ngoja nikuambie, kweli kabisa sio ya kutunga, kuna familia moja, baba na wanawe wana masikio makubwa kweli, kiasi ambacho wakitembea mbele wewe ukiwa nyuma unachokiona ni masikio kwao kwanza, na wapo okay tuu. kwenye mitandao wamejaa teleee hawakosekani.
sasa siku moja, mtoto wao mmoja akanambia, unajua sababu gani mama angu nywele zake huwa anaziachia upande wa kulia na nyengine upande wa kushoto? (maama ake ana nywele ndefu), nikamwambia sijui, akanambia mama angu ana masikio makubwa sana , anayaficha yasionekane kama hivi masikio yangu yalivyo, akacheka sanaa, akanambia tumepata masikio ya mama etu sisi, hapo baba yao masikio yao sio mchezo, ila watoto wanaona ya mama yao yamezidi kabisa kwa vile anayaficha.
nikasema wow! kumbe hii familia nzima ina masikio makubwa, ila ni happy family, kwa sababu hawajali kabisaaa ( mama tuu ndio style ya nywele ndo hivyo tene)
kwa kukunasihi, wewe usijali kabisa songa mbele na ujue tuu binaadamu tumeumbwa tofauti kabisaa na asiyekuwa na hili ana lile.
mimi nimeshapata matatizo ya kuchokozwa , na mbaya zaidi kuna siku ambayo hiyo iliniumiza kweli mwalim wa darasa alinita jina baya kwa sauti mbele ya wanafunzi wote. kwa vile nilikuwa mwema kwa wanafunzi wenzangu, hawakucheka, ila iliniuma sana,
katika maisha jitihada za kimaisha zitapelekea kupendwa sana na watu wote vyovyote utakavyokuwa, uwe na heshima, ujue tuu una neema nyingi sana katika mwili wako, na ushukuru neema hizo, ukitaka kujua kuwa wewe upo normal. ingia youtube, uone viumbe ambavyo unaweza kustuka sana,
HILO TATIZO LA KUTAKA KUJIUA ACHANA NALO KABISAAA