Dereva Bodaboda auawa kwa kukatwa shingo na watu wasiojulikana Ushetu

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Dereva bodaboda Stefano Maziku (25), mkazi wa Kitongoji cha Igwesa, Kijiji cha Iboja, Kata ya Ukune wilaya ya kipolisi Ushetu mkoani Shinyanga, amekutwa ameuawa kisha mwili wake kutelekezwa na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Jeshi la Polisi linawasaka waliofanya kitendo hicho.

Kamanda Magomi amesema tukio hilo limetokea Novemba 16, 2025 na mwili ulikutwa na jeraha lililoashiria kukatwa na kitu kinachodhaniwa kuwa na ncha kali shingoni na kisha kutobolewa jicho la upande wa kushoto.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni kuwania mali kwani baada ya wahalifu kutekeleza tukio hilo walitoweka na pikipiki ya marehemu.

Amesema, "Kwa upelelezi wa awali, chanzo cha tukio ni kuwania mali, kwani baada ya tukio, walichukua pikipiki ya marehemu na kutokomea kusikojulikana."

Aidha Kamanda Magomi amewataka maofisa usafirishaji mkoani humo kuwa makini na watu wasiowajua wanaowakodisha hususani nyakati za usiku.
​
 
So sad 😭
Apumzike Kwa amani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…