Depression inaniathiri, nakaribia kujiua

Habari za muda huu wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, mimi ni kijana wa kiume miaka 19 kwa muda mrefu sana nimekua nikisimbuliwa na depression "great depression" inayonifanya kutoyafurahia maisha na kujiona kama mtu anayeishi kwa bahati mbaya au labda sikustahili kuwepo duniani maana nimekua ni mtu wa kuchukiwa na watu mbali mbali either ninaowafahamu au hata wale ambao siwafahamu kwa sababu tu ya muonekano wangu hali iliyopelekea hata kujichukia mwenyewe.

Binafsi muonekano wa masikio yangu sio wa kawaida, kwani yametokeza sana kutokea usawa wa kichwa yani ni dizaini kama popo hivi (bat ears) hali inayopelekea kuwa bullied kila ninapokwenda, kuitwa majina yasiyofaa hata na watu nisiowafahamu, na wengine kwenda mbali zaidi kuukashifu uumbaji wa mwenyezi mungu.

Yafuatayo hapo chini ni baadhi tu ya matukio mengi niliyoyapitia so far ambayo sio siri yananila sana ndani kwa ndani;

✓ Ilikua siku ya jmosi asubuhi nimejiandaa nikasepa skonga Ile kufika nikazuiliwa kuingia simply because kulikua na rule kwamba mwanafunzi yeyoye ambaye ni day scholar siku za jmosi alitakiwa avae casual wear ambayo ni red and black ambavyo Ilikua tofauti kwangu mimi. Basi ikanibidi nivunge tu pale nje, baada ya muda kidogo akaja dem flani hivi wa form 2 (mimi nilikua form 4) basi katika kupiga stori mbili tatu na washkaji zangu wengine wawili tukaamua tutimbe maeneo flani (kupoteza muda of course,Ilikua bado asubuhi kurudi home Ilikua jau).

Kwenye mida ya kama saa nane hivi mchana wale washkaji zangu wawili wakaaga wakasepa nikabaki na yule demu ambapo pia aliniambia nimsindikize kwenye kituo cha daladala asepe na hapo ndipo msala ulipotokea, Ilikua hivi wakati tunatembea kando ya barabara alitokea jamaa flani kwa nyuma yetu akiwa kwenye bodaboda iliyokua ikitembea kwa mwendo wa taratibu, kimuonekano ni mtu mzima ambaye hakosi kuwa na mke na at least watoto wawili.

Kusema ukweli yule jamaa alinidhalilisha sana mbele za watu yani sijui hata nilimkosea nini au kosa langu nini mpaka afikie hatua ya kunifanyia kitendo cha kinyama namna Ile. Alianza kwa kucheka kwa nguvu sana kisha aliongea maneno ambayo yaliniumiza sana na nukuu .. " [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hivi hujaona wengine, na ex wako amesemaje kuhusu hili" hayo ni baadhi tu ya mengi aliyoyasema akimwambia yule dem. Kusema ukweli nilifedheheka sana mbele za watu, nilirudi home nikajifungia chumbani nikalia sana, sikuwa hata na hamu ya kukutana tena na yule dem jtatu skonga.

✓ siku hiyo baada ya kumaliza michosho ya home hapa nikawa sina chengine cha kufanya nikaamua ninyooshe miguu kitaa, sikufika ata hatua 20 nikakutana na kidem flani kikiwa na boyfriend wake.. aisee maneno yaliyomtoka yule dem kusema ukweli yaliniuma sana, alianza kwa kunishangaa kisha akasema " eeh Mungu anisaidie nisizae mtoto anayefanana kama huyu" . Kusema ukweli niliishiwa nguvu miguu ikanyong'onyea nikaamua tu nirudi home nikalale ..

✓ siku hiyo nikiwa town naelekea kituo cha daladala nisepe home kuna jamaa wawili nikawasikia wanaongea .. mmoja akimuuliza mwenzie " hivi mtu kama huyo unaweza kumuozesha binti yako ?" Nikageuka ghafla nikakuta ameninyooshea kidole . Dah nilicheka tu ila nikachukulia easy tu [emoji23][emoji23]

NB: hii imenitokea mara nyingi sana ndo maana nilichukulia kawaida yani hayo maneno nilisha yazoea ..

✓ kuna mwalimu aliwahi kuniambia mbele ya darasa zima kuwa sifanani na binadamu .. walinicheka sana wanafunzi wenzangu siku Ile [emoji1787][emoji1787]

✓Hayo ni baadhi tu ukiachana na yale madogo madogo kwa mfano unaweza ukawa unaongea na mtu ukimwangalia usoni utagundua ni dizaini kama anakucheka hivi ( japo sina uhakika kama ni kweli au najishtukia ), kingine pia sijui kama kuna jina baya au la kudhalilisha ambalo sijawahi kuitwa ..

Katika pitapita zangu mtandaoni nilikutana na hospitali moja Nairobi ambayo inajihusisha na cosmetic surgery mbali mbali ikiwemo Otoplasty ( ear shaping surgery). Basi nikaamua niwashirikishe wazazi wangu nione kama labda naweza kupata msaada wowote ukizingatia kwamba bei yake ni affordable ( japokua nikiri kwamba hii Ilikua last option kwangu), kwa jinsi nilivyo teseka sikua na jinsi.

Wazazi walikuja na response ambayo sikuitarajia kwani walinigomea katakata kwa hoja zisizo na mashiko sijui Michael Jackson and the like .. kilichoniuma zaidi bi mkubwa asubuhi na mapema akampigia kaka yangu mkubwa kunishtakia, bro nayeye alivyo mweupe kichwani bila ya kuuliza akanipandia hewani akawasha moto vilivyo [emoji23][emoji23].. tena kwa msisitizo akapayuka "SIO KWA HELA YANGU!, SIO KWA HELA YANGU!!"

Kusema ukweli nilivunjika sana moyo yani hapa saivi nnavyoandika nina zaidi ya miezi sita sijamtafuta mzee wala bimkubwa yani itokee sana wakipiga wao kwenye simu ya sister angu mkubwa wakiomba kuongea na mimi ndo huwa naongea nao tu hivo hivo kinafki lakini moyoni najikuta nawachukia sana wazazi wangu (Mungu anisamehe sijapenda ila depression inapelekea yote hayo)

Yani ukweli ni kwamba nimeathirika sana kisaikolojia nimekua mtu wa kujifungia tu chumbani siku nzima, hata darasani nashindwa kusimama mbele za watu nikazungumza yani itokee hata ka birthday party home nitajitungia tu kasafari ilimradi tu nisiwepo kwenye mkusanyiko wa watu.

Jambo linaloniumiza sana ni kwamba hakuna anayejali hali ninayopitia hata sister angu ninayeishi nae hapa ata akuone ni mwenye mawazo kiasi gani atakupita kama hakuoni jambo ambalo linazidi kuniongezea depression na kujiona sifai yani kwa kifupi sina mtu wa kumueleza hali ninayopitia. Ila yote kwa yote, shetani nae hachezi mbali maana wazo la kujiua limekua likinijia mara kwa mara lakini nashukuru Mungu amenisimamia mpaka leo sijachukua maamuzi magumu ..

Yote kwa yote naamini JF the home of great thinkers nitapata mawazo chanya yatakayo nisaidia kujua jinsi gani napambana na hali hii ya depression.

NB: Najua kuna wanaopitia magumu zaidi yangu ila amini usiamini mambo madogo madogo kama haya psychologically ni very draining yanaumiza.

#NAWASILISHA
Wewe komaa mtu akitalk shit na wewe mpe shit... Jifunze kukomaa kiume mtoto wa kike ndio analialia hovyo kwa sababu ya muonekano wake... Mtoto wa kiume asifiwi uzuri, mtoto wa kiume anasifiwa kuwa na roho ya Simba.. roho ya kiume. Yaani ngadu kwa ngadu *****.

Ukilemaa ukaweka lonyalonya utajiua kweli ila ukisimika na ukaacha kujali haitakusumbua.
 
Kijana pole sana kwa hiyo changamoto unayopitia.Ushauri wangu ni kwamba wawe usijishtukie uonapo watu wanacheka.
Kwa vile bado uko shuleni soma sana na ipo siku hao wanaokucheka watakuja kukupigia magoti kukuomba msaada. Mwisho tambua tu kuwa mungu kamuumba kila mtu kwa mfanowe.
Asante mkuu [emoji120][emoji120]
 
Pole sana mkuu. Be strong, kuna watu wanapitia makubwa kuliko hayo. Wewe jikaze, soon utapata hela zako,utafanya unachotaka.. Tafuta rafiki yako wa kweli wa shida na raha mueleze. Halaf uwe unajichanganya nae sehemu mbalimbali. Lakin pia ujasiri wa kuja kuyaongea haya hapa umeshayashinda
Nashukuru sana mkuu
 
Aisee polee sana, jikubali jinsi ulivo ukishajiona wewe upo kamili na wengine watakuona hivo, usiache nafsi yako na mawazo yako yakutawale kuwa ww ni kiumbe mbaya, jipende, jithamini, kamwe usijidharau! Soma kwa bidii tafuta pesa utasahau yote hayo!! Diamond mwenyew alikuwa anaitwa domo kutokana na maumbile makubwa ya mdomo wake, lakini kwa sasa anaitwa lips denda au Sadala.... so weka pamba masikioni songa mbele!!! Ukijiua ujue moja kwa moja jehanamu.
Nashukuru mkuu
 
Pole mdogo wangu! Najua nivigumu kuyakataa maumivu ya kushtukiza ila nikutie moyo mkuu- kumbuka MUNGU amekuumba kwa mfano wake kwahiyo usitingishike na kebehi za wenye mizaha! Alafu utambue hili kwamba hakuna kilichokamilika kisipitie testing hapo unajaribiwa tu ili ujikatae sasa wewe jikubali tena uwe proudly na ulivyoumbwa! Binafsi nina pua kubwa kuliko maelezo na nilichekwa sana na watu ila baadae pua hii hii ikampagawisha mutoto ya kizungu na ninaenjoy maana navuta oxygen yakutoosha!
Mtangulize MUNGU na usali uikatae hiyo roho ya kujikataa na kujiua! Hilo ni roho la mauti linakuonea wivu, linajua wewe ni nani baadae utakuwa nani na utawasubua katika ulimwengu wa kiroho! Sasa mkimbilie MUNGU na umpinge shetani naye atakukimbia!
Ubarikiwe mkuu [emoji120][emoji120]
 
Binafsi kama utafikia uamuzi wa kwenda kufanya surgery na ukapata kiasi cha pesa nami nitachangia.

Wadau huyu mtu ameshapoteza confidence yote, suala lilikobaki ni kuyapunguza au aendelee kuwa kwenye depression.

Mbona matako ya plastic mnayafurahia huko katika mitandao ya picha??
Nashukuru sana mkuu
 
Kuna kiumbe asiyesemwa chini ya jua,jikubali na ujione wewe ni bora,yaani kusemwa unaweka mambo moyoni kuna watu wanatamani hata hayo masikio ili wasikie vizuri.
 
Ila hili tatizo la depression naona linaongezeka kwa watu wengi hapa bongo. Hivi uku kwetu hamna ma specialist wa haya matatzo. Wale watoa ushauri
 
Sasa Rafiki; watu wanakushauri na kukutia Moyo kwamba kuna wabaya zaidi yako na Picha wametuma umeona; bado unalalamika! Haya ukijiua huko unakokwenda ndiyo kubaya zaidi! Maana Muumba atakusubiri na kukuadhibu kwa kuutoa uhai wako/wake! Sasa kama ulivyoshauriwa, Tafuta pesa hakuna anaemdharau Mwenye pesa. Hata shetani ana masikio kama punda na kichwa Kama paka lakini kuna watu wanampenda kwa kuwa anawapa Hela! Unaona bana, pia mtafute Muumba akupe nguvu za kuhubiri na miujiza watu watakuwa wanasema huyu ni malaika siyo wa kawaida kwa miujiza utakayokuwa unafanya. Kwa maana hiyo duniani utapeta na mbinguni utakula nyamachoma na soda vile2.
 
Habari za muda huu wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, mimi ni kijana wa kiume miaka 19 kwa muda mrefu sana nimekua nikisimbuliwa na depression "great depression" inayonifanya kutoyafurahia maisha na kujiona kama mtu anayeishi kwa bahati mbaya au labda sikustahili kuwepo duniani maana nimekua ni mtu wa kuchukiwa na watu mbali mbali either ninaowafahamu au hata wale ambao siwafahamu kwa sababu tu ya muonekano wangu hali iliyopelekea hata kujichukia mwenyewe.

Binafsi muonekano wa masikio yangu sio wa kawaida, kwani yametokeza sana kutokea usawa wa kichwa yani ni dizaini kama popo hivi (bat ears) hali inayopelekea kuwa bullied kila ninapokwenda, kuitwa majina yasiyofaa hata na watu nisiowafahamu, na wengine kwenda mbali zaidi kuukashifu uumbaji wa mwenyezi mungu.

Yafuatayo hapo chini ni baadhi tu ya matukio mengi niliyoyapitia so far ambayo sio siri yananila sana ndani kwa ndani;

✓ Ilikua siku ya jmosi asubuhi nimejiandaa nikasepa skonga Ile kufika nikazuiliwa kuingia simply because kulikua na rule kwamba mwanafunzi yeyoye ambaye ni day scholar siku za jmosi alitakiwa avae casual wear ambayo ni red and black ambavyo Ilikua tofauti kwangu mimi. Basi ikanibidi nivunge tu pale nje, baada ya muda kidogo akaja dem flani hivi wa form 2 (mimi nilikua form 4) basi katika kupiga stori mbili tatu na washkaji zangu wengine wawili tukaamua tutimbe maeneo flani (kupoteza muda of course,Ilikua bado asubuhi kurudi home Ilikua jau).

Kwenye mida ya kama saa nane hivi mchana wale washkaji zangu wawili wakaaga wakasepa nikabaki na yule demu ambapo pia aliniambia nimsindikize kwenye kituo cha daladala asepe na hapo ndipo msala ulipotokea, Ilikua hivi wakati tunatembea kando ya barabara alitokea jamaa flani kwa nyuma yetu akiwa kwenye bodaboda iliyokua ikitembea kwa mwendo wa taratibu, kimuonekano ni mtu mzima ambaye hakosi kuwa na mke na at least watoto wawili.

Kusema ukweli yule jamaa alinidhalilisha sana mbele za watu yani sijui hata nilimkosea nini au kosa langu nini mpaka afikie hatua ya kunifanyia kitendo cha kinyama namna Ile. Alianza kwa kucheka kwa nguvu sana kisha aliongea maneno ambayo yaliniumiza sana na nukuu .. " [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hivi hujaona wengine, na ex wako amesemaje kuhusu hili" hayo ni baadhi tu ya mengi aliyoyasema akimwambia yule dem. Kusema ukweli nilifedheheka sana mbele za watu, nilirudi home nikajifungia chumbani nikalia sana, sikuwa hata na hamu ya kukutana tena na yule dem jtatu skonga.

✓ siku hiyo baada ya kumaliza michosho ya home hapa nikawa sina chengine cha kufanya nikaamua ninyooshe miguu kitaa, sikufika ata hatua 20 nikakutana na kidem flani kikiwa na boyfriend wake.. aisee maneno yaliyomtoka yule dem kusema ukweli yaliniuma sana, alianza kwa kunishangaa kisha akasema " eeh Mungu anisaidie nisizae mtoto anayefanana kama huyu" . Kusema ukweli niliishiwa nguvu miguu ikanyong'onyea nikaamua tu nirudi home nikalale ..

✓ siku hiyo nikiwa town naelekea kituo cha daladala nisepe home kuna jamaa wawili nikawasikia wanaongea .. mmoja akimuuliza mwenzie " hivi mtu kama huyo unaweza kumuozesha binti yako ?" Nikageuka ghafla nikakuta ameninyooshea kidole . Dah nilicheka tu ila nikachukulia easy tu [emoji23][emoji23]

NB: hii imenitokea mara nyingi sana ndo maana nilichukulia kawaida yani hayo maneno nilisha yazoea ..

✓ kuna mwalimu aliwahi kuniambia mbele ya darasa zima kuwa sifanani na binadamu .. walinicheka sana wanafunzi wenzangu siku Ile [emoji1787][emoji1787]

✓Hayo ni baadhi tu ukiachana na yale madogo madogo kwa mfano unaweza ukawa unaongea na mtu ukimwangalia usoni utagundua ni dizaini kama anakucheka hivi ( japo sina uhakika kama ni kweli au najishtukia ), kingine pia sijui kama kuna jina baya au la kudhalilisha ambalo sijawahi kuitwa ..

Katika pitapita zangu mtandaoni nilikutana na hospitali moja Nairobi ambayo inajihusisha na cosmetic surgery mbali mbali ikiwemo Otoplasty ( ear shaping surgery). Basi nikaamua niwashirikishe wazazi wangu nione kama labda naweza kupata msaada wowote ukizingatia kwamba bei yake ni affordable ( japokua nikiri kwamba hii Ilikua last option kwangu), kwa jinsi nilivyo teseka sikua na jinsi.

Wazazi walikuja na response ambayo sikuitarajia kwani walinigomea katakata kwa hoja zisizo na mashiko sijui Michael Jackson and the like .. kilichoniuma zaidi bi mkubwa asubuhi na mapema akampigia kaka yangu mkubwa kunishtakia, bro nayeye alivyo mweupe kichwani bila ya kuuliza akanipandia hewani akawasha moto vilivyo [emoji23][emoji23].. tena kwa msisitizo akapayuka "SIO KWA HELA YANGU!, SIO KWA HELA YANGU!!"

Kusema ukweli nilivunjika sana moyo yani hapa saivi nnavyoandika nina zaidi ya miezi sita sijamtafuta mzee wala bimkubwa yani itokee sana wakipiga wao kwenye simu ya sister angu mkubwa wakiomba kuongea na mimi ndo huwa naongea nao tu hivo hivo kinafki lakini moyoni najikuta nawachukia sana wazazi wangu (Mungu anisamehe sijapenda ila depression inapelekea yote hayo)

Yani ukweli ni kwamba nimeathirika sana kisaikolojia nimekua mtu wa kujifungia tu chumbani siku nzima, hata darasani nashindwa kusimama mbele za watu nikazungumza yani itokee hata ka birthday party home nitajitungia tu kasafari ilimradi tu nisiwepo kwenye mkusanyiko wa watu.

Jambo linaloniumiza sana ni kwamba hakuna anayejali hali ninayopitia hata sister angu ninayeishi nae hapa ata akuone ni mwenye mawazo kiasi gani atakupita kama hakuoni jambo ambalo linazidi kuniongezea depression na kujiona sifai yani kwa kifupi sina mtu wa kumueleza hali ninayopitia. Ila yote kwa yote, shetani nae hachezi mbali maana wazo la kujiua limekua likinijia mara kwa mara lakini nashukuru Mungu amenisimamia mpaka leo sijachukua maamuzi magumu ..

Yote kwa yote naamini JF the home of great thinkers nitapata mawazo chanya yatakayo nisaidia kujua jinsi gani napambana na hali hii ya depression.

NB: Najua kuna wanaopitia magumu zaidi yangu ila amini usiamini mambo madogo madogo kama haya psychologically ni very draining yanaumiza.

#NAWASILISHA
Pole sana kijana, lakini kumbuka sote tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, unachotakiwa kufanya ni kuwa mpuuzi kwa baadhi ya maneno au kejeli za watu pia fanya mambo ambayo unajua yanakupa furaha pia unatakiwa kujiamini tu mbele za watu kwasababu sisi sote tunakasoro mbalimbali, Mungu akusaidie upate kujiamni pia washirikishe viongozi wa dini na watu wa saikolojia nazani watakupa msaada zaidi🙏🙏🙏
 
Muhimu Ni kujikubali wewe Kama ulivyo na utapata tu wa kufanana nae na atakupenda hivyo hivyo. Achana na masuala ya surgery kwa kitu ambacho hakiwezi kukuua.

Kwanza Jikubali hivyo hivyo... na ujue 2pac alipigwa risasi mguu mmoja ukawa mfupi akaambiwa akafanyiwe oparesheni akakataa... Akajikubali, Akaanza kutembea kwa kuchechemea Kama anadunda hivi baada ya hapo Dunia ikapenda zile swagger Basi wote wakaanza kudunda wakijua Ni fasheni kumbe muhuni kajikubali tu na maisha yakaendelea na akavumbua kutembea kwa kudunda Duniani.

Jikubali Mwanaume! [emoji41]
 
Ukiniona hata Mimi nna Bonge la tege Kama banio la ugali vile... Lakini nakomaa kuwaaminisha watu tege langu Ni zuri na Ni fashion Sasa hivi watu wanajitegesha na wao Kama Mimi. [emoji41][emoji16]
 
Usipo badilika na kubadili huo mtazamo utakuja haribu maisha yako yote. Kwanza hapo yameshaharibika
 
Nitajitahidi mkuu
Jitahidi bora yako hata wewe unasemwa kimya kimya kuna watu wamezaliwa na visanga, kuna siku dsm kkoo niliwahi shuhudia jamaa mrefu futi kama 7.5 anamzidi hadi hashem thabeet . Watu wamemjalia wanampiga picha wengine wanashangaa wanapiga kelele wengine wanacheka lakini jamaa aikuwa anajiamini.

Yule jamaa hata dalala hawezi kupanda, hata kitanda cha kawaida hawezi kulala maana miguu yote itaishia njee.

Kuna watu wamezaliwa wafupi sana kama yule dada anaeigiza huba hata futi 2 hafiki lakini events zote matamasha yote hata yakiserikali huwa anahudhuria maana ameshajikubali
 
Back
Top Bottom