Depression Itaniua

Depression Itaniua

Habari za leo wana GT.

Niende kwenye hoja ya msingi.
Kwa utambulisho huu mimi si mgeni humu ila ID nliyotumia ni mpya niliona nifungue hii ili nisiwezekujulikana na wanaoifahamu ID yangu iliyozoeleka hasa mke wangu.

Kwa hakika hapa nilipo nina msongo wa mawazo unanisumbua na ninahisi ninapoelekea sio pazuri, Miaka mitano nyuma nilichukua mkopo kwenye bank moja hivi hapa nchini. Huu mkopo nilichukua kwa udhamini wa mshahara wangu wa kipindi kile.

Kuna jambo lilitokea ofisini hivyo ilinibidi ni resign ndani ya 24hrs hivyo sikupata chochote pale ofisni, (hii nitakuja kuisimulia siku nyingine) lakini nilijipa moyo kuwa maisha hayatonisumbua kwa vile ile pesa nilianzsiha miradi mbalimbali.

Lakini bila kujua kuwa sina uzoefu na usimamizi wa hii miradi yangu niliingia kichwa kichwa mambo yalianza kwenda mrama. Miradi iliyumba mingine niliifunga ilinibidi niuzie gari yangu niweze kusimama tena , lakini bado kama vile nilijiongezea dhiki tu.

Sasa nina miezi 10 sijapeleka rejesho la bank, na bank wanapiga simu sana mpaka waliniambia nijitahidi niweke chochote kile ili nisiwekwe kwenye blacklist. Watoto wangu nimewarudisha shule za Kayumba, hela ya kula imekuwa changamoto kiasi kwamba natamani hata kufa ili nisione hawa watoto wangu wanavyoteseka.

Nafikiri niuze nyumba hii moja niliyobaki nayo ili tu nijaribu tena bahati yangu kwenye biashara zingine lakini nahofia hiyo biashara ikifilisika hawa watoto nitawaweka wapi.

Hofu kubwa niliyonayo ni hawa watu wa hii taasisi ya bank nao wasije wakaniuzia nyumba yangu maana nimeshavurugwa mpaka kila ninalowaza naona haliwezekani.

Kwa upande mwingine naendelea kutafuta kazi nimeshafanya interview sehemu nyingi tu lakini sijabahatika kuitwa, miezi mitatu iliyopita interview yangu ya mwisho niliambiwa nitaitwa kwa ajili ya kuanza kazi mwezi wa saba au wa nane. Lakini mpaka sasa hivi sioni faraja yoyote ile ya kuitwa kwenye hiyo taasisi ya kimataifa.

Wana GT naomba neno la faraja kutoka kwenu nifanyaje ili niweze kumudu hizi heka heka za maisha na hasira za watu wa bank wasije kunipeleka mahakamani na kunifilisi.
pole mkuu, Ni wengi wanapitia hayo,
hila Kuna siku utayasahau yote hayo, hiyo Ni mitihani tu wala usikate tamaa mkuu, hila Kama unaona ukiuza nyumba na ukalipa deni la bank na wewe utabakia na hela ya kueleweka isiyopungua hata milion 30 au 40,
Mi naona sio mbaya ili uangalie biashara yakufanya isiyo na risk sana. Hila usikate tamaa Ni mitihani tu hiyo tumeumbiwa binadamu
 
Jambo kama hili sio rahisi sana kukutana na ushauri makini kutoka kwa Mtu ambaye hajawahi kupitia hayo.

Mimi siungani na wanaosema usiuze nyumba kama haswa ndio itakayokusaidia kuishi kesho.

Iwapo utajiridhisha ya kuwa kuna pesa nzuri unaweza kuipata kwa kuuza nyumba basi weka mipango yako mezani mapema ujue utafanya nini kwa kiasi unachokitarajia.

Na iwapo utachelewa sana kufanya uamuzi basi kuna hatari ya kulazimika kuuza nyumba ukiwa na presha kubwa ukaishia kuiuza hata kwa robo ya thamani halisi ya nyumba yako.

Kwenye maisha kila dakika moja iliyopo mbele yako ina thamani kubwa, ndani ya dakika hiyo moja kuna ufumbuzi wa changamoto yako...hivyo fanya kila unaloweza kuhakikisha unaifikia hiyo dakika moja...na kwa kusema chochote basi hata kuuza nyumba ni moja ya hayo.

Sasa kipi bora, kukaa chini na kuangamia kwa depression ukaiacha familia au kuuza nyumba ukatafuta mlango wa matumaini?.

Wakati unasubiria kufikia uamuzi wowote ni vizuri wewe na Mkeo mkaanza kufikiria cha kufanya kuingiza chochote hata kama ni shughuli ya chini kama kupika vitafunio, mihogo, karanga n.k.

Unapopita pale Mbezi ukawakuta wale wanaorundikana pale kuuza ubuyu na tambi wengi wamekutwa na hayo yaliyokukuta wewe ni vile tu huwezi kupita kwa kila mmoja na kumuuliza.
ASIUZEE NYUMBAAAA.. yani hilo wazo alifute kabisaaa bora kupambana kupata hela ya kulaaa sio ainginee kwenye masuala ya kodi tenaaa... kusema auze nyumba ili afanye biashara ambayo hana uhakika itamlipa vipi duuh bado ni ngumu
 
Yaani mkuu una mke na bado unakuwa depressed?
Sasa mkuu kama hujamshirikisha mkeo nashauri umshirikishe na umwambie kila kitu, mke ndio mtu pekee anayekujua vizuri na ndio mtu pekee atakayekupa faraja ya kweli kwenye nyakati ngumu za maisha ili upambane zaidi na hilo ndio dhumuni kuu la ndoa. na hapo ndipo nguvu ya mwanamke inapoonekana na hilo ndio lengo kuu la uwepo wa mwanamke duniani.

Lakini kwa kuwa umekuja huku kwa wanaume wenzako basi tambua tu utapata ukweli na uhalisia mchungu wa maisha, trust me niliwahi kuwa na matatizo makubwa tena ya kutisha ambayo yangekukuta wewe mkuu bila shaka ungekuwa kichaa. hayo yako ni madogo sana. tena mimi hakuna aliyenionea huruma wala kunisadia chochote hata pole na ikawa kama mimi ndio mwenye makosa wakati ni innocent lakini sikukaa chini kulialia na kuomba faraja NO. nilipigana kwa hasira na uchungu. I fought back even harder.

Naona unaomba neno la faraja, binafsi sikuonei huruma wala kukupa pole kama kila mtu anavyofanya au kukupa moyo kwamba mungu atakusaidia ili upate nguvu ya kupambana, sababu nguvu ya kupambana inatakiwa kutoka ndani ya mtu binafsi yeye mwenyewe na sio kwa watu wengine. wewe ulizaliwa peke yako na utakufa peke yako sasa vipi hawa watu wanaokupa pole na kukufariji sasa hivi wakiwa hawapo? utafanya nini? je utajiua? au utalia?

Sikuonei huruma sababu najua matatizo ni sehemu ya maisha na uchungu wa maisha ndio maana ya maisha na najua jinsi gani dunia ilivyo mbaya na katili na watu walivyo wabaya na wanafiki wenye dhuruma isiyoelezeka. ni Survival of the fittest, dhaifu watakanyagwa na wenye nguvu, na wenye nguvu pekee ndio watakaobaki.

Sasa nakwambia ukweli na uhalisa wa maisha man to man.
Ni kwamba mwanaume hakimbii matatizo wala kulialia na kujiua alafu kuacha familia yake iteketee peke yake.
Ni muoga, mpumbavu na mjinga pekee anayeweza kuchukua mtoto wa watu kutoka kwao kwenye maisha ambayo labda yalikuwa mazuri alafu kumzalisha watoto na kumpa mzigo mzito na yeye mwenyewe kujiua au kufa kwa depression na kuacha huyo mwanamke na maumivu makali na majuto juu yako, kitu kichungu zaidi ni kwamba bila shaka mkeo ataolewa tena na mwanaume mwingine ambaye atalea familia yako. je uko tayari kuona watoto wako na mkeo wakilelewa na mwanaume mwengine? mwanaume mwenzako?
Mimi sijui.

Kama ulikuwa unaona wewe hauna uwezo wa kujipambania na kumpambania huyo mwanamke basi usingemuoa ungesubiri kufa peke yako, lakini hapana, ulioa sababu uliamnini ungeweza kumuhudumia.
Sasa thibitisha hilo au kila nilichokiandika mimi hapa kitakuja kutokea kweli, na kwakua hatujuani basi tambua wala sikutanii mkuu.

Mwanaume anatakiwa kutokata tamaa na sio kulialia kwa kuomba faraja na kutaka huruma, anatakiwa kusimamia misimamo yake na kamwe isiyumbishwe wala kuvunjwa na yoyote yule. atapambana na kupigana mpaka tone la jasho la mwisho la ushindi.

Kaa chini fikiria kwa makini na ufanye unachoona kinafaa kwako na familia yako na kuwa tayari kupokea matokeo mabaya yasiyofurahisha. baba ndio tegemo la familia wewe ukiwa dhaifu je mkeo na wanao wawe vipi na wafanye nini?
Siku zote tambua maisha hayako fair na hakuna atakayekuonea huruma, matatizo yapo ili yatatuliwe na sio kuyakimbia au yatakukimbiza na kukumaliza wewe.

Binafsi sipendi kuomba ushauri wala sijawahi kuomba ushauri sababu ninakuwa na uhakika na maamuzi yangu siku zote na sitokubali mtu yoyote aniamulie au aniambie nini cha kufanya japo nitamsikiliza mama na mke wangu pekee kwa asilimia 1%, namaanisha 1% kama ilivyo.

Kuna Mwanaume anaitwa Horatius, yeye alisimama katikati ya daraja peke yake dhidi ya jeshi zima.
Namaliza na alichokisema.
"To every man upon this earth Death cometh soon or late. And how can a man die better Than facing fearful odds, For the ashes of his fathers, And the temples of his Gods.”
hivi unajua ni bora asingekuwa na mke????
 
Kwa sasa naweza nisiwe na cha kukufariji, lakini nina nafasi ya kukwambia ukweli kwamba, pamoja na ugumu wa unayoyapitia, yatapita na kuwaacha wote mkiwa salama.

Siku moja yote yatabaki stori, na utakuwa sehemu ya faraja kwa wengine wanaopitia changamoto mbali mbali.

Asante.
 
Acha kumdanganya mwenzako, mkopo unakua na bima kuweza kufidia pale ukifariki au kupata ulemavu unaopelekea usiweze kufanya kazi.

Cha msingi aendelee kuwa na mahusiano mazuri na benki, hawawezi kuuza nyumba Kwa vile haikua sehem ya dhamana.
Una ufahamu kidogo na mambo ya mikopo?

Insurance ni kinga dhidi ya kufariki, kufukuzwa kazi, ulemavu nk. Sio kufariki tu.
 
Habari za leo wana GT.

Niende kwenye hoja ya msingi.
Kwa utambulisho huu mimi si mgeni humu ila ID nliyotumia ni mpya niliona nifungue hii ili nisiwezekujulikana na wanaoifahamu ID yangu iliyozoeleka hasa mke wangu.

Kwa hakika hapa nilipo nina msongo wa mawazo unanisumbua na ninahisi ninapoelekea sio pazuri, Miaka mitano nyuma nilichukua mkopo kwenye bank moja hivi hapa nchini. Huu mkopo nilichukua kwa udhamini wa mshahara wangu wa kipindi kile.

Kuna jambo lilitokea ofisini hivyo ilinibidi ni resign ndani ya 24hrs hivyo sikupata chochote pale ofisni, (hii nitakuja kuisimulia siku nyingine) lakini nilijipa moyo kuwa maisha hayatonisumbua kwa vile ile pesa nilianzsiha miradi mbalimbali.

Lakini bila kujua kuwa sina uzoefu na usimamizi wa hii miradi yangu niliingia kichwa kichwa mambo yalianza kwenda mrama. Miradi iliyumba mingine niliifunga ilinibidi niuzie gari yangu niweze kusimama tena , lakini bado kama vile nilijiongezea dhiki tu.

Sasa nina miezi 10 sijapeleka rejesho la bank, na bank wanapiga simu sana mpaka waliniambia nijitahidi niweke chochote kile ili nisiwekwe kwenye blacklist. Watoto wangu nimewarudisha shule za Kayumba, hela ya kula imekuwa changamoto kiasi kwamba natamani hata kufa ili nisione hawa watoto wangu wanavyoteseka.

Nafikiri niuze nyumba hii moja niliyobaki nayo ili tu nijaribu tena bahati yangu kwenye biashara zingine lakini nahofia hiyo biashara ikifilisika hawa watoto nitawaweka wapi.

Hofu kubwa niliyonayo ni hawa watu wa hii taasisi ya bank nao wasije wakaniuzia nyumba yangu maana nimeshavurugwa mpaka kila ninalowaza naona haliwezekani.

Kwa upande mwingine naendelea kutafuta kazi nimeshafanya interview sehemu nyingi tu lakini sijabahatika kuitwa, miezi mitatu iliyopita interview yangu ya mwisho niliambiwa nitaitwa kwa ajili ya kuanza kazi mwezi wa saba au wa nane. Lakini mpaka sasa hivi sioni faraja yoyote ile ya kuitwa kwenye hiyo taasisi ya kimataifa.

Wana GT naomba neno la faraja kutoka kwenu nifanyaje ili niweze kumudu hizi heka heka za maisha na hasira za watu wa bank wasije kunipeleka mahakamani na kunifilisi.
Oya kataa kubali.

Kuna mpuuzi yuko nyuma ya maisha yako anakuroga
 
Kama ulichukua Mkopo Bank kwa Udhamini wa Mshahara wako iweje Bank waje wauze Nyumba yako??Dhamana yako wewe ni Ofisi ndio iliyokudhamini hivyo Bank hawawezi kuwa na Hati ya Nyumba yako
Na mikopo huwa ina bima huyu cjui hajui,mi niliwahi pita situation km yake, lakini kila wakipiga cm niliwaambia sihusiki wadeal na muajiri, hivyo hawakuwah kunisumbua tena napeta tu.
 
Poleni I feel what you go through
Uza nyumba then upange eneo cheap then Jitose kwa Biashara yenye mzunguko hope utatoboa vizuri.
 
Yaani mkuu una mke na bado unakuwa depressed?
Sasa mkuu kama hujamshirikisha mkeo nashauri umshirikishe na umwambie kila kitu, mke ndio mtu pekee anayekujua vizuri na ndio mtu pekee atakayekupa faraja ya kweli kwenye nyakati ngumu za maisha ili upambane zaidi na hilo ndio dhumuni kuu la ndoa. na hapo ndipo nguvu ya mwanamke inapoonekana na hilo ndio lengo kuu la uwepo wa mwanamke duniani.

Lakini kwa kuwa umekuja huku kwa wanaume wenzako basi tambua tu utapata ukweli na uhalisia mchungu wa maisha, trust me niliwahi kuwa na matatizo makubwa tena ya kutisha ambayo yangekukuta wewe mkuu bila shaka ungekuwa kichaa. hayo yako ni madogo sana. tena mimi hakuna aliyenionea huruma wala kunisadia chochote hata pole na ikawa kama mimi ndio mwenye makosa wakati ni innocent lakini sikukaa chini kulialia na kuomba faraja NO. nilipigana kwa hasira na uchungu. I fought back even harder.

Naona unaomba neno la faraja, binafsi sikuonei huruma wala kukupa pole kama kila mtu anavyofanya au kukupa moyo kwamba mungu atakusaidia ili upate nguvu ya kupambana, sababu nguvu ya kupambana inatakiwa kutoka ndani ya mtu binafsi yeye mwenyewe na sio kwa watu wengine. wewe ulizaliwa peke yako na utakufa peke yako sasa vipi hawa watu wanaokupa pole na kukufariji sasa hivi wakiwa hawapo? utafanya nini? je utajiua? au utalia?

Sikuonei huruma sababu najua matatizo ni sehemu ya maisha na uchungu wa maisha ndio maana ya maisha na najua jinsi gani dunia ilivyo mbaya na katili na watu walivyo wabaya na wanafiki wenye dhuruma isiyoelezeka. ni Survival of the fittest, dhaifu watakanyagwa na wenye nguvu, na wenye nguvu pekee ndio watakaobaki.

Sasa nakwambia ukweli na uhalisa wa maisha man to man.
Ni kwamba mwanaume hakimbii matatizo wala kulialia na kujiua alafu kuacha familia yake iteketee peke yake.
Ni muoga, mpumbavu na mjinga pekee anayeweza kuchukua mtoto wa watu kutoka kwao kwenye maisha ambayo labda yalikuwa mazuri alafu kumzalisha watoto na kumpa mzigo mzito na yeye mwenyewe kujiua au kufa kwa depression na kuacha huyo mwanamke na maumivu makali na majuto juu yako, kitu kichungu zaidi ni kwamba bila shaka mkeo ataolewa tena na mwanaume mwingine ambaye atalea familia yako. je uko tayari kuona watoto wako na mkeo wakilelewa na mwanaume mwengine? mwanaume mwenzako?
Mimi sijui.

Kama ulikuwa unaona wewe hauna uwezo wa kujipambania na kumpambania huyo mwanamke basi usingemuoa ungesubiri kufa peke yako, lakini hapana, ulioa sababu uliamnini ungeweza kumuhudumia.
Sasa thibitisha hilo au kila nilichokiandika mimi hapa kitakuja kutokea kweli, na kwakua hatujuani basi tambua wala sikutanii mkuu.

Mwanaume anatakiwa kutokata tamaa na sio kulialia kwa kuomba faraja na kutaka huruma, anatakiwa kusimamia misimamo yake na kamwe isiyumbishwe wala kuvunjwa na yoyote yule. atapambana na kupigana mpaka tone la jasho la mwisho la ushindi.

Kaa chini fikiria kwa makini na ufanye unachoona kinafaa kwako na familia yako na kuwa tayari kupokea matokeo mabaya yasiyofurahisha. baba ndio tegemo la familia wewe ukiwa dhaifu je mkeo na wanao wawe vipi na wafanye nini?
Siku zote tambua maisha hayako fair na hakuna atakayekuonea huruma, matatizo yapo ili yatatuliwe na sio kuyakimbia au yatakukimbiza na kukumaliza wewe.

Binafsi sipendi kuomba ushauri wala sijawahi kuomba ushauri sababu ninakuwa na uhakika na maamuzi yangu siku zote na sitokubali mtu yoyote aniamulie au aniambie nini cha kufanya japo nitamsikiliza mama na mke wangu pekee kwa asilimia 1%, namaanisha 1% kama ilivyo.

Kuna Mwanaume anaitwa Horatius, yeye alisimama katikati ya daraja peke yake dhidi ya jeshi zima.
Namaliza na alichokisema.
"To every man upon this earth Death cometh soon or late. And how can a man die better Than facing fearful odds, For the ashes of his fathers, And the temples of his Gods.”

Aisee ww jamaa noma mm nilishawah waza kujiua ila aisee mambo huwa yanatulia ish n subra tu na hakuna wakukusaidia hata mama mzaz utakufa peke ako kwenye shida
 
Changamoto sio kwako kaka sema tu wewe unahuzunika bure mkuu kwa sababu hujazoea hii hali, usije ukapanic kaka nakuambia tena wewe ni mgeni wa tatizo, uliishi vizuri, mshahara mzuri, nyumba nzuri, gari nzuri, kula na kuvaa pazuri, na sasa umerudi pabovu, hii hali hupata wengi hata mimi nishapitia hii hali, lakini tafuta fursa yoyote ya kupata kwanza mahitaji yako.

Alafu ukikaa kitaa utazoea tu ndio maana ya dunia kaka, kua uyaone kwani shida ni kipimo cha akili, unapitia kipindi cha kujifunza najua unajifunza sasa ulikosea wapi na kaa urekebishe, kama ni bahati mbaya pole na jipe moyo kupata vingine.

Nyumba si dhamana ya benki na dhamana yako ni mshahara kama walivyo eleza hapa una deadline ya muda kadhaa tafuta pesa kaka.
 
Yaani mkuu una mke na bado unakuwa depressed?
Sasa mkuu kama hujamshirikisha mkeo nashauri umshirikishe na umwambie kila kitu, mke ndio mtu pekee anayekujua vizuri na ndio mtu pekee atakayekupa faraja ya kweli kwenye nyakati ngumu za maisha ili upambane zaidi na hilo ndio dhumuni kuu la ndoa. na hapo ndipo nguvu ya mwanamke inapoonekana na hilo ndio lengo kuu la uwepo wa mwanamke duniani.

Lakini kwa kuwa umekuja huku kwa wanaume wenzako basi tambua tu utapata ukweli na uhalisia mchungu wa maisha, trust me niliwahi kuwa na matatizo makubwa tena ya kutisha ambayo yangekukuta wewe mkuu bila shaka ungekuwa kichaa. hayo yako ni madogo sana. tena mimi hakuna aliyenionea huruma wala kunisadia chochote hata pole na ikawa kama mimi ndio mwenye makosa wakati ni innocent lakini sikukaa chini kulialia na kuomba faraja NO. nilipigana kwa hasira na uchungu. I fought back even harder.

Naona unaomba neno la faraja, binafsi sikuonei huruma wala kukupa pole kama kila mtu anavyofanya au kukupa moyo kwamba mungu atakusaidia ili upate nguvu ya kupambana, sababu nguvu ya kupambana inatakiwa kutoka ndani ya mtu binafsi yeye mwenyewe na sio kwa watu wengine. wewe ulizaliwa peke yako na utakufa peke yako sasa vipi hawa watu wanaokupa pole na kukufariji sasa hivi wakiwa hawapo? utafanya nini? je utajiua? au utalia?

Sikuonei huruma sababu najua matatizo ni sehemu ya maisha na uchungu wa maisha ndio maana ya maisha na najua jinsi gani dunia ilivyo mbaya na katili na watu walivyo wabaya na wanafiki wenye dhuruma isiyoelezeka. ni Survival of the fittest, dhaifu watakanyagwa na wenye nguvu, na wenye nguvu pekee ndio watakaobaki.

Sasa nakwambia ukweli na uhalisa wa maisha man to man.
Ni kwamba mwanaume hakimbii matatizo wala kulialia na kujiua alafu kuacha familia yake iteketee peke yake.
Ni muoga, mpumbavu na mjinga pekee anayeweza kuchukua mtoto wa watu kutoka kwao kwenye maisha ambayo labda yalikuwa mazuri alafu kumzalisha watoto na kumpa mzigo mzito na yeye mwenyewe kujiua au kufa kwa depression na kuacha huyo mwanamke na maumivu makali na majuto juu yako, kitu kichungu zaidi ni kwamba bila shaka mkeo ataolewa tena na mwanaume mwingine ambaye atalea familia yako. je uko tayari kuona watoto wako na mkeo wakilelewa na mwanaume mwengine? mwanaume mwenzako?
Mimi sijui.

Kama ulikuwa unaona wewe hauna uwezo wa kujipambania na kumpambania huyo mwanamke basi usingemuoa ungesubiri kufa peke yako, lakini hapana, ulioa sababu uliamnini ungeweza kumuhudumia.
Sasa thibitisha hilo au kila nilichokiandika mimi hapa kitakuja kutokea kweli, na kwakua hatujuani basi tambua wala sikutanii mkuu.

Mwanaume anatakiwa kutokata tamaa na sio kulialia kwa kuomba faraja na kutaka huruma, anatakiwa kusimamia misimamo yake na kamwe isiyumbishwe wala kuvunjwa na yoyote yule. atapambana na kupigana mpaka tone la jasho la mwisho la ushindi.

Kaa chini fikiria kwa makini na ufanye unachoona kinafaa kwako na familia yako na kuwa tayari kupokea matokeo mabaya yasiyofurahisha. baba ndio tegemo la familia wewe ukiwa dhaifu je mkeo na wanao wawe vipi na wafanye nini?
Siku zote tambua maisha hayako fair na hakuna atakayekuonea huruma, matatizo yapo ili yatatuliwe na sio kuyakimbia au yatakukimbiza na kukumaliza wewe.

Binafsi sipendi kuomba ushauri wala sijawahi kuomba ushauri sababu ninakuwa na uhakika na maamuzi yangu siku zote na sitokubali mtu yoyote aniamulie au aniambie nini cha kufanya japo nitamsikiliza mama na mke wangu pekee kwa asilimia 1%, namaanisha 1% kama ilivyo.

Kuna Mwanaume anaitwa Horatius, yeye alisimama katikati ya daraja peke yake dhidi ya jeshi zima.
Namaliza na alichokisema.
"To every man upon this earth Death cometh soon or late. And how can a man die better Than facing fearful odds, For the ashes of his fathers, And the temples of his Gods.”
Huu ni zaidi ya ushauri.
Hata mimi umenisaidia.
 
Back
Top Bottom