Depression inaniua

kwanza kabisa Lovie lazima ujue kuwa hakuna gumu linalodumu kwa muda mrefu, hata liwe gumu kiasi gani, fahamu kuwa kiza kitapita na jua litawaka tena..!!

Yes, umeibiwa kazini, you gotta first thankful hata unacho cha kuibiwa, kuna watu hawana hata hiyo kazi Lovie, hawana hata hiyo Pesa ya kuibiwa, na bado hawakati tamaa, wanatabasamu, wana tumaini na wanaamini ipo siku itakuwa sawa...!

Jifunze kwanza kuwa na moyo wa shukrani hata kama hali ni ngumu kiasi gani, kinachotutesa siku zote siyo hali zetu hapana, tunateswa na 'attitude' zetu - namna tunayachukulia matatizo yetu, jambo likitokea kwenye maisha yako unalibebaje, unahisi umebeba dunia sivyo.!?? Hiyo itakuumiza sana..!!

Wameiba Pesa right..?? Hawajaiba uzima wala afya yako Lovie, hawajaiba mikono yako ya kupambana tena, kwanini unaruhusu waibe na amani yako..?? Waondoke na furaha yako..?? till date Pesa zimepotea ngapi..?? uliwahi kufa toka umeanza poteza Pesa..? Hell nuh'..!!

start from the scratch, kisha pambana tena, tena zaidi ya mwanzo, tukianguka kwenye tope tukachafuka, hatulali kwenye tope milele, tunanyanyuka tunakung'uta tope tunasonga mbele, wakati umekaa hapa unalia kwa kila kilichopotea, maisha hayasimami yakakungojea umalize kwanza kulia, hapana mamaa, watu wanaendelea mbele na maisha yao, hasara hapa inakuwa ni yako..!!

this Life is 100% You Vs. You, kuanzia sahii, badili kabisa namna unaichukulia kila situation inayopita kwenye maisha yako, Jifunze kuliona tatizo in a very Positive Version, Yes, hili limekuja na limetokea lakini najua limetokea ili nipambane zaidi, halijaja kukurudisha nyuma, Limekuja kukuongezea ujasiri, kuna wakati matatizo yanakuja ili kutuandaa na baraka kubwa zaidi ya pale tulipokuwepo,

wewe ni dhahabu, na dhahabu haiwezi ng'aa mpaka ipite kwenye moto mkali, Kukata TAMAA ni Mwiko Lovie, unakata tamaa..?? Umeichungulia kesho yako ukaiona inafananaje..?? Unakata tamaa kwani ni mwisho wa maisha yako..!!?? Usimpe shetani nafasi kwenye maisha yako kamwe..!!

Mungu akutie nguvu, akufariji, akupe tabasamu na aiponye nafsi yako, ALL IS WELL SWEETHEART..!!

The Monk
 
Asante sana mummie❀️
 
Dada ubarikiwe kila unachogusa kiwe chenye nuru umeandika maneno ambayo kila neno limejaa tumaini 😍
 
Pole sana waone wataalamu hata humu wapo utapata Muongozo
Hata wewe unaweza kumsaidia mkuu, haitajiki taaluma kumpa mtu neno la kumjaza matumaini, tena wenye taaluma ndiyo watamchanganya kabisa maana ataanza kutumia vitu vya kitaaluma zaidi na ndiyo kumchanganya kabisa,

wakati wewe mkuu huna taaluma utaweza kumsaidia kikawaida tu na akajazwa, chukua fursa ya kusaidia mmoja katika jamii kuokoa maisha yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…