Depression inaniathiri, nakaribia kujiua

Depression inaniathiri, nakaribia kujiua

hilo tukio la kwanza mimi naona ni kawaida ningepotezea.

hilo la pili huyo msichana ningemzibua kofi ambalo bila shaka asingesimama kabla ya dk5 na hako kajamaa kake kakileta ubabe tungemalizana kiume kufa kupona either unipige au nikunipige mpaka nihakikishe wewe sio threat kwangu tena.
niwe clear sitaki utani kabisa juu ya chochote kinachonihusisha mimi yaani huwezi kunijugde vibaya alafu ubaki salama nakuangalia tu au nicheke hapana tunamalizana sababu wewe ndio umechokoza vita.
kiuhalisia ningekuwa wewe huyo msichana asingeweza kuniangalia usoni hata mara mbili hata kama masikio yangu yangekuwa kama dishi la azam au dstv.

hilo namba tatu ningewafata hao jamaa then ningewauliza warudie walichokisema huku nipo serious na sura ambayo hata bundi angeacha kukuangalia kwa uoga.
alafu ningescan chochote kutoka kwenye miili kama ni mikono au pua kubwa then ningewarudishia disstrack ambayo wasingeamini alafu kama tungemalizana kwa maneno au vinginevyo trust me wasingerudia tena hiyo tabia mbovu.

kuhusu hilo la mwalimu huyo mwalimu ningejipanga kwenye somo lake then ningemtafutia siku nimdharirishe kwenye somo lake mwenyewe then heshima ingekuwepo au anichukie.


mimi ni 17 mwembamba kiasi ila ni 6feet pia mpole kama hunijui ila ukinijaribu utafurahi hakuna mtu anayejaribu kunichezea au kunitania to be honest watu wazima wengi ninapoishi wananiheshimu au wengine kunichukia na kuniogopa, vyote hivyo sio coincidence bali ni life style niliyoipanga mwenyewe kwa kujua kucheza na akili za watu na kuwazidi akili.

sababu kabla nilikuwa kama wewe kiufupi ni kuweza kujiamini na kupandikiza fear kwenye akili zao badala ya wao kupandikiza fear kwako then unabaki na hiyo aura. pia kujua tabia za watu na akili zao na kujua weaknesses zao na kujua anachokifikiria mtu hivyo unajua unaplay nae vipi, kuna mengi ya kujua kuhusu binadamu then hatokupa shida ni kama mbwa tu au mnyama mwengine yoyote wa porini.
mbwa anaweza kuwa chini yako ni sababu umemzidi akili vivyohivyo kwa binadamu considering binadamu naye ni mnyama tu.
kuna movie inaitwa joker ni movie nzuri inayoonyesha watu wema wanavyogeuka wabaya kutokana na jamii mbovu kama yako.

kuna mengi ila kiufupi wewe ni mpole au una mwonekano wa kipole na hujiamini bila shaka hivyo watu wanatake advantage.
sababu wanajua you can't fight back.

mimi sio psychologist ila nina experience hivyo najua ninachokiandika.
 
Dogo Avatar Utoto pia unakusumbua... Deal with your own life..tafuta pesa uone kama hujasifiwa.. utasikia yule mkaka handsome ana masikio flani hivi amazing...
 
Pole sana ndugu.

Mimi pia nimepitia changamoto kama yako.Naambiwaga nina uume mkubwa kama wa punda
 
Dogo vipi aisee, hebu tulia hizo ni mambo ndogo sana na ujue walimwengu hawaishi yao. Hata ukifanya surgery kesho na kesho kutwa utataniwa kuhusu lingine.
Hebu take easy aisee maisha yana mengi zaidi ya hayo.
 
Mdogoangu Kwanza jikubali kwamba hakuna kama wewe popote pale kubali muonekano wako,jifunze kupuuza maneno unayosikia,halafu pia unapokuwa haupo shule tafuta kofia(kepu) zile pendelea kuvaa,mwisho kazana na masomo ukipata pesa hayo yote yanabaki historia
 
Habari za muda huu wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, mimi ni kijana wa kiume miaka 19 kwa muda mrefu sana nimekua nikisimbuliwa na depression "great depression" inayonifanya kutoyafurahia maisha na kujiona kama mtu anayeishi kwa bahati mbaya au labda sikustahili kuwepo duniani maana nimekua ni mtu wa kuchukiwa na watu mbali mbali either ninaowafahamu au hata wale ambao siwafahamu kwa sababu tu ya muonekano wangu hali iliyopelekea hata kujichukia mwenyewe.

Binafsi muonekano wa masikio yangu sio wa kawaida, kwani yametokeza sana kutokea usawa wa kichwa yani ni dizaini kama popo hivi (bat ears) hali inayopelekea kuwa bullied kila ninapokwenda, kuitwa majina yasiyofaa hata na watu nisiowafahamu, na wengine kwenda mbali zaidi kuukashifu uumbaji wa mwenyezi mungu.

Yafuatayo hapo chini ni baadhi tu ya matukio mengi niliyoyapitia so far ambayo sio siri yananila sana ndani kwa ndani;

✓ Ilikua siku ya jmosi asubuhi nimejiandaa nikasepa skonga Ile kufika nikazuiliwa kuingia simply because kulikua na rule kwamba mwanafunzi yeyoye ambaye ni day scholar siku za jmosi alitakiwa avae casual wear ambayo ni red and black ambavyo Ilikua tofauti kwangu mimi. Basi ikanibidi nivunge tu pale nje, baada ya muda kidogo akaja dem flani hivi wa form 2 (mimi nilikua form 4) basi katika kupiga stori mbili tatu na washkaji zangu wengine wawili tukaamua tutimbe maeneo flani (kupoteza muda of course,Ilikua bado asubuhi kurudi home Ilikua jau).

Kwenye mida ya kama saa nane hivi mchana wale washkaji zangu wawili wakaaga wakasepa nikabaki na yule demu ambapo pia aliniambia nimsindikize kwenye kituo cha daladala asepe na hapo ndipo msala ulipotokea, Ilikua hivi wakati tunatembea kando ya barabara alitokea jamaa flani kwa nyuma yetu akiwa kwenye bodaboda iliyokua ikitembea kwa mwendo wa taratibu, kimuonekano ni mtu mzima ambaye hakosi kuwa na mke na at least watoto wawili.

Kusema ukweli yule jamaa alinidhalilisha sana mbele za watu yani sijui hata nilimkosea nini au kosa langu nini mpaka afikie hatua ya kunifanyia kitendo cha kinyama namna Ile. Alianza kwa kucheka kwa nguvu sana kisha aliongea maneno ambayo yaliniumiza sana na nukuu .. " [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hivi hujaona wengine, na ex wako amesemaje kuhusu hili" hayo ni baadhi tu ya mengi aliyoyasema akimwambia yule dem. Kusema ukweli nilifedheheka sana mbele za watu, nilirudi home nikajifungia chumbani nikalia sana, sikuwa hata na hamu ya kukutana tena na yule dem jtatu skonga.

✓ siku hiyo baada ya kumaliza michosho ya home hapa nikawa sina chengine cha kufanya nikaamua ninyooshe miguu kitaa, sikufika ata hatua 20 nikakutana na kidem flani kikiwa na boyfriend wake.. aisee maneno yaliyomtoka yule dem kusema ukweli yaliniuma sana, alianza kwa kunishangaa kisha akasema " eeh Mungu anisaidie nisizae mtoto anayefanana kama huyu" . Kusema ukweli niliishiwa nguvu miguu ikanyong'onyea nikaamua tu nirudi home nikalale ..

✓ siku hiyo nikiwa town naelekea kituo cha daladala nisepe home kuna jamaa wawili nikawasikia wanaongea .. mmoja akimuuliza mwenzie " hivi mtu kama huyo unaweza kumuozesha binti yako ?" Nikageuka ghafla nikakuta ameninyooshea kidole . Dah nilicheka tu ila nikachukulia easy tu [emoji23][emoji23]

NB: hii imenitokea mara nyingi sana ndo maana nilichukulia kawaida yani hayo maneno nilisha yazoea ..

✓ kuna mwalimu aliwahi kuniambia mbele ya darasa zima kuwa sifanani na binadamu .. walinicheka sana wanafunzi wenzangu siku Ile [emoji1787][emoji1787]

✓Hayo ni baadhi tu ukiachana na yale madogo madogo kwa mfano unaweza ukawa unaongea na mtu ukimwangalia usoni utagundua ni dizaini kama anakucheka hivi ( japo sina uhakika kama ni kweli au najishtukia ), kingine pia sijui kama kuna jina baya au la kudhalilisha ambalo sijawahi kuitwa ..

Katika pitapita zangu mtandaoni nilikutana na hospitali moja Nairobi ambayo inajihusisha na cosmetic surgery mbali mbali ikiwemo Otoplasty ( ear shaping surgery). Basi nikaamua niwashirikishe wazazi wangu nione kama labda naweza kupata msaada wowote ukizingatia kwamba bei yake ni affordable ( japokua nikiri kwamba hii Ilikua last option kwangu), kwa jinsi nilivyo teseka sikua na jinsi.

Wazazi walikuja na response ambayo sikuitarajia kwani walinigomea katakata kwa hoja zisizo na mashiko sijui Michael Jackson and the like .. kilichoniuma zaidi bi mkubwa asubuhi na mapema akampigia kaka yangu mkubwa kunishtakia, bro nayeye alivyo mweupe kichwani bila ya kuuliza akanipandia hewani akawasha moto vilivyo [emoji23][emoji23].. tena kwa msisitizo akapayuka "SIO KWA HELA YANGU!, SIO KWA HELA YANGU!!"

Kusema ukweli nilivunjika sana moyo yani hapa saivi nnavyoandika nina zaidi ya miezi sita sijamtafuta mzee wala bimkubwa yani itokee sana wakipiga wao kwenye simu ya sister angu mkubwa wakiomba kuongea na mimi ndo huwa naongea nao tu hivo hivo kinafki lakini moyoni najikuta nawachukia sana wazazi wangu (Mungu anisamehe sijapenda ila depression inapelekea yote hayo)

Yani ukweli ni kwamba nimeathirika sana kisaikolojia nimekua mtu wa kujifungia tu chumbani siku nzima, hata darasani nashindwa kusimama mbele za watu nikazungumza yani itokee hata ka birthday party home nitajitungia tu kasafari ilimradi tu nisiwepo kwenye mkusanyiko wa watu.

Jambo linaloniumiza sana ni kwamba hakuna anayejali hali ninayopitia hata sister angu ninayeishi nae hapa ata akuone ni mwenye mawazo kiasi gani atakupita kama hakuoni jambo ambalo linazidi kuniongezea depression na kujiona sifai yani kwa kifupi sina mtu wa kumueleza hali ninayopitia. Ila yote kwa yote, shetani nae hachezi mbali maana wazo la kujiua limekua likinijia mara kwa mara lakini nashukuru Mungu amenisimamia mpaka leo sijachukua maamuzi magumu ..

Yote kwa yote naamini JF the home of great thinkers nitapata mawazo chanya yatakayo nisaidia kujua jinsi gani napambana na hali hii ya depression.

NB: Najua kuna wanaopitia magumu zaidi yangu ila amini usiamini mambo madogo madogo kama haya psychologically ni very draining yanaumiza.

#NAWASILISHA
Wazazi wako hali zao kiuchumi zipoje ? Wewe ni mtoto wa mwisho kuzaliwa, ama unamdogo wako ?. Wakati ukijibu maswali hayo zingatia pia ndugu zako ni vigumu kukulea au kukuchukua kama mtoto wao, huwenda wewe unaona hizo gharama ni ndogo kwa adha uipatayo lakini kimsingi hizo gharama(za upasuaji - Nairobi) zikawa kwao ni jambo lisilo wezekana.
 
Pole sana mi watu walikua wananambia nimelegea kama mwanamke mara nina damu imelela simply nilikua nacheka tu ,sasa weee ishi maisha yako jaribu kuwa na low cycle hakuna aleikamilikaa,ukijiua unamkosoa muumba wako,na pia embu acha usenge .mamayo haujuia hii miili yetu ni ya muda tu inaenda ishia ktk udongo hata uwe mzuri kiasi gani so tafuta elaaa
 
Una mawazo ya mgando sana mkuu...Mgoogle jamaa anaitwa Seal "Kipande Kimeshake" lakini anachukua warembo "wakare" sana ,itoshe kusema tafuta pesa.
 
Hizo hasira usizipeleke kwenye mawazo ya kujiua peleka kwenye mawazo ya kutafuta pesa kwanza mfano mdogo si unaona diamond sahiv hata wenye midomo midogo wanaiga kuwa na midomo mikubwa ili wafanane nae
 
Atatafutaje hela mkuu wakati ni mwanafunzi na ni mtoto?
Mkuu labda sababu point yangu ilikuwa fupi sana, nilikuwa na maana in the future afanye kazi vya kutosha apate hela.... Na hata ukiangalia point ya hela imekuwa mwishoni na ni fupi. Asante mkuu.
 
Kwanza ujijue uko tofauti,ambayo ujue ni kawaida kuwa tofauti,kila mmoja anatofauti yake,zingine zinaonekana kama yako,zingine hazionekani kama wenye uume mkubwa kupita kawaida au mdogo kama nukta. Ukiyajua hayo enjoy your life,ishi kama hawapo watu,tafuta fursa kwa kuwa nirahisi kwako kuwa maarufu utafanikiwa. Jipe jina la utani kabisa "masikio".
 
Sio huyo tu mkuu hata beyonce nae ana alishwahi kusema kipindi anasoma watu walimtania sana na kumcheka kuhusu muonekano wake wa masikio.

Tutoke huko tuje hapa bongo "harmorapa" angalia jinsi watu walivyokua wanamshambulia, kumcheka, kumtukana wengine kumfananisha na nyani na watu wakacheka na kufurahi. Mbaya zaidi ni Tanzania nzima sio mtaa mmoja tu. Mkuu simamia unachokiamini ziba masikio usiskie maneno yao ukiwa mnyonge zaidi na wao wanapiga hapo hapo.
 
Back
Top Bottom