baraka the prince🀣 ila wakati wa utoto mtu anakushambulia wewe mweusi, kweli ukijiona kwenye kioo unajisikia vibaya wakati ni issue ya kijinga tu.
 
Dogo usikate tamaa na vitu ambavyo huwezi kuvi control. Relax
Then litafute kusudi la kuumbwa kwetu na uendelee kuishi.zingatia tumeumbwa ili
1. Tumjue Mungu
2. Tumtumikie Mungu
3.Tumpende
4 na tuishi nae milele.

Ishu ukizingatia haya mambo manne.
Usiruhusu hata siku.moja Hali yako ikakupelekea kushindwa kutimiza haya.
Na ukitaniwa husionyeshe kukasirika kwa kuwa utazidisha utani na watu wapuuzi. Ila naimani hujakutana na mitoto mitukutu ya uswazi, wakikutania ukionyesha tu hasira UMEISHaa.
 
Dogo, dawa siyo kujiua! Dawa nzuri ni kutafuta tu hela kwa bidii! Halafu utashangaa utakavyo sifiwa ya kwamba wewe ni handsome! Na una masikio mazuri kama Jay Z!! πŸ₯΅

Hujamuona hata yule msanii wetu aliyekuwa akidharauliwa enzi akiwa hana kitu? Eti alikuwa na mdomo mkubwa! πŸ˜ƒ Leo hii anakula tu na kuwazalisha watoto wazuri! Wanamuona ni bonge la handsome! Tafuta hela Dogo, halafu utakuja kunishukuru baadae kwa huu ushauri.
 
Kwanza hongera kwa uandishi bora kabisa.Hakika na class utakuwa vizuri ila hio ni inferior complex.Wote tumeubwa kwa mfano wake hakuna aliye mbaya ila kikubwa mkuu.Tutafute pesa uone kama kuna mtu atakudharau..Jikubali your the best mbona mi na kibyongo ila am still the best.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…