Benson Mramba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 766
- 1,884
Kwa mtu aliye na rafiki yake nchi za nje sio Uganda wala Rwanda, au kama una mwanao ambaye ameshabalehe ukamwambia reforms ambazo Chadema wanataka na serikali haizitaki;
Kwanza atakuona fala wewe na wananchi wenzio wote.
Pili atashangaa mmeshirikije chaguzi zote zilizopita kwa tume ya namna hii na kwa mazingira haya ya uchaguzi.
Mwisho atajua viongozi wote wa nchi hii sio wa Chama tawala wala upinzani wamekuwa hawachaguliwi na wananchi bali wanawekwa na serikali.
Ndio maana wapo wapinzani wanapambana kushiriki uchaguzi huu wakijua watatengenezwa na mfumo kuwa vyama vikuu vya upinzani. Na wengine walishafanya udalali kwa ahadi ya serikali ya nusu mkate.
Derby ya leo aliyeshinda kashinda na aliyeshindwa kashindwa hakuna malalamiko wala vita wala fujo. Tufanye mabadiliko tusijifanye hatuelewi au kuona wanaoongozwa hamnazo.
Hata CCM wanataka mabadiliko. Bila chadema imara kwenye uchaguzi CCM mikoani, wilayani, kata na mashinani watakufa njaa. Hela watapataje? Wangojee miaka mitano mengine?
Zamani nikiwa kiongozi wa chadema kuna maeneo CCM walitulipia fomu na saa nyingine kutuazima wagombea na kufadhili mikutano upinzani uonekane una nguvu kwenye maeneo yao ili wapewe hela na chama za kupambana upinzani.
Uchaguzi ni biashara kubwa kwa taifa kuliko hata sikukuu ya sabasaba