Depression inaniathiri, nakaribia kujiua

Pole bwana mdogo ,Dunia inachangamoto nyingi.

Jitahidi uyashinde mapito hayo ,focus kwenye masomo tu usigeuke nyuma .
Kwa uandishi wako na kupanga visa ,unaonekana akili kubwa .
Kila lakheri Mungu akusaidie
 
Habari za muda huu wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, mimi ni kijana wa kiume miaka 19 kwa muda mrefu sana nimekua nikisimbuliwa na depression "great depression" inayonifanya kutoyafurahia maisha na kujiona kama mtu anayeishi kwa bahati mbaya au labda sikustahili kuwepo duniani maana nimekua ni mtu wa kuchukiwa na watu mbali mbali either ninaowafahamu au hata wale ambao siwafahamu kwa sababu tu ya muonekano wangu hali iliyopelekea hata kujichukia mwenyewe.

Binafsi muonekano wa masikio yangu sio wa kawaida, kwani yametokeza sana kutokea usawa wa kichwa yani ni dizaini kama popo hivi (bat ears) hali inayopelekea kuwa bullied kila ninapokwenda, kuitwa majina yasiyofaa hata na watu nisiowafahamu, na wengine kwenda mbali zaidi kuukashifu uumbaji wa mwenyezi mungu.

Yafuatayo hapo chini ni baadhi tu ya matukio mengi niliyoyapitia so far ambayo sio siri yananila sana ndani kwa ndani;

✓ Ilikua siku ya jmosi asubuhi nimejiandaa nikasepa skonga Ile kufika nikazuiliwa kuingia simply because kulikua na rule kwamba mwanafunzi yeyoye ambaye ni day scholar siku za jmosi alitakiwa avae casual wear ambayo ni red and black ambavyo Ilikua tofauti kwangu mimi. Basi ikanibidi nivunge tu pale nje, baada ya muda kidogo akaja dem flani hivi wa form 2 (mimi nilikua form 4) basi katika kupiga stori mbili tatu na washkaji zangu wengine wawili tukaamua tutimbe maeneo flani (kupoteza muda of course,Ilikua bado asubuhi kurudi home Ilikua jau).

Kwenye mida ya kama saa nane hivi mchana wale washkaji zangu wawili wakaaga wakasepa nikabaki na yule demu ambapo pia aliniambia nimsindikize kwenye kituo cha daladala asepe na hapo ndipo msala ulipotokea, Ilikua hivi wakati tunatembea kando ya barabara alitokea jamaa flani kwa nyuma yetu akiwa kwenye bodaboda iliyokua ikitembea kwa mwendo wa taratibu, kimuonekano ni mtu mzima ambaye hakosi kuwa na mke na at least watoto wawili.

Kusema ukweli yule jamaa alinidhalilisha sana mbele za watu yani sijui hata nilimkosea nini au kosa langu nini mpaka afikie hatua ya kunifanyia kitendo cha kinyama namna Ile. Alianza kwa kucheka kwa nguvu sana kisha aliongea maneno ambayo yaliniumiza sana na nukuu .. " [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hivi hujaona wengine, na ex wako amesemaje kuhusu hili" hayo ni baadhi tu ya mengi aliyoyasema akimwambia yule dem. Kusema ukweli nilifedheheka sana mbele za watu, nilirudi home nikajifungia chumbani nikalia sana, sikuwa hata na hamu ya kukutana tena na yule dem jtatu skonga.

✓ siku hiyo baada ya kumaliza michosho ya home hapa nikawa sina chengine cha kufanya nikaamua ninyooshe miguu kitaa, sikufika ata hatua 20 nikakutana na kidem flani kikiwa na boyfriend wake.. aisee maneno yaliyomtoka yule dem kusema ukweli yaliniuma sana, alianza kwa kunishangaa kisha akasema " eeh Mungu anisaidie nisizae mtoto anayefanana kama huyu" . Kusema ukweli niliishiwa nguvu miguu ikanyong'onyea nikaamua tu nirudi home nikalale ..

✓ siku hiyo nikiwa town naelekea kituo cha daladala nisepe home kuna jamaa wawili nikawasikia wanaongea .. mmoja akimuuliza mwenzie " hivi mtu kama huyo unaweza kumuozesha binti yako ?" Nikageuka ghafla nikakuta ameninyooshea kidole . Dah nilicheka tu ila nikachukulia easy tu [emoji23][emoji23]

NB: hii imenitokea mara nyingi sana ndo maana nilichukulia kawaida yani hayo maneno nilisha yazoea ..

✓ kuna mwalimu aliwahi kuniambia mbele ya darasa zima kuwa sifanani na binadamu .. walinicheka sana wanafunzi wenzangu siku Ile [emoji1787][emoji1787]

✓Hayo ni baadhi tu ukiachana na yale madogo madogo kwa mfano unaweza ukawa unaongea na mtu ukimwangalia usoni utagundua ni dizaini kama anakucheka hivi ( japo sina uhakika kama ni kweli au najishtukia ), kingine pia sijui kama kuna jina baya au la kudhalilisha ambalo sijawahi kuitwa ..

Katika pitapita zangu mtandaoni nilikutana na hospitali moja Nairobi ambayo inajihusisha na cosmetic surgery mbali mbali ikiwemo Otoplasty ( ear shaping surgery). Basi nikaamua niwashirikishe wazazi wangu nione kama labda naweza kupata msaada wowote ukizingatia kwamba bei yake ni affordable ( japokua nikiri kwamba hii Ilikua last option kwangu), kwa jinsi nilivyo teseka sikua na jinsi.

Wazazi walikuja na response ambayo sikuitarajia kwani walinigomea katakata kwa hoja zisizo na mashiko sijui Michael Jackson and the like .. kilichoniuma zaidi bi mkubwa asubuhi na mapema akampigia kaka yangu mkubwa kunishtakia, bro nayeye alivyo mweupe kichwani bila ya kuuliza akanipandia hewani akawasha moto vilivyo [emoji23][emoji23].. tena kwa msisitizo akapayuka "SIO KWA HELA YANGU!, SIO KWA HELA YANGU!!"

Kusema ukweli nilivunjika sana moyo yani hapa saivi nnavyoandika nina zaidi ya miezi sita sijamtafuta mzee wala bimkubwa yani itokee sana wakipiga wao kwenye simu ya sister angu mkubwa wakiomba kuongea na mimi ndo huwa naongea nao tu hivo hivo kinafki lakini moyoni najikuta nawachukia sana wazazi wangu (Mungu anisamehe sijapenda ila depression inapelekea yote hayo)

Yani ukweli ni kwamba nimeathirika sana kisaikolojia nimekua mtu wa kujifungia tu chumbani siku nzima, hata darasani nashindwa kusimama mbele za watu nikazungumza yani itokee hata ka birthday party home nitajitungia tu kasafari ilimradi tu nisiwepo kwenye mkusanyiko wa watu.

Jambo linaloniumiza sana ni kwamba hakuna anayejali hali ninayopitia hata sister angu ninayeishi nae hapa ata akuone ni mwenye mawazo kiasi gani atakupita kama hakuoni jambo ambalo linazidi kuniongezea depression na kujiona sifai yani kwa kifupi sina mtu wa kumueleza hali ninayopitia. Ila yote kwa yote, shetani nae hachezi mbali maana wazo la kujiua limekua likinijia mara kwa mara lakini nashukuru Mungu amenisimamia mpaka leo sijachukua maamuzi magumu ..

Yote kwa yote naamini JF the home of great thinkers nitapata mawazo chanya yatakayo nisaidia kujua jinsi gani napambana na hali hii ya depression.

NB: Najua kuna wanaopitia magumu zaidi yangu ila amini usiamini mambo madogo madogo kama haya psychologically ni very draining yanaumiza.

#NAWASILISHA
Kama nimekusoma kuwa hali ya kukutana na comment za hovyo juu ya masikio yako umeshazoea. Sasa hiyo depression inatoka wapi? Everything begins with you...yes, it begins with u😡! Hutaki kujikubali ww mwenyewe jinsi ulivyo...sasa unategemea nani akukubali? Kila binadamu ni unique...ingawa uniqueness muda mwingine Muumba huipeleka another level 😜! Ni jukumu lako muumbwaji kupokea uumbwaji wako na kuukubali na hata kuutumia kwa faida yako mwenyewe 😜! Sehemu moja wapo ambayo inaweza kukulipa ni ucheza filamu nk! Sakamya hela tu hao mabinti watakuja kukugombania tu hapo baadae! Acha kulialia hao hawakukuumba ww! Aliyekuumba hivyo ilimpendeza hivyo kwa kusudi maalumu ktk dunia hii🤔! Unachotakiwa kufanya kwa sasa ni kujijua ww ni mtu maalum kwa kazi maalum mfyuuuuu 😡!
 
Muonekano wa nn dogo? Lilia vitu vya msingi Soma kwa bidii ufute ujinga, fanya kazi kwa bidii upate kipato halali ili ukwepe umasikini na upate tiba bora ili utibu maradhi ya kibinadamu
Kumbuka maadui wakubwa wa binadamu Ni
1 ujinga
2 maradhi
3 umasikini
 
Jitahidi bora yako hata wewe unasemwa kimya kimya kuna watu wamezaliwa na visanga, kuna siku dsm kkoo niliwahi shuhudia jamaa mrefu futi kama 7.5 anamzidi hadi hashem thabeet . Watu wamemjalia wanampiga picha wengine wanashangaa wanapiga kelele wengine wanacheka lakini jamaa aikuwa anajiamini.

Yule jamaa hata dalala hawezi kupanda, hata kitanda cha kawaida hawezi kulala maana miguu yote itaishia njee.

Kuna watu wamezaliwa wafupi sana kama yule dada anaeigiza huba hata futi 2 hafiki lakini events zote matamasha yote hata yakiserikali huwa anahudhuria maana ameshajikubali
Shukrani mkuu
 
Pole bwana mdogo ,Dunia inachangamoto nyingi.

Jitahidi uyashinde mapito hayo ,focus kwenye masomo tu usigeuke nyuma .
Kwa uandishi wako na kupanga visa ,unaonekana akili kubwa .
Kila lakheri Mungu akusaidie
Shukrani mkuu [emoji120][emoji120]
 
Kama nimekusoma kuwa hali ya kukutana na comment za hovyo juu ya masikio yako umeshazoea. Sasa hiyo depression inatoka wapi? Everything begins with you...yes, it begins with u[emoji35]! Hutaki kujikubali ww mwenyewe jinsi ulivyo...sasa unategemea nani akukubali? Kila binadamu ni unique...ingawa uniqueness muda mwingine Muumba huipeleka another level [emoji12]! Ni jukumu lako muumbwaji kupokea uumbwaji wako na kuukubali na hata kuutumia kwa faida yako mwenyewe [emoji12]! Sehemu moja wapo ambayo inaweza kukulipa ni ucheza filamu nk! Sakamya hela tu hao mabinti watakuja kukugombania tu hapo baadae! Acha kulialia hao hawakukuumba ww! Aliyekuumba hivyo ilimpendeza hivyo kwa kusudi maalumu ktk dunia hii[emoji848]! Unachotakiwa kufanya kwa sasa ni kujijua ww ni mtu maalum kwa kazi maalum mfyuuuuu [emoji35]!
Mkuu nimeshazoea ila kuna mambo yanadhalilisha sana
 
Inasikitisha sana watu wanapomdhiahaki mtu kwa alivyoumbwa utadhani kuna mtu anajiumba na kujichagulia aweje.

Aslimia kubwa wanaoweza kukucheka ni akili ndogo na wendawazimu.
Amini nakuambia kuna sehemu Mungu kakuumba ukiwa the best kuliko wengine. Boresha zaidi hapo uonapo uko vizuri.
 
Mkuu nimeshazoea ila kuna mambo yanadhalilisha sana
Achana nao, hao wote ni wapuuzi kama walivyowapuuzi wengine! Dawa yao ni kuwapuuza! Ww hukujiumba kama wao wasivyojiumba😡!
 
Soma na tafuta pesa kwa bidii,hayo yote utaona ni upuuzi na hata watu wataanza kukuiga hivyo ulivyo,umeshawahi kumuangalia vizuri masikio ya Will Smith View attachment 1816082 ni kwasababu tu ana pesa na hakuna hata anaejali muonekano wake,kaa ukijua kuwa hakuna mtu alieumbwa kwa kukosewa hapa duniani,wote tunapendeza ni hivyo hatuna pesa tu...
Hata Usher Raymond
 
Tumia changamoto kuwa furusa! Fungua banda la masikio!
Andiko masikio adimu yanaonekana hapa!
Weka picha ya sungura halafu kwa pembeni weka njoo ujionee masikio yanayogeuka, ongezea na chumvi kwamba masikio yako yanasikia hadi usiku ukiwa umelala hivyo kampuni za ulinzi zitakugombania kwa dau!
Hukupewa masikio hayo bila kusudi la Mungu, huenda huo ndiyo mgodi wako wa kupiga hela, wengine wanapewa kipaji wewe umepewa masikio!

Ebu njoo inbobo tuyajenge nikupe mtaji
Yaaan wewe[emoji16][emoji16][emoji849]

Kama sio comedian sijui

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
We dogo utoto unakusumbua sana....viungo vyote unavyo ila unataka kujinyonga kwa sababu ya masikio kuwa makubwa?![emoji849]

Humu duniani kuna changamoto ni usipime, hiyo ya masikio mbona kitu kidogo, fungia raia tinted soma, tafuta pesa!...mpaka unakuwa mkaka huko umewin life, michuchu shobo kama lote!

Ila narudia ..

Tafuta pesa, na uhakikishe umeipata!

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Habari za muda huu wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, mimi ni kijana wa kiume miaka 19 kwa muda mrefu sana nimekua nikisimbuliwa na depression "great depression" inayonifanya kutoyafurahia maisha na kujiona kama mtu anayeishi kwa bahati mbaya au labda sikustahili kuwepo duniani maana nimekua ni mtu wa kuchukiwa na watu mbali mbali either ninaowafahamu au hata wale ambao siwafahamu kwa sababu tu ya muonekano wangu hali iliyopelekea hata kujichukia mwenyewe.

Binafsi muonekano wa masikio yangu sio wa kawaida, kwani yametokeza sana kutokea usawa wa kichwa yani ni dizaini kama popo hivi (bat ears) hali inayopelekea kuwa bullied kila ninapokwenda, kuitwa majina yasiyofaa hata na watu nisiowafahamu, na wengine kwenda mbali zaidi kuukashifu uumbaji wa mwenyezi mungu.

Yafuatayo hapo chini ni baadhi tu ya matukio mengi niliyoyapitia so far ambayo sio siri yananila sana ndani kwa ndani;

✓ Ilikua siku ya jmosi asubuhi nimejiandaa nikasepa skonga Ile kufika nikazuiliwa kuingia simply because kulikua na rule kwamba mwanafunzi yeyoye ambaye ni day scholar siku za jmosi alitakiwa avae casual wear ambayo ni red and black ambavyo Ilikua tofauti kwangu mimi. Basi ikanibidi nivunge tu pale nje, baada ya muda kidogo akaja dem flani hivi wa form 2 (mimi nilikua form 4) basi katika kupiga stori mbili tatu na washkaji zangu wengine wawili tukaamua tutimbe maeneo flani (kupoteza muda of course,Ilikua bado asubuhi kurudi home Ilikua jau).

Kwenye mida ya kama saa nane hivi mchana wale washkaji zangu wawili wakaaga wakasepa nikabaki na yule demu ambapo pia aliniambia nimsindikize kwenye kituo cha daladala asepe na hapo ndipo msala ulipotokea, Ilikua hivi wakati tunatembea kando ya barabara alitokea jamaa flani kwa nyuma yetu akiwa kwenye bodaboda iliyokua ikitembea kwa mwendo wa taratibu, kimuonekano ni mtu mzima ambaye hakosi kuwa na mke na at least watoto wawili.

Kusema ukweli yule jamaa alinidhalilisha sana mbele za watu yani sijui hata nilimkosea nini au kosa langu nini mpaka afikie hatua ya kunifanyia kitendo cha kinyama namna Ile. Alianza kwa kucheka kwa nguvu sana kisha aliongea maneno ambayo yaliniumiza sana na nukuu .. " [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hivi hujaona wengine, na ex wako amesemaje kuhusu hili" hayo ni baadhi tu ya mengi aliyoyasema akimwambia yule dem. Kusema ukweli nilifedheheka sana mbele za watu, nilirudi home nikajifungia chumbani nikalia sana, sikuwa hata na hamu ya kukutana tena na yule dem jtatu skonga.

✓ siku hiyo baada ya kumaliza michosho ya home hapa nikawa sina chengine cha kufanya nikaamua ninyooshe miguu kitaa, sikufika ata hatua 20 nikakutana na kidem flani kikiwa na boyfriend wake.. aisee maneno yaliyomtoka yule dem kusema ukweli yaliniuma sana, alianza kwa kunishangaa kisha akasema " eeh Mungu anisaidie nisizae mtoto anayefanana kama huyu" . Kusema ukweli niliishiwa nguvu miguu ikanyong'onyea nikaamua tu nirudi home nikalale ..

✓ siku hiyo nikiwa town naelekea kituo cha daladala nisepe home kuna jamaa wawili nikawasikia wanaongea .. mmoja akimuuliza mwenzie " hivi mtu kama huyo unaweza kumuozesha binti yako ?" Nikageuka ghafla nikakuta ameninyooshea kidole . Dah nilicheka tu ila nikachukulia easy tu [emoji23][emoji23]

NB: hii imenitokea mara nyingi sana ndo maana nilichukulia kawaida yani hayo maneno nilisha yazoea ..

✓ kuna mwalimu aliwahi kuniambia mbele ya darasa zima kuwa sifanani na binadamu .. walinicheka sana wanafunzi wenzangu siku Ile [emoji1787][emoji1787]

✓Hayo ni baadhi tu ukiachana na yale madogo madogo kwa mfano unaweza ukawa unaongea na mtu ukimwangalia usoni utagundua ni dizaini kama anakucheka hivi ( japo sina uhakika kama ni kweli au najishtukia ), kingine pia sijui kama kuna jina baya au la kudhalilisha ambalo sijawahi kuitwa ..

Katika pitapita zangu mtandaoni nilikutana na hospitali moja Nairobi ambayo inajihusisha na cosmetic surgery mbali mbali ikiwemo Otoplasty ( ear shaping surgery). Basi nikaamua niwashirikishe wazazi wangu nione kama labda naweza kupata msaada wowote ukizingatia kwamba bei yake ni affordable ( japokua nikiri kwamba hii Ilikua last option kwangu), kwa jinsi nilivyo teseka sikua na jinsi.

Wazazi walikuja na response ambayo sikuitarajia kwani walinigomea katakata kwa hoja zisizo na mashiko sijui Michael Jackson and the like .. kilichoniuma zaidi bi mkubwa asubuhi na mapema akampigia kaka yangu mkubwa kunishtakia, bro nayeye alivyo mweupe kichwani bila ya kuuliza akanipandia hewani akawasha moto vilivyo [emoji23][emoji23].. tena kwa msisitizo akapayuka "SIO KWA HELA YANGU!, SIO KWA HELA YANGU!!"

Kusema ukweli nilivunjika sana moyo yani hapa saivi nnavyoandika nina zaidi ya miezi sita sijamtafuta mzee wala bimkubwa yani itokee sana wakipiga wao kwenye simu ya sister angu mkubwa wakiomba kuongea na mimi ndo huwa naongea nao tu hivo hivo kinafki lakini moyoni najikuta nawachukia sana wazazi wangu (Mungu anisamehe sijapenda ila depression inapelekea yote hayo)

Yani ukweli ni kwamba nimeathirika sana kisaikolojia nimekua mtu wa kujifungia tu chumbani siku nzima, hata darasani nashindwa kusimama mbele za watu nikazungumza yani itokee hata ka birthday party home nitajitungia tu kasafari ilimradi tu nisiwepo kwenye mkusanyiko wa watu.

Jambo linaloniumiza sana ni kwamba hakuna anayejali hali ninayopitia hata sister angu ninayeishi nae hapa ata akuone ni mwenye mawazo kiasi gani atakupita kama hakuoni jambo ambalo linazidi kuniongezea depression na kujiona sifai yani kwa kifupi sina mtu wa kumueleza hali ninayopitia. Ila yote kwa yote, shetani nae hachezi mbali maana wazo la kujiua limekua likinijia mara kwa mara lakini nashukuru Mungu amenisimamia mpaka leo sijachukua maamuzi magumu ..

Yote kwa yote naamini JF the home of great thinkers nitapata mawazo chanya yatakayo nisaidia kujua jinsi gani napambana na hali hii ya depression.

NB: Najua kuna wanaopitia magumu zaidi yangu ila amini usiamini mambo madogo madogo kama haya psychologically ni very draining yanaumiza.

#NAWASILISHA
Hakuna mkamilifu wote tunamapungufu ingawa tunazidiana ,,ikubal hiyo changamoto,,wapuuzie wote wanaokudis,,,Mungu ana makusudi nawe,,,kuna ambao hawana macho ,masikio ,vilema viwete,,unawachukuliaje kwa upande wako ,,huoni bado Mungu kakupendelea hayo masikio kuzidi centremeter kadhaaa ndo unakuwa hivo,,badilika ndg,hiyo ni changamoto ndogo sana ,,jikubal na wapuuzie hao wapuuz ,maisha yaendelee,
 
Back
Top Bottom