Depression Itaniua

Depression Itaniua

geresho la kata

New Member
Joined
Aug 5, 2022
Posts
3
Reaction score
39
Habari za leo wana GT.

Niende kwenye hoja ya msingi.
Kwa utambulisho huu mimi si mgeni humu ila ID nliyotumia ni mpya niliona nifungue hii ili nisiwezekujulikana na wanaoifahamu ID yangu iliyozoeleka hasa mke wangu.

Kwa hakika hapa nilipo nina msongo wa mawazo unanisumbua na ninahisi ninapoelekea sio pazuri, Miaka mitano nyuma nilichukua mkopo kwenye bank moja hivi hapa nchini. Huu mkopo nilichukua kwa udhamini wa mshahara wangu wa kipindi kile.

Kuna jambo lilitokea ofisini hivyo ilinibidi ni resign ndani ya 24hrs hivyo sikupata chochote pale ofisni, (hii nitakuja kuisimulia siku nyingine) lakini nilijipa moyo kuwa maisha hayatonisumbua kwa vile ile pesa nilianzsiha miradi mbalimbali.

Lakini bila kujua kuwa sina uzoefu na usimamizi wa hii miradi yangu niliingia kichwa kichwa mambo yalianza kwenda mrama. Miradi iliyumba mingine niliifunga ilinibidi niuzie gari yangu niweze kusimama tena , lakini bado kama vile nilijiongezea dhiki tu.

Sasa nina miezi 10 sijapeleka rejesho la bank, na bank wanapiga simu sana mpaka waliniambia nijitahidi niweke chochote kile ili nisiwekwe kwenye blacklist. Watoto wangu nimewarudisha shule za Kayumba, hela ya kula imekuwa changamoto kiasi kwamba natamani hata kufa ili nisione hawa watoto wangu wanavyoteseka.

Nafikiri niuze nyumba hii moja niliyobaki nayo ili tu nijaribu tena bahati yangu kwenye biashara zingine lakini nahofia hiyo biashara ikifilisika hawa watoto nitawaweka wapi.

Hofu kubwa niliyonayo ni hawa watu wa hii taasisi ya bank nao wasije wakaniuzia nyumba yangu maana nimeshavurugwa mpaka kila ninalowaza naona haliwezekani.

Kwa upande mwingine naendelea kutafuta kazi nimeshafanya interview sehemu nyingi tu lakini sijabahatika kuitwa, miezi mitatu iliyopita interview yangu ya mwisho niliambiwa nitaitwa kwa ajili ya kuanza kazi mwezi wa saba au wa nane. Lakini mpaka sasa hivi sioni faraja yoyote ile ya kuitwa kwenye hiyo taasisi ya kimataifa.

Wana GT naomba neno la faraja kutoka kwenu nifanyaje ili niweze kumudu hizi heka heka za maisha na hasira za watu wa bank wasije kunipeleka mahakamani na kunifilisi.
 
Hapo uliporesign ni private au government na imekuwaje ?binafsi naona kama isingekuwa na mkopo na nyumba unayo ungeficha aibu kwani ungetafuta pesa ya kula kwa kutumia gari kama Uber au bolt .

Nyumba ndo kila kitu Tena kama mkeo akikuunga mkono mpambane hata biashara ndogo mnaishi .

Mungu akusimamie ipo siku utaamka Tena inshallah
 
Hakika maisha yetu ni fumbo kama ni muumini basi Jitahid kujiweka karibu na Muumba sali na kesha ukimuomba Mungu hakika milango itafunguka na njia ya kutokea itapatika Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi InshaAllah.
 
Tuseme tu pole.

Mikopo ya benki inatesa sana, kwa hii miezi ambayo hujapeleka rejesho riba ya adhabu itakuwa imeshapaa.

Ungeweza uza hiyo nyumba ulipe deni la watu, kiasi kinachobaki kikusogeze, pole
 
pole sana

punguza kukaa peke yako na kama unaishi uswazi na ushenzini kama mimi jichanganye sana uswahilini utakutana na watu wana shida na matatizo mengi sana kuliko ya kwako hali itakayokusaidia sana kisaikolojia

pia imarisha sana mahusiano yako ya kiimani kwa kuswali na kuomba sana mola wako kwa kuwa hatupaswi kukata tamaa kwny neema za Mola wetu
 
Habari kaka nitakushauri kadiri ya maelezo yako;

1. Una panic burr kuhusu mkopo wa bank kwa udhamini wa mshahara, wambie kaz huna na ikpata utaendelea kulipa.. FYI black list ni baada ya miaka 7 na hawawez uza nyumba ambayo hukuweka kama collateral

2. Issue ya biashara, nakushauri anza nz biashara ambayo wewe unaona rahisi, kama kweli inatoka moyoni. Kurudi kazini ni kufeli upya kama kwel lengo lilikuwa kujiajiri

Sijui background yako; lakini kama una ndugu unaweza kopa chochote ukaanza kioambana na kama una mke lazima wote muwe watu wa mshike mshike... mke duka wewe kuparangana..
Naimani utasimama tena... Mungu atakusaidia kaka
 
Habari za leo wana GT.

Niende kwenye hoja ya msingi.
Kwa utambulisho huu mimi si mgeni humu ila ID nliyotumia ni mpya niliona nifungue hii ili nisiwezekujulikana na wanaoifahamu ID yangu iliyozoeleka hasa mke wangu.

Kwa hakika hapa nilipo nina msongo wa mawazo unanisumbua na ninahisi ninapoelekea sio pazuri, Miaka mitano nyuma nilichukua mkopo kwenye bank moja hivi hapa nchini. Huu mkopo nilichukua kwa udhamini wa mshahara wangu wa kipindi kile.

Kuna jambo lilitokea ofisini hivyo ilinibidi ni resign ndani ya 24hrs hivyo sikupata chochote pale ofisni, (hii nitakuja kuisimulia siku nyingine) lakini nilijipa moyo kuwa maisha hayatonisumbua kwa vile ile pesa nilianzsiha miradi mbalimbali.

Lakini bila kujua kuwa sina uzoefu na usimamizi wa hii miradi yangu niliingia kichwa kichwa mambo yalianza kwenda mrama. Miradi iliyumba mingine niliifunga ilinibidi niuzie gari yangu niweze kusimama tena , lakini bado kama vile nilijiongezea dhiki tu.

Sasa nina miezi 10 sijapeleka rejesho la bank, na bank wanapiga simu sana mpaka waliniambia nijitahidi niweke chochote kile ili nisiwekwe kwenye blacklist. Watoto wangu nimewarudisha shule za Kayumba, hela ya kula imekuwa changamoto kiasi kwamba natamani hata kufa ili nisione hawa watoto wangu wanavyoteseka.

Nafikiri niuze nyumba hii moja niliyobaki nayo ili tu nijaribu tena bahati yangu kwenye biashara zingine lakini nahofia hiyo biashara ikifilisika hawa watoto nitawaweka wapi.

Hofu kubwa niliyonayo ni hawa watu wa hii taasisi ya bank nao wasije wakaniuzia nyumba yangu maana nimeshavurugwa mpaka kila ninalowaza naona haliwezekani.

Kwa upande mwingine naendelea kutafuta kazi nimeshafanya interview sehemu nyingi tu lakini sijabahatika kuitwa, miezi mitatu iliyopita interview yangu ya mwisho niliambiwa nitaitwa kwa ajili ya kuanza kazi mwezi wa saba au wa nane. Lakini mpaka sasa hivi sioni faraja yoyote ile ya kuitwa kwenye hiyo taasisi ya kimataifa.

Wana GT naomba neno la faraja kutoka kwenu nifanyaje ili niweze kumudu hizi heka heka za maisha na hasira za watu wa bank wasije kunipeleka mahakamani na kunifilisi.
...'au wa Nane'!... Mwezi wa Nane ndiol Umeanza huu. Uwe na Imani. Watakuita TU. Pole Sana Kwa Yanayokusibu.
 
Labda utuambie ukweli, kazi uliresign ama ulikimbia?

Na ulikuwa private ama government?

Na mkopo ulichukua kwa dhamana ya muajiri ama nyumba?

Kama mdhamini wako alikuwa ni muajiri, basi alipaswa kabla hujaacha kazi awe ameclear hizo sintofahamu..

Kama dhamana uliweka nyumba basi hamna namna lazima uiuze kabla bank hawajaja kuifilisi..

BTW weka mkeka wa deni lako ili watu tuamini hili andiko lako.
 
Pole bro kwa masahibu lakini usijichanganye ukauza nyumba pambana hata kama mtashindia uji na watoto lakini pakulala patakuwepo, ukiuza nyumba mambo yakaenda mrama huna pa kulaza familia,huna chakula unadhani itakuwaje??
...na Benki waliamua kuipiga Mnada? SI Bora aiuze Mwenyewe apate Cha kusimama wakati akihangaika? SI ataweza kupanga?
 
Labda utuambie ukweli, kazi uliresign ama ulikimbia?

Na ulikuwa private ama government?

Na mkopo ulichukua kwa dhamana ya muajiri ama nyumba?

Kama mdhamini wako alikuwa ni muajiri, basi alipaswa kabla hujaacha kazi awe ameclear hizo sintofahamu..

Kama dhamana uliweka nyumba basi hamna namna lazima uiuze kabla bank hawajaja kuifilisi..

BTW weka mkeka wa deni lako ili watu tuamini hili andiko lako.
Ushauri mzuri sn

Awawahi benki

Anunue gari ist awe derevea bolt labda
Au heri bodaboda?
 
Pole sana mkuu, Ninaamini hichi ni kipindi cha mpito tu

Kuna watu nawafahamu walishawahi kupita katika hali kama yako ila waka bounce back na life likaendelea vizuri tu, kikubwa zaidi unahitaji kujiweka karibu na watu wako unaominiana nao kupata company
 
Back
Top Bottom