Depression inaniua

Depression inaniua

Amen love.
Kuna store hua naweka vitu vyangu vya kazi.
Nikipata harusi au sherehe yoyote pesa nyingine nanunua vitu baadhi ambavyo sina.
Sasa dear nimekuta makufuli yameegeshwa na vitu vya muhimu vimebebwa.
😢😢

Mara ya kwanza 2021 nilifungua duka la nguo tena nikaibiwa nikaanza kurandaranda kazi.
Pole sana wewe ni mpambaji, mc, mpishi ama unafanya vyote?
 
Hii inaitwa Double standard toka kwako,

Vipi yeye kunijibu mimi kifedhuli kua nibalehe nitoke Nyumbani alikua sawa? Ulifurahia yeye kuniambia hivyo? Kwanini yeye hukumwambia kua kuniambia vile ilikua ni dharau na sio sahihi tena kwa mtu usiyemjua? Mimi nampokea mtu kama anavyokuja,alileta lugha ya kejeli kwangu ikabidi na mimi nimpokee kama alivyokuja
Nimekuelewa, naomba unisamehe kwa kukaa upande mmoja.
 
Lovelovie unapitia kitu kinaitwa wanaume wa jf umiza ubongo. Hawajui wanataka nini kila daily wanakuaminisha humu kuna ndoa ila humu hakuna ndoa . Ila hawasemi wengi ni mariooo tu nawanakupiga na vitu vizito hadi unazima kimaukweli ushauri wangu kunywa maji mengi anza na kusali muombe Mungu msamaha umrudie yeye anaweza na anajua unapitia nini msirikishe ita roho mtakatifu akusaidie uweze kupata njia ile sahihi kwako atakuja wakwako hatojali wewe ni single mom .Good day usimshirikushe mtu wewe loa ba Mungu wako anatosha abafariji kuliko mtu yeyote.
Kasema kaibiwa haya ulio andika umeyatoa wapi mkuu?
 
Namba ya mtu kuweka hapa hakuna shida mkuu? Au ndiyo kazi zake hizo
Haina shida mkuu ndio kazi yake. Nmeweka ili na wengine wenye shida na uhitaji wa huduma hiyo wanufaike pia. Huyo ni daktari na anaipenda na kuifanya kazi yake vyema.
 
kwanza kabisa Lovie lazima ujue kuwa hakuna gumu linalodumu kwa muda mrefu, hata liwe gumu kiasi gani, fahamu kuwa kiza kitapita na jua litawaka tena..!!

Yes, umeibiwa kazini, you gotta first thankful hata unacho cha kuibiwa, kuna watu hawana hata hiyo kazi Lovie, hawana hata hiyo Pesa ya kuibiwa, na bado hawakati tamaa, wanatabasamu, wana tumaini na wanaamini ipo siku itakuwa sawa...!

Jifunze kwanza kuwa na moyo wa shukrani hata kama hali ni ngumu kiasi gani, kinachotutesa siku zote siyo hali zetu hapana, tunateswa na 'attitude' zetu - namna tunayachukulia matatizo yetu, jambo likitokea kwenye maisha yako unalibebaje, unahisi umebeba dunia sivyo.!?? Hiyo itakuumiza sana..!!

Wameiba Pesa right..?? Hawajaiba uzima wala afya yako Lovie, hawajaiba mikono yako ya kupambana tena, kwanini unaruhusu waibe na amani yako..?? Waondoke na furaha yako..?? till date Pesa zimepotea ngapi..?? uliwahi kufa toka umeanza poteza Pesa..? Hell nuh'..!!

start from the scratch, kisha pambana tena, tena zaidi ya mwanzo, tukianguka kwenye tope tukachafuka, hatulali kwenye tope milele, tunanyanyuka tunakung'uta tope tunasonga mbele, wakati umekaa hapa unalia kwa kila kilichopotea, maisha hayasimami yakakungojea umalize kwanza kulia, hapana mamaa, watu wanaendelea mbele na maisha yao, hasara hapa inakuwa ni yako..!!

this Life is 100% You Vs. You, kuanzia sahii, badili kabisa namna unaichukulia kila situation inayopita kwenye maisha yako, Jifunze kuliona tatizo in a very Positive Version, Yes, hili limekuja na limetokea lakini najua limetokea ili nipambane zaidi, halijaja kukurudisha nyuma, Limekuja kukuongezea ujasiri, kuna wakati matatizo yanakuja ili kutuandaa na baraka kubwa zaidi ya pale tulipokuwepo,

wewe ni dhahabu, na dhahabu haiwezi ng'aa mpaka ipite kwenye moto mkali, Kukata TAMAA ni Mwiko Lovie, unakata tamaa..?? Umeichungulia kesho yako ukaiona inafananaje..?? Unakata tamaa kwani ni mwisho wa maisha yako..!!?? Usimpe shetani nafasi kwenye maisha yako kamwe..!!

Mungu akutie nguvu, akufariji, akupe tabasamu na aiponye nafsi yako, ALL IS WELL SWEETHEART..!!

The Monk
Ubarikiwe mpaka ushangae
 
Back
Top Bottom