Depression Itaniua

Depression Itaniua

Nyinyi si ndiyo mnakuwaga motiveshoni spika kwa majobulesi humu, ili wajiajiri? Umeona moto wake.
Hahaaaa huwa nawaambia watu life la kitaa ni nioko ,sasa imagine magraduate jobless wanamaliza vyuo wanasugua benchi ten years tena bila support yeyote wala Mtaji wala asset yeyote wala connection yeyote ya kupata kipato , qmama£ . Hawa wenye ajira Wana mitaji na assets hata za kukopa na connections mbalimbali Ila bado wanalilia ajira .Huyu ndugu yenu kamaliza miezi tisa Tu kitaa na Mtaji juu kachoma sasa hivi analia ,sasa imagine Sisi tusio na ajira miaka yote hiyo msoto tunaopitia , mpaka tumekuwa maninja kabisa , yaani unapigwa na msoto mpaka unaota sugu qmama£

Halafu kumer mmoja anawananga jobless , jobless tujengewe mnara kabisa na tuvikwe nyota
 
Yaani mkuu una mke na bado unakuwa depressed?
Sasa mkuu kama hujamshirikisha mkeo nashauri umshirikishe na umwambie kila kitu, mke ndio mtu pekee anayekujua vizuri na ndio mtu pekee atakayekupa faraja ya kweli kwenye nyakati ngumu za maisha ili upambane zaidi na hilo ndio dhumuni kuu la ndoa. na hapo ndipo nguvu ya mwanamke inapoonekana na hilo ndio lengo kuu la uwepo wa mwanamke duniani.

Lakini kwa kuwa umekuja huku kwa wanaume wenzako basi tambua tu utapata ukweli na uhalisia mchungu wa maisha, trust me niliwahi kuwa na matatizo makubwa tena ya kutisha ambayo yangekukuta wewe mkuu bila shaka ungekuwa kichaa. hayo yako ni madogo sana. tena mimi hakuna aliyenionea huruma wala kunisadia chochote hata pole na ikawa kama mimi ndio mwenye makosa wakati ni innocent lakini sikukaa chini kulialia na kuomba faraja NO. nilipigana kwa hasira na uchungu. I fought back even harder.

Naona unaomba neno la faraja, binafsi sikuonei huruma wala kukupa pole kama kila mtu anavyofanya au kukupa moyo kwamba mungu atakusaidia ili upate nguvu ya kupambana, sababu nguvu ya kupambana inatakiwa kutoka ndani ya mtu binafsi yeye mwenyewe na sio kwa watu wengine. wewe ulizaliwa peke yako na utakufa peke yako sasa vipi hawa watu wanaokupa pole na kukufariji sasa hivi wakiwa hawapo? utafanya nini? je utajiua? au utalia?

Sikuonei huruma sababu najua matatizo ni sehemu ya maisha na uchungu wa maisha ndio maana ya maisha na najua jinsi gani dunia ilivyo mbaya na katili na watu walivyo wabaya na wanafiki wenye dhuruma isiyoelezeka. ni Survival of the fittest, dhaifu watakanyagwa na wenye nguvu, na wenye nguvu pekee ndio watakaobaki.

Sasa nakwambia ukweli na uhalisa wa maisha man to man.
Ni kwamba mwanaume hakimbii matatizo wala kulialia na kujiua alafu kuacha familia yake iteketee peke yake.
Ni muoga, mpumbavu na mjinga pekee anayeweza kuchukua mtoto wa watu kutoka kwao kwenye maisha ambayo labda yalikuwa mazuri alafu kumzalisha watoto na kumpa mzigo mzito na yeye mwenyewe kujiua au kufa kwa depression na kuacha huyo mwanamke na maumivu makali na majuto juu yako, kitu kichungu zaidi ni kwamba bila shaka mkeo ataolewa tena na mwanaume mwingine ambaye atalea familia yako. je uko tayari kuona watoto wako na mkeo wakilelewa na mwanaume mwengine? mwanaume mwenzako?
Mimi sijui.

Kama ulikuwa unaona wewe hauna uwezo wa kujipambania na kumpambania huyo mwanamke basi usingemuoa ungesubiri kufa peke yako, lakini hapana, ulioa sababu uliamnini ungeweza kumuhudumia.
Sasa thibitisha hilo au kila nilichokiandika mimi hapa kitakuja kutokea kweli, na kwakua hatujuani basi tambua wala sikutanii mkuu.

Mwanaume anatakiwa kutokata tamaa na sio kulialia kwa kuomba faraja na kutaka huruma, anatakiwa kusimamia misimamo yake na kamwe isiyumbishwe wala kuvunjwa na yoyote yule. atapambana na kupigana mpaka tone la jasho la mwisho la ushindi.

Kaa chini fikiria kwa makini na ufanye unachoona kinafaa kwako na familia yako na kuwa tayari kupokea matokeo mabaya yasiyofurahisha. baba ndio tegemo la familia wewe ukiwa dhaifu je mkeo na wanao wawe vipi na wafanye nini?
Siku zote tambua maisha hayako fair na hakuna atakayekuonea huruma, matatizo yapo ili yatatuliwe na sio kuyakimbia au yatakukimbiza na kukumaliza wewe.

Binafsi sipendi kuomba ushauri wala sijawahi kuomba ushauri sababu ninakuwa na uhakika na maamuzi yangu siku zote na sitokubali mtu yoyote aniamulie au aniambie nini cha kufanya japo nitamsikiliza mama na mke wangu pekee kwa asilimia 1%, namaanisha 1% kama ilivyo.

Kuna Mwanaume anaitwa Horatius, yeye alisimama katikati ya daraja peke yake dhidi ya jeshi zima.
Namaliza na alichokisema.
"To every man upon this earth Death cometh soon or late. And how can a man die better Than facing fearful odds, For the ashes of his fathers, And the temples of his Gods.”
Napenda wanaume wa hivi sio limwanaume linajiliza liza eti maisha magumu au linaomba wanawake hela
 
Hilo tatizo ni dogo sana, watu Wana matatizo zaidi yako na still Wana matumaini, bora afya.
Biashara zote ni rahisi kwenye makaratasi. Mimi kabla ya kusimama jumla ya pesa nilizopoteza zinafika milioni 300 lakini, sikuhesabu kama ni hasara bali nimelipa tuition ya kupata uzoefu wa maisha. Nasonga
 
Kuna watu wana roho ya Ibilisi kabisa.
Mateso unayoyapitia ukienda kwa mitume na manabii bado watakupiga pesa tena.
Hope utapata kazi katika hiyo NGO na mambo yatakaa vizuri zaidi.
 
Umejificha kwa codes ila tumeshakujua .

Si uliacha kazi kwa mbwembwe na kiburi sasa unakuja kulialia humu nini? Ngoja sasa watu waanze kukugongea mkeo ndo utajua hujui halafu ule mpango wa kujifanya kushindana na majirani zako kimaisha ni ubwege wa kittoto psmbana fwala wewe na bado utaomba poooh.
Mkuu umemjua huyu mtu?
 
Waaambie bank huna kazi kwa hivyp wastopishe kucharge riba kwy marejesho na riba kuu pia,ili uje badae ulipe principal. Haya mambo yanazungumzika vizuri na hao jamaa.Nyumba haiwezi kuuzwa kwa kua haikua dhamana ya mkopo hilo lipo wazi unless km uliiitoa kama amana ya mkopo hapo wanaweza kuiuza kisheria ila bado unaeza weka zuio la kimahakama kwa kua bado unapambana kutafuta kazi,pili ukipata chochote we tupia huko bank waone unapambana kuclear deni lao.
Maisha lazima yaendelee jitoe ufaham piga mishe yeyote cha msingi huibi cha mtu.
 
naomba kuuliza je ntajuaje kama nina kpaj cha biashara? Je ina mana nkifanya biashara mbili tatu zkafeli ndo sna kipaji cha biashara?
Kipaji cha biashara ni kuwa na roho ngumu kama gamba la kobe na kujinyima. Mtu kama mimi ambaye nikiotea kibunda lazma nile kuku sikuhiyo ni ngumu sana ku manage biashara sababu money management ni zoezi gumu kwangu.

Labda iwe biashara ya mtaji mkubwa ambao ukiuza unit 1 unaweza ukala na kusaza kwa faida yake. Ndio ntadumu dumu.

Siwezi kuteseka na njaa eti kuna laki 2 tu ya kununulia gunia la mchele, si nanyofoa elfu kumi nakula kwanza 😂😂😂 kwa akili kama hizo hutoboi!
 
Hilo ni kosa kubwa sana atalifanya. Mie nina kanuni moja huwa siuzi asset hata kama nina njaa ya kuniua.

Roho ya kuuza uza vitu nilishaikataa kitambo sana baada ya kuona uzembe wa aina hio kwa mzee aliuza nyumba ya vyumba vitano kwa 7M mwanzoni mwa 2OOO's kwa kuendekeza njaa...Ile nyumba imepakana na ingine anayoishi kila nikienda home huwa naskitika tu sababu ingekuwepo leo asingekosa kuwa anakula kodi zake tu sahizi. Kama kuiuza hata 2010 tu ilikuwa inatoa hela 1O TIMES hela aliopokeaga.

Aliiuza afungue kampuni ila still kampuni haikufanikiwa nyumba ikaenda na kampuni ikamshindaga. Hawakuwahi kupata tender hata moja 😂😂😂. Hili linafundisha usiuze asset kwa sababu ya kuanzisha biashara lazma uyumbe.

Seven years ahead aka partner na mtu mwengine akafungua kampuni ingine ndio ikafanikiwa!
Poleni I feel what you go through
Uza nyumba then upange eneo cheap then Jitose kwa Biashara yenye mzunguko hope utatoboa vizuri.
 
Hilo ni kosa kubwa sana atalifanya. Mie nina kanuni moja huwa siuzi asset hata kama nina njaa ya kuniua.

Roho ya kuuza uza vitu nilishaikataa kitambo sana baada ya kuona uzembe wa aina hio kwa mzee aliuza nyumba ya vyumba vitano kwa 7M mwanzoni mwa 2OOO's kwa kuendekeza njaa...Ile nyumba imepakana na ingine anayoishi kila nikienda home huwa naskitika tu sababu ingekuwepo leo asingekosa kuwa anakula kodi zake tu sahizi. Kama kuiuza hata 2010 tu ilikuwa inatoa hela 1O TIMES hela aliopokeaga.

Aliiuza afungue kampuni ila still kampuni haikufanikiwa nyumba ikaenda na kampuni ikamshindaga. Hawakuwahi kupata tender hata moja 😂😂😂. Hili linafundisha usiuze asset kwa sababu ya kuanzisha biashara lazma uyumbe.

Seven years ahead aka partner na mtu mwengine akafungua kampuni ingine ndio ikafanikiwa!
yani suala la kuuza NYUMBA ALIONDOE KABISA AKILINI..
 
Back
Top Bottom